Posts

KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA.

Image
  KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA. Boss! Siyo  kila mara, kusahau ni ishara ya Ubongo dhaifu, mara nyingi ni namna tunavyojifunza ndugu. Nimekutana na watu wengi wakisema: "Mimi sina akili kubwa." Wengine "Kumbukumbu yangu ni mbaya." Mara "Ubongo wangu hauhifadhi vitu." Lakini ukweli ni kwamba, mara nyingi tatizo si ukubwa wa akili yako wala uwezo wa ubongo wako. Tatizo ni kwamba watu wengi hawajawahi kufundishwa jinsi kumbukumbu (memory) inavyofanya kazi boss. Sikia ndugu; Ubongo wa binadamu umeumbwa kwa ustadi mkubwa. Kazi yake si kuhifadhi kila kitu unachokiona au kukisikia, bali ni kuchagua filtering taarifa muhimu na kuacha zisizo muhimu wala matumizi. Kwa hiyo, kusahau si kasoro ya ubongo ni sehemu ya kawaida ya jinsi unavyofanya kazi. Hebu tuangalie sababu kuu zinazowafanya watu kusahau mara kwa mara. 1. Kukariri Bila Kuelewa (memorising without understanding). Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo wanafunzi na hata watu wazima...

JE MAARIFA YANAKUIMARISHA AU YANAKUHARIBU?

Image
JE MAARIFA YANA KUIMARISHA AU YANA KUHARIBU? “Learning makes a wise wiser and a fool more foolish” . Huu ni moja kati ya semi ninazozipenda sana, sababu umebeba uhalisia fulani hivi kwa namna ambavyo dunia ya sasa inaenenda. Hebu ngoja tuone maana yake kwanza ambayo ni kwamba “kujifunza kunamfanya mtu mwenye hekima kuwa na hekima Zaidi na mjinga kuwa mjinga Zaidi ”. Ukweli huu nauunga mkono kwa 100% kabisa nadhani hata wewe utakuja kuungana na mimi katika hili hapo baadaye. Na Mara, utakapo maliza kusoma andiko hili hutabaki kama ulivyo. Hivi ulishawahi kuona mtu wa namna hii? Kwamba kabla ya kwenda shule tuseme labda sekondari au chuo alikuwa na nidhamu, heshima, maadili, utii, kufanya kazi kwa bidii, uzalendao, tabia njema na alikuwa mfano wa kuigwa katika jamii. Lakini mara baada tu! Ya kwenda shule au chuo mambo yanabadilika kabisa na kuwa tofauti na vile alivyokuwa mwanzo, utashangaa anaanza kuwa mkaidi, tabia mbaya kama vile uraibu wa pombe, umalaya , anapoteza uaminifu n.k. ya...

SABABU 5 KWANINI WATU WANASHINDWA KUTEKELEZA MIKAKATI WALIYO JIWEKEA?

Image
SABABU 5 KWANINI WATU WANASHINDWA KUTEKELEZA MIKAKATI WALIYO JIWEKEA? Siku moja nilikuwa naongea na mtu mmoja. Katika mazungumzo yetu, ambayo, yalitumia muda mrefu kidogo. Kimya kilitawala muda kuashiria kuwa mada zimeisha na kusubiri mada yingine mezani. Baadaye, nilichomekea swali na kumuuliza kuhusu mipango yake ya maisha ndani ya mwaka tuliokuwa tumeuanza maana ilikuwa ni mwanzoni kabisa mwa mwaka 2022. Naye alijibu akanieleza mipango na mikakati yake ambayo alipanga kuitekeleza ndani ya mwaka mmoja . Ukweli nilimpenda bure, kwa namna ambayo alikuwa ameandaa mipango na mikakati ya kuukabili mwaka huo mpya. Kwa mipango ile mtu yeyote angeweza kutoboa kama angeifanyia kazi. Kwa kufupisha sana nilimpongeza na kumtakia utekelezaji mwema ndani ya huo mwaka. Niseme tu kuwa, saa zilienda,siku zikaenda, wiki ndo usiseme na miezi ilikatika hadi mwaka ukaelekea ukingoni. Nilipo kutananaye nikamuuliza vipi rafiki umefikia wapi, akajibu akasema, we acha tu! Mambo yaliingiliana na mipango ika...

NJIA 7 ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

Image
  NJIA ZA KUOSHA UBONGO WAKO. Hivi ulisha wahi kwenda hospitali na kupata ushauri wa daktari juu ya afya ya mwili wako? Au basi ulisha wahi kumsikia mtu yeyoye pengine rafiki, ndugu, mke, kaka yako au mtu yeyote akisimulia kuhusu ushauri wa daktari katika kutunza na kuimarisha afya ya mwili wake?  Bila shaka ulisha wahi na kama bado usihamaki, kwani utaelewa tu.  Ukweli ni kwamba mara nyingi watu wamekuwa na utaratibu wa kwenda hospitali kwaajili ya afya za miili yao na hapo watapewa dawa za kutosha, ili kujiponya na malazi yanayo wasibu.  Na mara nyingi hupewa dawa za kutumia, wengine huchomwa   sindano, wengine kupewa masharti ya namna ya kutumia dawa hizo wengine huambiwa kula baadhi ya vyakula wengine mazoezi n.k Kwa kawaida mwanadamu ameundwa na sehemu kuu mbili, nazo ni utu wa nje na utu wa ndani .  Utu wa nje ndio huu mwili ambao unashikika yaani, huu mwili wa damu na nyama.  Ili kuuimarisha mwili huu wanadamu wamekuwa wakifanya vitu kama ma...

