MAAJABU YA AKIBA

JIFUNZE KUJIFUNZA PART VIII.
KANUNI ZINAZOENDESHA KUMBUKUMBU NDANI YA AKILI YAKO.
Ndugu msomaji u hali gani! Bila sha haujambo na unaendelea vyema, na kama si hivyo Mungu akupe
wepesi katika hilo. Kama utakuwa unafuatilia somo hili la jifunze kujifunza utakumbuka
kuwa tuliishia part vii huko tumejifunza
mambo kibao na kama hujasoma au
kufuatilia sehemu zilizopita ni wazi kuwa kuna vitu umekosa. Lakini habari njema
kwako ni kuwa kupitia hapa hapa addvaluenetwork unakwenda
kuyapata masomo yaliyopita hivyo fuatilia kupitia linki hapo chini.
Kama ilivyo kwa bank kuhifadhi pesa, ghala kuhifadhi
chakula, tank kuhifadhi maji, mtungi kuhifadhi gasi, zizi kuhifadhi mifugo,
nyumba kuhifadhi watu na mali zao, flash kuhifadhi taarifa, ndivyo ilivyo kwa
akili kuwa na MEMORY ya kuhifadhi taarifa na michakato mingine ndani ya ubongo wa mwanadamu. Niseme tu kuwa hii
ndiyo sehemu ambayo inatunza na kuhifadhi kumbukumbu zako, watu hukumbuka
matukio mbali mbali yaliyotokea muda mfupi au mrefu kutokana na kuwepo kwa sehemu
hii.
Zipo sheria na kanunia ambazo zinaendesha na kuongoza
memory katika kukumbuka na kuhifadhi
taarifa. Haijarishi ni kwa namna gani utakumbuka lakini, linapokuja suala la
namna memory yako inavyofanya kazi huwa kuna sheria na kanuni kadhaa
zinazoongoza memory yako katika kukumbuka. Hivyo hapa tunakwenda kuangalia kanuni
hizo, fuatana nami;
..............................................................
Hukumbuka kwa haraka kitu cha kwanza na cha
mwisho kuingia; Hiii wakati mwingine wazungu huiita primacy
and recency effect. Ambapo mtu hukumbuka kwa haraka
kitu cha kwanza na cha mwisho kuingia ndani yake, na ndiyo maana kama
utakumbuka somo la pili tuliaangalia wakati gani mzuri wa kuiamru akili yako na
tukaona kuwa ni wakati wa kwenda kulala au baada ya kuamka, kwasababu wakati huo
subconscious mind huwa iko makini kupokea taarifa. Hali hii huchangiwa na namna
memory yako inavyofanya kazi. Hata katika vikao ni rahisi kumbuka namna mlivyoanza kikao na namna kikao
kilivyo malizika, au namna muhubiri alivyoaanza kuhubiri na namna alivyomaliza
ni rahisi sana kukumbuka nyakati hizi mbili kuliko zingine, hii ni kutokana na
kanuni hii. Sijui kama unanipata.
..............................................................
Kama itapata mifumo (patterns) na miunganiko
(connections) ya vitu ni rahisi kuvikumbuka; Kama
utakumbuka katika sehemu ya tano tulizungumza kuhusu mifumo na miunganiko hii katika ufanyaji kazi wa
akili ya mwadamu, ambayo hufanya miunganiko na mifumo kama
njia ya kupita hata unapojifunza kitu kipya
hutengeneza njia na hupita katika njia ziyo. Hivi ulisha wahi kukutana na
mtu ambaye umemsahau jina lake? Hapo utashangaa utaanza kuvuta kumbukumbu na
kujiuliza hivi ulikutana naye wapi kwa mara ya kwanza? Alikuwa na nani? Alikwambia
anaitwa nani? Pengine ukikumbuka tu kuwa mlikutanaye kwenye tukio fulani, na
alikuwa na mtu fulani pengine utajikuta umemkumbuka tayari hadi jina lake. Ipo mifano
mingi sana kuitaja yote muda hautoshi lakini nadhani umepata picha.
..............................................................
Hukumbuka vitu ambavyo vilikushangaza au vipo
tofauti na mifumo au miunganiko ya akili;
katika kuvuta kumbukumbu
akili yako hukumbuka kwa wepesi vitu ambavyo hutokea kwa kushangaza na venye
utofauti kwenye kundi husika. Hebu jiulize kwamfano ukiwa katika kikao watu
wanasimama kawaida tu na kutoa hija zao, lakini akatokea mmoja akasimama na
kupita mbele huku akitoa hoja zake. Au kwenye
kundi utakuta kuna waafrika 50 na mzungu mmoja ni rahisi sana kukumbuka habari
za mzungu huyo hata siku nyingi zikipita kwasababu ya utofauti wake. Au watu wote
wanafanya biashara moja lakini akatokea mtu mmoja akaanzisha biashara yake tofauti
na wengi, mtu huyu ni rahisi sana kufahamika kwa sababu ya utofauti wake. Hapa kunajambo
la kujifunza kuwa ukitaka kuwa mtu wa tofauti lazima
ukubali kufanya vitu vya tofauti.
..............................................................
Uwezo wako wa kukumbuka huimarika kutokana na kujikumbusha vitu ulivyojifunza; kama utakumbuka kwa habari ya REPEATITION kama moja ya silaha za kupandikiza maneno ndani
ya subconscious mind kama hujasoma rudi kapitie kufuata linki hapo juu. Nasema kwamba
kadiri kitu unapokifanya kwa kurudia rudia kwa muda mrefu hugeuka na kuwa tabia.
Hivyo hata katika kumbu kumbu memory yako hukumbuka kitu ambacho unakifanya
mara kwa mara. Wakati mwingine kadiri unavyofanya mazoezi ndivyo unavyo zidi
kuimarika na kuwa imara zaidi. Au hujasikia wahenga walivyosema kuwa “Practice makes improvement”, kujifunza pekee yake
hakutoshi bali inahitajika kufanyia kazi
au mazoezi kwa kile ulichojifunza. kwani kadiri unavyojifunza na kufanyia kazi kile
ulichojifunza ndivyo utakavyokuwa nguli katika eneo husika. Si unajua
kujifunza ni hitaji la chini sana katika mafanikio kwenye eneo lolote lile eeh!
Hivyo iwe katika kazi yako yeyote ile ongeza maarifa hutabaki kama ulivyo.
..............................................................
Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza
kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya
kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia
mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT
lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS
Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na
Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluenetwork. Karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>> Migongoe.
Instagram>> migongo_elias.
Pinterest>> eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi
kujifunza pamoja nawe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Gody · 88 weeks ago
Migongo 9p · 88 weeks ago
MARCO JINAYI · 88 weeks ago
Elias · 88 weeks ago