P5. SABABU YA MAISHA YAKO KUBADILIKA AU KUHARIBIKA INAWEZA KUWA MAZINGIRA YAKO.

Image
  P5. SABABU YA MAISHA YAKO KUBADILIKA AU KUHARIBIKA INAWEZA KUWA MAZINGIRA YAKO. Self-awareness haiishi ndani yako  peke yako. Sehemu muhimu ya kujitambua ni kuelewa jinsi unavyoathiriwa na wengine na mazingira yanayokuzunguka, na pia jinsi unavyowaathiri wengine/ mazingira yako. Hii inaitwa Social & Environmental Awareness au Reciprocal Influence boss. 1. JINSI UNAVYOATHIRIWA NA WENGINE NA MAZINGIRA (Incoming Influence). Wewe ni kamq kisiwa,  ambapo kila siku, mazingira na watu  wengine wanaingiza: mawazo, mitazamo, hisia na tabia mbali mbali ndani yako. Wakati mwengine bila hata wewe kujua. Kwa mfano: Watu (Social Influence): Marafiki au jamaa wanaweza kukufanya uone shaka, hofu, au kuacha jambo muhimu sana maishani. Na Ukiwa na watu wenye nidhamu na maono, unachukua tabia zao mfano kuamka mapema, kupanga bajeti, au kufanya mazoezi. Unaishi Mazingira (Environmental Influence): Mazingira yenye kelele, vurugu, au tabia zisizo za tija huathiri mood na ...

UKIGUNDUA THAMANI ZAKO ZA KWELI, MAISHA YAKO YATABADILIKA KABISA.

 


UKIGUNDUA THAMANI ZAKO ZA KWELI, MAISHA YAKO YATABADILIKA KABISA.


Watu wengi wanaishi maisha ambayo kwa nje yanaonekana sawa, yenye furaha na amani, lakini kwa ndani wanahisi: kuchoka, kukosa amani,  kutokuridhika, na utupu ambao hawawezi kuuelezea vizuri.

Tena wakati mwingine unaweza kuwa: una kazi,
una kipato kizuri tu, una marafiki,
hata mafanikio fulani hivi kwenye maisha yako boss.
Lakini bado ndani yako kuna sauti inasema:
👉 “Kuna kitu hakiko sawa.”

Hata hivyo Mara nyingi tatizo si kwamba huna uwezo.
Bali tatizo ni kwamba unaishi maisha yasiyoendana na thamani zako za msingi. Ndiyo thamani zako boss.

Bila shaka kunaswali umepata ambalo ni,
THAMANI NI NINI HASA?
Simple ni kwamba,
Thamani ni kanuni za ndani zinazokuongoza kufanya maamuzi yako, hata kama unajua au hujui moja kwa moja.

Ni vitu ambavyo: vina maana kubwa kwako,
vinakugusa ndani kabisa,
na vinaathiri namna unavyoishi, kuchagua, na kuhusiana na watu wengine boss.

Inshort ni kwamba hii ni mipaka uliyojiwekea na inaendesha na kuongoza maisha yako boss. Yaani, vitu unavyoviamini kuwa ni kweli katika maisha yako.

Kwa lugha rahisi: thamani ni jibu la swali:
“Nini kilicho muhimu kwangu kweli kweli?”
Kwa mfano:
mtu mmoja anaweza kuthamini uhuru kuliko fedha,
mwingine anathamini familia kuliko umaarufu,
mwingine ukuaji binafsi kuliko starehe.
Na ukiishi kinyume na hivyo, utaanza kupoteza amani yako polepole bila hata wewe kujua, unakuwa na huzuni au kukosa amqni kwasababu thqmani/kunampaka wako umevunjwa. Sijui unanipatq boss.

KUNA ISHARA KWAMBA UNAISHI KINYUME NA THAMANI ZAKO BOSS.
Watu wengi hawajui kuwa tatizo lao si kazi, biashara, au mazingira yanayowazunguka noo.
Tatizo haswa ni kuwa maisha yao hayaendani na kile wanachoamini ndani yao. Au wanaishi nje na thamani values, mipaka yao bila hata wao wenyewe kujua.

Hizi ni baadhi ya dalili zitakazokusaidia boss.
1. Unafanya kazi lakini huna amani
Unafanya kila kitu “sahihi” lakini bado huhisi furaha na  utimilifu.