KANUNI MAKINI YA KUPAMBANIA NDOTO YAKO:

Image
                      KANUNI MAKINI YA KUPAMBANIA NDOTO YAKO: Kuna njia nyingi sana tumeambiwa na kufundishwa kwa namna tofautitofauti sana ilikupambana na maisha yetu hasa katika kuyafikia malengo na mafanikio yetu.na kwa bahati nzuri au mbaya njia hizo zimekuwa zikiwasaidia wengi na wengine kuwahalibia kabisa na wengine kuwaboresha huku wengine zikiwabomoa kabisa .kiuhalisia hakuna njia ambayo imethibitishwa na kutumika kuwa ni njia bora kwa 100% ambayo inaleta mafanikio kwa watu wote kwa kweli bado sijaona.kwasababu njia ambayo ilimfanikisha John akiitumia Anna kwa namna ileile inaweza kumfilisi na kumharibia kabisa,njia iliyo mfilisi Huyu ndiyo itakayo mfanikisha yule.Unaweza ukaambiwa   weka malengo,amka mapema ,weka vipa umbele,fanya kazi kwa bidii,fanya mambo kwa utofauti,fanya kwa ubora,jifunze vitu vipya kila siku ,ajabu ni kwamba unaweza kufanya yote hayo na ukapata matokeo tofauti kabisa na ulivyo tarajia sababu zi...

JINSI YA KUSEMA UKWELI NA KUWA MWAMINIFU

Siku Moja nilikuwa katika pitapita zangu nikasikia mtu akisema siku hizi kumpata mtu mkweli haiwezekani. Nilipouliza kinagaubaga akasema watu ni waongo sana, hakuna anayeweza kuongea ukweli wakati Wote na Uongo umekuwa ni sehemu ya Maisha yetu. Na akachimba zaidi akasema kama utachagua kuwa mkweli itakubidi utafute kadunia Kako ukaishi kivyako huko. Ni kama kuna kaukweli Fulani hivi ukiangalia kadiri siku zinavyozidi kwenda watu wanazidi kupoteza UKWELI na UAMINIFU. Utashangaa mtu unamuuliza umefika wapi nipo hapa corner nakuja chapu,unakaa saa za kutosha hata hatokei kumbe bado yupo nyumbani kabisa.Mwingine anakwambia tutakutana saa 4:00 afu haonekani kabisa, mwingine anaenda kutoa sadaka hewa ili aonekane ametoa, yaani uongo umetapakaa Kila mahali UAMINIFU umekuwa bidhaa adimu sana. UKWELI umefichika umekuwa wa kumlika na tochi. kuwaridhisha na kujionyesha kwa wengine ni moja ya kitu kinachopelekea kusambaa na kuenea kwa uongo kuliko UKWELI. Hiki kitu kimekuwa ni kilio Cha wengi sana...

TATUA TATIZO LOLOTE UNALOPITIA KWA NJIA HIZI!

Image
  TATUA TATIZO LOLOTE KWA NJIA HIZI! Siku zote ukiishi katika dunia hii kila kukicha utakutanana na migogoro na matatizo ya kutosha.Yaani, ukikwepa upande huu utakutananayo tu upande wa pili. Kumbe matatizo katika dunia hii ni sehemu ya maisha. watu wengi hawakubaliani na ukweli huu matokeo yake matatizo yamekuwa yakiwashangaza kila leo. Nimewahi kukutana na usemi mmoja ambao sina budi kukujuza nawewe leo. Nao ni huu “ kuishi duniani huku ukitegemea kuishi bila matatizo ni chanzo cha matatizo yote. ”, kuna watu wana amini kuwa wao hawajaumbwa kukutana na matatizo yeyote hapa duniani, hapo utakuta mtu anasema  “ hivi kwanini mimi tu Mungu yanipate haya ”. Ajabu kweli yaani matatizo anataka yawapate watu wengine tu ila yeye hapana, ndugu ilihali unakaa kwa hii dunia hiki kitu ni ngumu kukikwepa asee . Ndugu yangu kama unakaa kwenye hii dunia matatizo yatakuja tu aidha upende au usipende, uwe mwema au mbaya kiasi gani ,mcha Mungu au muovu kiasi gani, uwe tajiri au uwe masikin...

SAMEHE KWA FAIDA YAKO MWENYEWE!.

Image
    SAMEHE KWA FAIDA YAKO MWENYEWE. Mtu mmoja alisikika akisema nimekusamehe lakini sitakusahau katika maisha yangu kwa hichi ulicho nitendea! Kama utakuwa mfuatariaji na mdadsi wa mambo na watu utagundua kuwa suala la kusamehe limekuwa ni changamoto kubwa sana kwa watu wengi. Wengi wamebaki na vinyongo, visasi, machungu, na hasira kupita kiasi kuhusu ulio   wakosea au kutokuwasamehe. Mwalimu mmoja aliwaagiza wanafunzi wake kila mmoja aje na nyanya kulingana na idadi ya watu anaowachukia. Wanafunzi walikuja nazo siku iliyofuata, wengine walikuja na nyanya moja, wengine mbili, wengine tano, na wengine nyanya za kutosha   na walipo kuja nazo aliwaambia waandike  majina ya watu wanaowachukia ko, waziache kwenye mikoba yao na mwalimu aliwaambia watakuwa wanakuja nazo kila siku bila  kuzitupa au kuziacha. Baada ya siku kadhaa wanafunzi walianza kulalamika kuwa mzigo umekuwa mzito na umekuwa ni ngumu kuja nao kwani zilikuwa zimeshaanza kuoza na kunuka hivy...

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

LEVEL ZA MAFANIKIO SEHEMU YA KWANZA.

MISINGI YA UWEKEZAJI SEHEMU YA PILI..