P5. SABABU YA MAISHA YAKO KUBADILIKA AU KUHARIBIKA INAWEZA KUWA MAZINGIRA YAKO.

Image
  P5. SABABU YA MAISHA YAKO KUBADILIKA AU KUHARIBIKA INAWEZA KUWA MAZINGIRA YAKO. Self-awareness haiishi ndani yako  peke yako. Sehemu muhimu ya kujitambua ni kuelewa jinsi unavyoathiriwa na wengine na mazingira yanayokuzunguka, na pia jinsi unavyowaathiri wengine/ mazingira yako. Hii inaitwa Social & Environmental Awareness au Reciprocal Influence boss. 1. JINSI UNAVYOATHIRIWA NA WENGINE NA MAZINGIRA (Incoming Influence). Wewe ni kamq kisiwa,  ambapo kila siku, mazingira na watu  wengine wanaingiza: mawazo, mitazamo, hisia na tabia mbali mbali ndani yako. Wakati mwengine bila hata wewe kujua. Kwa mfano: Watu (Social Influence): Marafiki au jamaa wanaweza kukufanya uone shaka, hofu, au kuacha jambo muhimu sana maishani. Na Ukiwa na watu wenye nidhamu na maono, unachukua tabia zao mfano kuamka mapema, kupanga bajeti, au kufanya mazoezi. Unaishi Mazingira (Environmental Influence): Mazingira yenye kelele, vurugu, au tabia zisizo za tija huathiri mood na ...

MAWAZO YAKO SIYO WEWE.

 


MAWAZO YAKO SIYO WEWE.

Hebu, Kaa kimya kidogo ujiulize na mimi,
Ni mara ngapi umejisikia vibaya si kwa sababu ya kile kilichotokea, bali kwa sababu ya kile akili yako ilikuambia?
Yaani, Nimefeli, Watanicheka, Mimi sifai wakati mwingine unajiambia ushindi n.k

Siyo wewe pekee yako, sauti hii ipo kwa kila mtu.
Lakini hapa ndipo watu wengi wanakosea:
Wanadhani hiyo sauti ni  WAO.
๐Ÿ“˜ Kutoka kwenye The Untethered Soul, kuna ukweli mmoja rahisi lakini wenye nguvu:
๐Ÿ‘‰ Kama unaweza kusikia mawazo yako, basi wewe si hayo mawazo.
Hii inamaanisha kuwa, kuna vitu viwili ndani yako:
1. Mawazo —hii ni nishati inayozunguka huku nakule, na yanakuja na kuondoka kila wakati hayakae kwako milele.

2. Wewe — unayeyaona hayo mawazo
๐Ÿ‘‰ Wewe ni “mtazamaji/observer”, si hiyo “sauti”
Hebu Fikiria hivi:
Akili yako ni kama redio ๐Ÿ“ป inayoongea bila kupumnzika(nonstop).
Wakati mwingine inasema ukweli,
lakini mara nyingi:
inaogopa, na mawazo yako yanacomment kila kitu, yanadrama etc.
inazidisha na kukuza mambo,
inakuambia hadithi zisizo na uhakika.

๐Ÿ‘‰ Sasa jiulize: Je, kila kitu kinachosemwa kwenye redio ni lazima kiwe kweli?
Tatizo haliko kwenye kuwa na mawazo. Lakini,
Tatizo ni kuyaamini kama ukweli bila kuyachunguza.

Goja nikwambie, Wazo moja linaweza kubadilisha hali yako yote:
Mfano wazolinasema “Sitafanikiwa”
→ unakata tamaa
→ unaacha kujaribu
Lakini ukweli ni huu:
๐Ÿ‘‰ Hilo lilikuwa wazo tu, si ukweli. Shida ni kwamba umelichukua na kuliamini moja kwa moja.
Wakati mwingine mimi huwa nasema, Mawazo ni kama mawingu:
yanakuja, yanapita, hayakai milele
Lakini wewe ni kama anga.
๐Ÿ‘‰ Hubadiliki kwa sababu ya wingu kupita.

Sasa, nini cha kufanya?
Jaribu kufanya hivi, kila siku:
✔️ Tambua – “hili ni wazo, na wala si mimi”
✔️ Angalia – usikimbilie kuliamini moja kwa moja lichunguze kwanza.
✔️ Usishike – usiliweke moyoni hadi uwe umejiridhisha nalo.
✔️ Achia – kama utalipima nakuona kuwa halina manufaa liache lipite.
๐Ÿ‘‰ Hii ndiyo njia muhimu ya kujikomboa.

Vile vile katika, hisia kama,
Hasira. Hofu. Huzuni.
Hizi si adui zako , lakini pia,
๐Ÿ‘‰ Ni nishati inayopita ndani yako.
Tatizo linaanza pale unapofanya:
kuzing'ang'ania au kuzishikilia sana.
Hapo ndipo zinakaa ndani na kukuumiza, si unajua vizuri maswala ya nishati boss.

Ukweli ni kwamba, Ukijifunza:
kutotawaliwa na mawazo
kutoshikilia hisia
๐Ÿ‘‰ unapata kitu ambacho watu wengi wanakitafuta maisha yao yote:
uhuru wa ndani the inner peace.

Sasq basi,  Kuanzia leo:
Usiamini kila kitu unachofikiria.
Usikimbie kila hisia unayohisi.
๐Ÿ‘‰ Angalia. Tambua. Achia.
Hapo ndipo maisha halisi yanaanza.

Je katika maisha yako kuna hisia au mawazo yeyote uliyoyabakiza huenda ulitakiwa kuyaachia yapite?

Share na na mimi kupitia comment. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.

Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697.


Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29