NGUVU YA TATHMINI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAKO.

Image
  NGUVU YA TATHMINI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAKO. Kuna jambo moja muhimu sana katika safari ya mafanikio ambalo watu wengi hulipuuzia, lakini lina uwezo mkubwa wa kubadilisha kabisa mwelekeo wa maisha ya mtu yeyote. Jambo hilo si lingine bali ni TATHMINI. Ndiyo tathmini boss. Boss in short tathmini ni uwezo wa kusimama kwa muda, kuangalia ulipotoka, ulipo sasa hivi, na kule unakoelekea. Yaani ni sawa na kujiuliza hivi; Je, njia ninayotumia inanifikisha ninapotaka kwenda? Nimefanikiwa kwa kiwango gani? Nimekosea wapi? Nini kimefanya mambo yasiende kama nilivyopanga? Nifanye nini tofauti ili kupata matokeo bora zaidi? Kwa sababu huwezi kuboresha kitu ambacho hukijui wala hujakipima boss. Ndugu, TATHMINI SI KUSHINDWA HII NI HEKIMA Watu wengi wakiona mipango yao haijafanikiwa haraka huamua kuiacha na kuibwaga ghafla tu. Kibaya zaidi wengine huanza kulaumu: mazingira, watu wengine, bahati, hali ya maisha au kujilaumu wao wenyewe. Lakini mtu mwenye hekima hufanya kitu cha to...

UFUNGUO WA KUJIFUNGULIA MAISHA YAKO.



UFUNGUO WA KUJIFUNGULIA MAISHA YAKO.

Mara nyingi sana watu hulichukulia swala la kujitambua kwa juu juu tu, na kwa mtazamo mdogo sana. Wengi hudhani KUJITAMBUA ni kujua tu jina lako, historia yako, au kusema “mimi ni mtu wa aina fulani” kisha wanaishia hapo tu. Kama ndivyo hivyo kuna ukweli wanamiss boss.

Na ukweli ukweli wenyewe ni huu 👇
Kujitambua ni zaidi ya hapo. Ni nguvu ya ndani ambayo huamua mwelekeo mzima wa maisha yako. Kama ingekuwa ni ujenzi basi hii ni RAMANI ya jengo la injinia. Na kama ingekuwa ni chombo cha moto hii ni INJINI yenyewe boss. Huenda ikiwa ini mlango basi huu ni UFUNGUO wenyewe wa maisha yako boss.

Na leo nataka uone jambo hili kwa jicho jipya na tofauti  kabisa ndugu yangu.

Labda nikuulize swali boss, kwani wewe kujitambua ni nini hasa?
Ninajua unajibu lako, hebu kaa nalo kwanza na ikiwezekana utanijibu kwa comment boss.

Ndugu yangu, kujitambua (Self Awareness) si kujua tu “mimi ni nani”, bali ni:

1. Kuelewa kwa kina hisia zako.
Unapojisikia hasira, furaha, wivu, hofu au msongo wa mawazo. je, unaelewa zinatoka wapi?
Watu wengi wanaishi maisha yao wakiongozwa na hisia bila hata kuzitambua. Hivyo basi ukizielewa hisia zako, zinatoka wapi na ukawa na uwezo wa kuzimudu hiyo nayo ni sehemu ya KUJITAMBUA. Lakini pia ni,

2. Kujua tabia zako halisi.
Unajua tabia zako zinakujenga au zinakubomoa?
Tabia zako ndizo zinaunda maisha yako. Kama huzijui, basi huwezi kuzidhibiti. Hata mafanikio yako yanaundwa na tabia zako za kila siku.

3. Kugundua nguvu na udhaifu wako.
Hili ndio eneo nyeti zaidi katika self awareness.
Kujua unachoweza kufanya vizuri (nguvu zako), kipaji, au uwezo binafsi na  kujua ni wapi haupo vizuri au unapohitaji kuboresha (udhaifu wako) kunakupa mwelekeo sahihi wa kukua.
Watu wengi wanapoteza muda mwingi wakipambana na udhaifu wao badala ya kuimarisha nguvu zao hili ni kisa sana boss.

4. Kuelewa athari yako kwa wengine na mazingira yako
Wewe ni nani ndani ya jamii?
Unawajenga au unawachosha watu wanaokuzunguka?
Na pia, mazingira yako yanakuathiri vipi? Yaani, unaathirika vipi na mazingira yako?

⚠️ Ukweli mchungu:
Bila kujitambua, unaweza kuishi maisha yako yote ukiwa busy  lakini si productive. Ukifanya mambo mengi, lakini bila mwelekeo sahihi.
Hapa ndipo siri kubwa ilipo,
Kujitambua ni kama kuwa rais na rubani wa maisha yako mwenyewe.
Huwezi kuongoza taifa usilolijua.
Huwezi kuendesha ndege usiyoelewa mfumo wake.

Vivyo hivyo:
Huwezi kufanikiwa kama hujijui.

.Faida ya Kujitambua (Real Impact boss)
• Unafanya maamuzi sahihi kwa uhakika zaidi.
• Unapunguza makosa ya kurudia.
• Unajenga mahusiano bora.
• Unakuwa na amani ya ndani. Hii ni amani ya kweli boss.
• Unapata mwelekeo wazi wa maisha yako.


Ndugu Ukweli wa wazi  (Wake-Up Call):
Mabadiliko hayatokei nje yako boss,  yanaanzia ndani mwako ndugu yangu.

Na ndani yako kuna ramani yote ya mafanikio yako, kuna ile funguo ya maisha yako. Lakini lazima ujitambue kwanza boss.

Sasa hebu jiulize leo:
• Hivi mimi ni nani hasa?
• Ninasimamia nini?
• Nguvu zangu halisi ni zipi?
• Ni nini kinanirudisha nyuma?
• Naziwezaje hisia zangu?

Ukijibu maswali haya kwa uaminifu, umeanza safari ya kweli ya mafanikio ya kujitambua kwako.

Kwa kuhitimisha kabisa ni kwamba: kama unataka mafanikio na kufika mbali;

Kujitambua si chaguo, hii ni lazima boss.
Ni msingi wa kila kitu mfano kuanzia biashara, mahusiano, hadi maisha na maendeleo yako binafsi.
👉 Ukijitambua wewe ni nani hapo, ndipo dunia itaanza kukutambua.

Share na na mimi kupitia comment. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.

Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697.


Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29