KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA.

Image
  KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA. Boss! Siyo  kila mara, kusahau ni ishara ya Ubongo dhaifu, mara nyingi ni namna tunavyojifunza ndugu. Nimekutana na watu wengi wakisema: "Mimi sina akili kubwa." Wengine "Kumbukumbu yangu ni mbaya." Mara "Ubongo wangu hauhifadhi vitu." Lakini ukweli ni kwamba, mara nyingi tatizo si ukubwa wa akili yako wala uwezo wa ubongo wako. Tatizo ni kwamba watu wengi hawajawahi kufundishwa jinsi kumbukumbu (memory) inavyofanya kazi boss. Sikia ndugu; Ubongo wa binadamu umeumbwa kwa ustadi mkubwa. Kazi yake si kuhifadhi kila kitu unachokiona au kukisikia, bali ni kuchagua filtering taarifa muhimu na kuacha zisizo muhimu wala matumizi. Kwa hiyo, kusahau si kasoro ya ubongo ni sehemu ya kawaida ya jinsi unavyofanya kazi. Hebu tuangalie sababu kuu zinazowafanya watu kusahau mara kwa mara. 1. Kukariri Bila Kuelewa (memorising without understanding). Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo wanafunzi na hata watu wazima...

HUWEZI KUBADILIKA BILA KUJITAMBUA.


HUWEZI KUBADILIKA BILA KUJITAMBUA.

Watu wengi hutamani kubadilisha maisha ya tabia, kipato, mahusiano, au jinsi wanavyojiona. Wengine husoma vitabu, huhudhuria semina, na kuweka malengo mapya kila mwaka. Lakini, pamoja na juhudi zote hizo, hujikuta wakirudia hali ileile.

Sababu si kukosa bidii, no. Mara nyingi ni kukosa #KUJIJUA wao kama wao.

Kujiboresha bila kujitambua ni kama kujenga bila ramani.

Unapojaribu kubadilika bila kuelewa wewe ni nani, unaishia kuiga maisha ya wengine tu. Utaweka malengo yasiyoendana na hali yako, uwezo wako, au hali yako ya ndani.

Ndiyo maana baadhi ya malengo huonekana mazuri kwa macho ya watu, lakini moyoni hayana uzito wowote. Unapoanza kuchoka haraka, si uvivu tu, wakati mwingine ni ishara kwamba njia uliyopo siyo yako.

Kujitambua kunahitaji ujasiri wa kukubali ukweli kuhusu wewe.

#Kujitambua siyo kujipongeza kila wakati. Ni kukubali ukweli wote mtamu na mchungu.

Ni kuona #NGUVU zako bila kiburi, na #UDHAIFU wako bila kujilaumu. 

Ni kujiuliza maswali magumu kama: Mimi ni nani? Ninakwenda wapi? Kwa nini narudia makosa yaleyale? au Ni hofu gani inaniongoza bila kujua?

Huwezi kurekebisha kile ambacho hujakikubali.

Kujitambua huzaa mabadiliko ya kudumu

Unapojifahamu, maamuzi yako yanabadilika. Unaacha kuishi kwa mazoea na kuanza kuishi kwa #MAKUSUDI.

Unaacha kuhiuliza, “Watu watasemaje?” na kuanza kuuliza, “Hili linaendana na mimi?”

Mabadiliko yanayotokana na #SAUTI na #UELEWAwa ndani hudumu kwa sababu yanajengwa juu ya #UKWELI, si msukumo wa muda mfupi tu!.

Namaliza kwa kusema,

Kama kweli unataka kubadilika na kubadilisha chochote kwenye maisha yako, anza kwa kujifahamu wewe kwanza. Kaa kimya mara kwa mara tafakari, jisikilize kitokea ndani yako, na ukubali ukweli wako bila #KUHOFIA WALA #KUKIMBIA.


Kujitambua si mwisho wa #SAFARI—ni mwanzo wa #MABADILIKO ya #KWELI. Chukua muda mchache ujiulize swali hili:

Ni eneo gani la maisha yangu najidanganya

 mwenyewee na ninahitaji mabadiliko gani?


Add Value Network 

Migongo Elias 

#SeeYouNextLevel

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31