2.  Unahisi kuna kitu hakiko sawa ndani yako
Lakini huwezi kueleza hasa ni nini.

3. Unafanikiwa nje lakini una utupu ndani
Watu wanakuona umefanikiwa, lakini wewe mwenyewe hujisikii hivyo wala huna furaha kabisa na mafanikio yako.
4. Maamuzi yako yanakufanya ujute baadaye
Kwa sababu uliamua kwa presha ya watu au mazingira not your true self.

Boss ukwel ni kwamba:
Ukisaliti thamani zako kwa muda mrefu, hata mafanikio hayatakupa furaha au maana ya kweli.

Najua kunaswali unajiuliza.
JINSI GANI YA KUGUNDUA THAMANI ZAKO ZA KWELI.
Watu wengi wanaishi bila kujua:
nini kinawaendesha, nini kinawapa maana,
au nini hasa kinawafanya wajisikie hai na amani zaidi.
Lakini kuna njia rahisi ya kuanza kujitambua.
ZOEZI LA “WAKATI BORA”
Fikiria nyakati 3 maishani mwako ambapo:  ulihisi furaha ya kweli, amani ya ndani,
au utimilifu mkubwa.

Halafu jiulize hivi:
1. Nilikuwa nafanya nini?
Je:ulikuwa unasaidia watu?, ukifundisha?,
ukijifunza kitu kipya?, ukiongoza watu?
ukiwa na familia?  N.k

2. Nilikuwa wapi na nani?
Mazingira na watu pia hutoa clues kuhusu thamani zako boss. Si unajua kuna sehemu ukiwa au watu ukiwa nao kuhali fulani unajiskia.

3. Nini hasa kilinifanya nihisi hivyo?
Hapa ndipo siri ipo.
Labda: ulihisi uhuru, upendo, maana,
maendeleo, au connection ya kweli boss.
Hapa  Jibu lako linaonesha kile moyo wako unathamini kwa undani.

BOSS GOJA NIKUPE MIFANO YA THAMANI ZA MSINGI KATIKA MAISHA YA KAWAIDA.
Ndugu yangu Kila mtu ana values tofauti ambazo zinaweza kumatter kwake na kwako zisilete mashiko kabisa.
Baadhi ya thamani za kawaida ni:
Uhuru, uaminifu, Familia, Ukuaji binafsi, Heshima
,Ubunifu, ukweli, Huduma kwa watu, Ujasiri, Upendo, Imani, msimao, Afya, Maarifa, Utulivu, Mafanikio
Mahusiano bora, ubora n.k

Hakuna value “sahihi” au “mbaya.”
Muhimu ni:  kujua zipi ni zako halisi na kuishi nazo huku ukiziacha zikuongoze.

HATA HIVYO UKWELI NI KWAMBA,
Watu wengi wanaishi maisha waliyochaguliwa na: jamii, marafiki, jamilia, au mitandao ya kijamii.
Ndiyo maana:
wanafanya kazi wasizozipenda,
wanaingia mahusiano yasiyowafaa,
na wanafuata ndoto ambazo si zao kabisa boss wangu.

Lakini maisha yenye maana huanza pale unapojua: wewe ni nani, unasimamia nini
na nini kina maana kwako kweli kweli boss.

NDUGU UKIISHI KWA KUTEGEMEA THAMANI ZAKO:  maamuzi yatakuwa rahisi, utakuwa na amani zaidi,
confidence itaongezeka,
na utaacha kuishi kwa kuigiza
Kwa sababu:  hutakuwa unaishi ili kufurahisha watu, jamii au dunia.
👉 utakuwa unaishi kwa uhalisia wako boss. Utakuwa unaishi kutokea ndani kabisa.

Ndugu, ujitambua si kujua jina lako tu.
Ni kujua: moyo wako unasimamia nini,
maisha yako yanapaswa kuelekea wapi,
na nini kina maana ya kweli kwako. Angalia misinga yako ya maisha.

Maisha mazuri si yale yenye pesa nyingi tu.
Ni yale yanayoendana na misingi, miiko, mipaka, na thamani zako za msingi katika maisha yako.

Boss kama boss, naamini umenielewa sana.  Na kama kweli umenielewa hebu nipe misingi au thamani zako 3 tu za maisha yako boss.

Kwa sababu kumbuka:
Ukijua thamani zako, utaanza kuishi maisha yako halisi not maisha ya watu wengine boss.

See you then.

Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.

Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026/05/level-za-mafanikio-sehemu-ya-tano.html

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697. 

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29