P5. SABABU YA MAISHA YAKO KUBADILIKA AU KUHARIBIKA INAWEZA KUWA MAZINGIRA YAKO.

 


P5. SABABU YA MAISHA YAKO KUBADILIKA AU KUHARIBIKA INAWEZA KUWA MAZINGIRA YAKO.


Self-awareness haiishi ndani yako  peke yako.
Sehemu muhimu ya kujitambua ni kuelewa jinsi unavyoathiriwa na wengine na mazingira yanayokuzunguka, na pia jinsi unavyowaathiri wengine/ mazingira yako. Hii inaitwa Social & Environmental Awareness au Reciprocal Influence boss.

1. JINSI UNAVYOATHIRIWA NA WENGINE NA MAZINGIRA (Incoming Influence).

Wewe ni kamq kisiwa,  ambapo kila siku, mazingira na watu  wengine wanaingiza: mawazo, mitazamo, hisia na tabia mbali mbali ndani yako.
Wakati mwengine bila hata wewe kujua.
Kwa mfano: Watu (Social Influence):
Marafiki au jamaa wanaweza kukufanya uone shaka, hofu, au kuacha jambo muhimu sana maishani.

Na Ukiwa na watu wenye nidhamu na maono, unachukua tabia zao mfano kuamka mapema, kupanga bajeti, au kufanya mazoezi.
Unaishi
Mazingira (Environmental Influence):
Mazingira yenye kelele, vurugu, au tabia zisizo za tija huathiri mood na ushawishi wako wa maamuzi, hisia na tabia boss.
Hakika ni kwamba, Mazingira yenye amani, utulivu, na fursa huchochea ukuaji wako.

Hivyo, Kujua ni nani na ni nini kinachoathiri mawazo na tabia zako ni hatua ya kwanza ya kujitambua kikamilifu boss.

2. JINSI UNAVYOWAATHIRI WENGINE NA MAZINGIRA (Outgoing Influence)
Kila neno unalosema, kila kitendo unachofanya, kina athari kwa watu au mazingira yako boss.
Kama ndivyo hivyo basi wewe ni nafasi ya mabadiliko.
Kwamfano jiulize kuwa, maneno yako yanawasha/kujenga mioyo au kuumiza wengine.
Tabia zako za nidhamu huongeza au kupunguza ushawishi wa timu au familia na mazingira yako kiujumla.
Uwekezaji wako, jinsi unavyoishi maisha yako, huathiri moja kwa moja watu wanaokuzunguka.

Ndugu, Kuwa makini na jinsi unavyoathiri wengine kwa sababu  ushawishi wako ni muhimu wana kwa dunia hii.

Leo staandika sana, nihitimishe tu kwa kusema
Kujitambua hakuishii ndani yako tu; ni kujua mahusiano yako na dunia pia.
Kila kitu unachofanya kina ripple effect kwa wengine na kwa mazingira yako boss.

Kuwa na ufahamu huu huongeza nguvu ya maamuzi yako, ukuaji wa kibinafsi, na uwezo wa kuunda mazingira yenye tija boss.

Hivyo, Angalia watu na mazingira yanavyokuathiri kila siku tambua tabia unazochukua kutoka kwa wengine
Fikiria jinsi unavyoweza kuathiri wengine vyema
Chukua hatua moja leo kuboresha ushawishi wako na mazingira yanayokuzunguka boss.

Nb. Kujitambua ni kuweza kuunda maisha yako na kuunda dunia inayokuzunguka.

#SeeYouNextLevel

Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.

Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026/05/p2-watu-wengi-wanatafuta-pesa-na.html

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork.
+255767653697. 

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29