NGUVU YA TATHMINI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAKO.

Image
  NGUVU YA TATHMINI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAKO. Kuna jambo moja muhimu sana katika safari ya mafanikio ambalo watu wengi hulipuuzia, lakini lina uwezo mkubwa wa kubadilisha kabisa mwelekeo wa maisha ya mtu yeyote. Jambo hilo si lingine bali ni TATHMINI. Ndiyo tathmini boss. Boss in short tathmini ni uwezo wa kusimama kwa muda, kuangalia ulipotoka, ulipo sasa hivi, na kule unakoelekea. Yaani ni sawa na kujiuliza hivi; Je, njia ninayotumia inanifikisha ninapotaka kwenda? Nimefanikiwa kwa kiwango gani? Nimekosea wapi? Nini kimefanya mambo yasiende kama nilivyopanga? Nifanye nini tofauti ili kupata matokeo bora zaidi? Kwa sababu huwezi kuboresha kitu ambacho hukijui wala hujakipima boss. Ndugu, TATHMINI SI KUSHINDWA HII NI HEKIMA Watu wengi wakiona mipango yao haijafanikiwa haraka huamua kuiacha na kuibwaga ghafla tu. Kibaya zaidi wengine huanza kulaumu: mazingira, watu wengine, bahati, hali ya maisha au kujilaumu wao wenyewe. Lakini mtu mwenye hekima hufanya kitu cha to...

KUACHA URITHI.

 


#KUACHA #URITHI.

Watu wengi wanaishi wakifikiria leo tu.

Lakini wachache wanaishi wakijenga urithi wa kesho.

Ukweli ni huu ;

Maisha ya mtu hayapimwi tu kwa muda aliokaa duniani,

bali kwa athari na alama  aliyoiacha katika maisha ya wengine.


Wengine wanaacha majumba.

Wengine wanaacha mali.

Wengine wanacha mashamba.

Wengine wanaacha Magari.

Na hilo ni jambo jema, na ni urithi mzuri.


Lakini kuna urithi mkubwa zaidi kuliko mali.

Urithi wa maadili.

Urithi wa maneno ya kutia moyo.

Urithi wa mfano wa maisha uliouonyesha.

Urithi wa mifumo na mienendo ya maisha.


Kuna mtu leo anapigana vita za maisha kwa ujasiri kwa sababu kuna mtu aliwahi kumwambia, “USIKATE TAMAA.”

Kuna mtoto anajua KUHESHIMU kwa sababu kuna mtu aliwahi kumfundisha heshima. kuna mtu anajali #thamani na #utu wa watu sababu kuna mtu amewahi kumfundisha hivyo.


Maneno madogo yanaweza kujenga maisha na HATIMA ya mtu.

Na vitendo vidogo vinaweza kubadilisha #KIZAZI kizima.

Ndiyo maana maisha hayapaswi kuishi ishi tu.

yanapaswa kuishi kwa KUSUDI.


Jiulize kwa utulivu mkubwa:

Kama siku moja nitaondoka duniani, nitakuwa nimeacha nini nyuma yangu?


Kwa sababu mwisho wa siku,

mali inaweza kuisha. Vile vile pesa, majumba, magari vinaweza kuhàribika.


Lakini MOYO ULIOGUSA maisha ya watu,

MAADILI uliyopanda ndani ya wengine,

na MWANGA uliowasha katika maisha yao.

NJIA NA UJASIRI ulio upanda katikati yao.


vinaweza kuendelea kuishi hata baada yako.

Usiishi tu kupita duniani.

Ishi ukiacha kitu kitakachoendelea kuzungumza hata baada yako.


Hebu wajengee urithi wa kudumu watoto wako,  wafundishe nidhamu, wafundishe mifumo ya maisha, wafundishe kujitegemea, wafundishe nidhamu ya pesa, kutatua matatito, kufikiria, kujiamini, kujali kazi na utu,  wafundishe uongozi na mambo mengine kama hayo.

Wakumbuke hata watu, kama akina Mwl. Nyerere,  Mandela, mahathima, Magufuli n.k

Bado wanaishi wangali hawapo.

Huo ndiyo urithi wa kweli. 🔥

Kama umejifunza kitu tuambie kisha share ujumbe huu kwa uwapendao.

Migongo Elias 

Add Value Network 

#seeyounextlevel 

#knowledgeispower

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29