Posts

Showing posts from September, 2023

KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA.

Image
  KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA. Boss! Siyo  kila mara, kusahau ni ishara ya Ubongo dhaifu, mara nyingi ni namna tunavyojifunza ndugu. Nimekutana na watu wengi wakisema: "Mimi sina akili kubwa." Wengine "Kumbukumbu yangu ni mbaya." Mara "Ubongo wangu hauhifadhi vitu." Lakini ukweli ni kwamba, mara nyingi tatizo si ukubwa wa akili yako wala uwezo wa ubongo wako. Tatizo ni kwamba watu wengi hawajawahi kufundishwa jinsi kumbukumbu (memory) inavyofanya kazi boss. Sikia ndugu; Ubongo wa binadamu umeumbwa kwa ustadi mkubwa. Kazi yake si kuhifadhi kila kitu unachokiona au kukisikia, bali ni kuchagua filtering taarifa muhimu na kuacha zisizo muhimu wala matumizi. Kwa hiyo, kusahau si kasoro ya ubongo ni sehemu ya kawaida ya jinsi unavyofanya kazi. Hebu tuangalie sababu kuu zinazowafanya watu kusahau mara kwa mara. 1. Kukariri Bila Kuelewa (memorising without understanding). Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo wanafunzi na hata watu wazima...

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA KUMI NA TANO.

Image
SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”.   SEHEMU YA KUMI NA TANO.  Ilipoishia... Usisogee maana hapo unaposogea ndipo nataka kudondokea kwahiyo pishaaa!!" Kabla hajayatafakari yale maneno yule mtu alijiachia makusudi kabisa na kujitupa chini. Elvine alishangaa zaidi. Alitaka kusogea ili akatoe msaada lakini yule mtu ghafla alipotea.         Elvine alipata hofu zaidi. Akakimbia mpaka chumbani kwake na akajihisi kabisa hadi ile kiu imekata. Lakini alipofika chumbani kwake alipigwa na butwaa kwa kile alichokuwa anakiona mbele yake na wala hakuamini kwa haraka.... Kusoma sehemu ya 14 bonyeza hapa Inaendelea...     Alipotazama kitandani kwake alimuona kijana yule aliyekuwa kaanguka mchana na ndiye aliyemuona kajiangusha muda sio mrefu kutoka kwenye ngazi tena akiwa anacheka sana.       "Kumbe ni wewe? Unajua nilikuwa najiuliza sana kuwa ni kijana yupi ambaye anakaa hapa na anauwezo wa kufanya mambo makubwa. Kwakwel...

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA KUMI NA TATU.

Image
  SIMULIZI YA KUFURAHISHA,   “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA KUMI NA TATU.     Ilipoishia..   Aligundua kuwa kumbe Elimina anamachungu sana moyoni mwake. Aliacha kumfokea na kuanza kumwomba msamaha huku akitamani kujua tatizo ni nini hasa. Wakati akiwa anambembeleza alikaa pembeni ya Elimina kwenye sofa huku akisema samahani. Ghafla mama aliingia na kushangaa kwa kile alichokiona "Nyie watoto ni upuuzi gani mnafanya hapo?....." kusoma sehemu ya kumi na mbili bofya hapa   Sasa inaendelea....   Elvine hawakujua wamjibi nini maana walijua kabisa mama atakuwa kaelewa kwa tofauti sana.     "Samahani mama sio kama unavyofikiria. Ni kwamba Elimina hajisikii vizuri. Na alikuwa akilia na mimi sijui shida ni nini na ndio maana nilitaka aniambie" Elvine alijaribu kujitetea       "Jiandaeni kwaajili ya kikao cha familia akija baba yenu" mama aliongea kwa mkato kisha akaondoka na kuelekea chumbani. ...

Popular posts from this blog