Posts

Showing posts from March, 2026

USIISHI TU ISHI KWA KUSUDI.

Image
  USIISHI TU ISHI KWA KUSUDI. Kuna watu wengi wanaamka kila siku, wanafanya kazi, wanatafuta pesa, wanapambana na maisha. Lakini ndani yao kuna swali ambalo bado halijajibiwa. Ambalo ni, “NIMEKUJA DUNIANI KUFANYA NINI?” Kwa sababu ukweli ni huu: sio kila mtu anayeishi anaelewa kusudi la maisha yake hapa duniani. Wengine wanafuata mkondo wa dunia. Wengine wanaiga maisha ya wengine. Wengine wanapoteza miaka mingi wakikimbiza vitu ambavyo havina maana ya kudumu. Lakini maisha hubadilika na kuwa na maana pale unapogundua kwa nini upo hapa duniani. Kusudi la maisha sio tu kupata pesa. Sio tu kuwa maarufu. Sio tu kumiliki vitu vingi. Wala si kuwa na kazi nyingi. Bali, Kusudi la maisha ni kugundua ZAWADI (uwezo, kipaji, karama, nguvu n.k) uliyopewa na Mungu. na kuitumia kuleta MWANGA(wepesi) katika maisha yako na maisha ya wengine. Ndiyo maana watu wanaoishi kwa kusudi huwa na nguvu tofauti. Changamoto zinakuja, lakini hawaachi kufanya. Wanakosolewa, lakini bado wanaende...

KUACHA URITHI.

Image
  #KUACHA #URITHI. Watu wengi wanaishi wakifikiria leo tu. Lakini wachache wanaishi wakijenga urithi wa kesho. Ukweli ni huu ; Maisha ya mtu hayapimwi tu kwa muda aliokaa duniani, bali kwa athari na alama  aliyoiacha katika maisha ya wengine. Wengine wanaacha majumba. Wengine wanaacha mali. Wengine wanacha mashamba. Wengine wanaacha Magari. Na hilo ni jambo jema, na ni urithi mzuri. Lakini kuna urithi mkubwa zaidi kuliko mali. Urithi wa maadili. Urithi wa maneno ya kutia moyo. Urithi wa mfano wa maisha uliouonyesha. Urithi wa mifumo na mienendo ya maisha. Kuna mtu leo anapigana vita za maisha kwa ujasiri kwa sababu kuna mtu aliwahi kumwambia, “USIKATE TAMAA.” Kuna mtoto anajua KUHESHIMU kwa sababu kuna mtu aliwahi kumfundisha heshima. kuna mtu anajali #thamani na #utu wa watu sababu kuna mtu amewahi kumfundisha hivyo. Maneno madogo yanaweza kujenga maisha na HATIMA ya mtu. Na vitendo vidogo vinaweza kubadilisha #KIZAZI kizima. Ndiyo maana maisha hayapaswi kuishi ishi tu. yanap...

KUJILINGANISHA NI SUMU HATARI.

Image
  KUJILINGANISHA NI SUMU HATARI. Tatizo kubwa la kizazi hiki si kukosa UWEZO binafsi. Bali ni KUJILINGANISHA kupita kiasi. Hebu tazama kwa mfano, nafungua simu yako, unaona maisha ya wengine, yanaonekana yamepangwa. Wamefanikiwa. Wanasafiri. Wanaonekana kuwa na furaha sana. Wanavaa na kula vizuri. Halafu unaanza kujiuliza: “Mimi niko wapi?” mara unasema mimi si chochote. Mdogo mdogo, unajikuta unapima thamani yako kwa vipimo vya watu wengine. Hapo ndipo tatizo linapo anzia. Lakini ukweli ni huu;  👉 kila mtu ana safari yake, kila mtu anasababu yake. Ambayo yaweza kuwa nitofauti kabisa na wengine. Kuna anayekimbia haraka kwa sababu alianza mapema. Kuna anayepanda polepole kwa sababu anajenga msingi imara. Kuna anayeficha mapambano yake nyuma ya picha nzuri. Usilinganishe mwanzo wako na mwisho wa mtu mwingine. Si unajua maisha ni kama kitabu, ukurasa wako wa kwanza una weza kuwa ni wa mwisho kwa mwingine. Kila mtu anakitabu chake na kurasa zake. Maisha yako hayakuitwa KUIGA watu...

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.