Posts

Showing posts from September, 2025

USIISHI TU ISHI KWA KUSUDI.

Image
  USIISHI TU ISHI KWA KUSUDI. Kuna watu wengi wanaamka kila siku, wanafanya kazi, wanatafuta pesa, wanapambana na maisha. Lakini ndani yao kuna swali ambalo bado halijajibiwa. Ambalo ni, “NIMEKUJA DUNIANI KUFANYA NINI?” Kwa sababu ukweli ni huu: sio kila mtu anayeishi anaelewa kusudi la maisha yake hapa duniani. Wengine wanafuata mkondo wa dunia. Wengine wanaiga maisha ya wengine. Wengine wanapoteza miaka mingi wakikimbiza vitu ambavyo havina maana ya kudumu. Lakini maisha hubadilika na kuwa na maana pale unapogundua kwa nini upo hapa duniani. Kusudi la maisha sio tu kupata pesa. Sio tu kuwa maarufu. Sio tu kumiliki vitu vingi. Wala si kuwa na kazi nyingi. Bali, Kusudi la maisha ni kugundua ZAWADI (uwezo, kipaji, karama, nguvu n.k) uliyopewa na Mungu. na kuitumia kuleta MWANGA(wepesi) katika maisha yako na maisha ya wengine. Ndiyo maana watu wanaoishi kwa kusudi huwa na nguvu tofauti. Changamoto zinakuja, lakini hawaachi kufanya. Wanakosolewa, lakini bado wanaende...

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31 Ilipoishia………. Elvine alipoteza amani kuliko hata mkewe maana kila alipomtazama mkewe basi moyo wake ni kama ulikuwa unachomwa na mwiba uliojishikiza huko kwenye mishipa ya moyo. Nafsi yake ilitaabika na ndipo alipoamua kutafuta muda mzuri, baada ya chakula cha jioni, azungumze na mkewe, maana ule ukimya wa siku mbili ulikuwa adhabu kubwa sana kwake. Kusoma sehemu ya 30 bonyeza hapa Sasa inaendelea………. Elimina mamy naomba kujua kwanini hutaki kuniuliza kuhusu sababu ya haya yote? Maana najua unajua kuwa kuna mahali mimi nilikosea, sasa unapokaa kimya hivyo… kiukweli unazidi kunichanganya maana ni kama hutaki kujua, sasa unadhani mimi roho yangu itatulia kweli?. Hata kama ungekuwa wewe lazima usingepata amani, ungekuwa hata unawaza hivi nakuwaziaje, nakuonaje na ninajisikiaje ninapokuona, sasa kwanini wewe umekaa kimya, sema neno tafadhali? (Elvine alikuwa akiongea bila kumtazama mkewe usoni maana moyo wake haukuwa katika hali ya utulivu). Pamoja na ...

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.