NGUVU YA TATHMINI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAKO.

Image
  NGUVU YA TATHMINI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAKO. Kuna jambo moja muhimu sana katika safari ya mafanikio ambalo watu wengi hulipuuzia, lakini lina uwezo mkubwa wa kubadilisha kabisa mwelekeo wa maisha ya mtu yeyote. Jambo hilo si lingine bali ni TATHMINI. Ndiyo tathmini boss. Boss in short tathmini ni uwezo wa kusimama kwa muda, kuangalia ulipotoka, ulipo sasa hivi, na kule unakoelekea. Yaani ni sawa na kujiuliza hivi; Je, njia ninayotumia inanifikisha ninapotaka kwenda? Nimefanikiwa kwa kiwango gani? Nimekosea wapi? Nini kimefanya mambo yasiende kama nilivyopanga? Nifanye nini tofauti ili kupata matokeo bora zaidi? Kwa sababu huwezi kuboresha kitu ambacho hukijui wala hujakipima boss. Ndugu, TATHMINI SI KUSHINDWA HII NI HEKIMA Watu wengi wakiona mipango yao haijafanikiwa haraka huamua kuiacha na kuibwaga ghafla tu. Kibaya zaidi wengine huanza kulaumu: mazingira, watu wengine, bahati, hali ya maisha au kujilaumu wao wenyewe. Lakini mtu mwenye hekima hufanya kitu cha to...

YUPO MBADALA WAKO.

 


YUPO MBADALA WAKO.


Kuna ukweli mmoja ambao wengi wetu hatupendi kuusikia, lakini ni muhimu sana leo tuuelewe;
"Haijalishi wewe ni muhimu kiasi gani leo, siku moja nafasi yako itachukuliwa na mtu mwingine.

Kwa kimombo ni kusema, No matter how important you're one day you'll be replaced."

Unajua boss unaweza kuwa: mwenye elimu kubwa sana, mwenye kipaji cha kipekee, tajiri mkubwa, kiongozimzuri, mtaalamu sana, maarufu sana, mfanyabiashara mkubwa,
au mtu anayependwa na wengi yaani, mtu wa watu.

Lakini ukweli wa maisha ni kwamba hakuna anadumu milele except God and his promises.
Siku moja utaondoka, na maisha yataendelea kama kawaida boss.
Nachotakq kusema ni kwamba boss, Usilewe nafasi uliyopewa leo, kwa sababu siku moja itachukuliwa na mwingine na bado maisha yanaendelea kama kawa boss.

UNAJUA BOSS HISTORIA IMEJAA MIFANO
Kabla yetu walikuwepo watu:
wenye majina makubwa, wenye ushawishi mkubwa,
wenye mali mingi sana,
wenye hekima ya kipekee, waliopendwa sana na watu,  wachezaji wazuri sana, walimu makini, wavumbuzi na wenye mamlaka makubwa boss.

Walikuwa wakionekana kama watu wasioweza kubadilishwa kabisa kwa nyakati zao.
Huemda ilikuwa ni kweli. Lakini leo wengi wao hawapo boss. Hebu wakumbuke watu kama akina, Nyerere, Mandela, Mothertalesa, Gadafi, Magu, Osama, Pele, Kanumba, Michael Jackson,  list ni ndefu boss.

Hawa wote hawapo, lakini cha kushangaza zaidi ni kwamba:  Dunia haikusimama.
Biashara zao zinaendelea.
Taasisi zao zinaendelea.
Familia zao zinaendelea.
Nafasi zao zimechukuliwa na wengine kiloho safi kabisa.
Yaani, pamoja na yote maisha bado  yalisonga mbele.

Huu ni ujumbe boss kwamba SILEWE NA SIFA.

Tatizo la baadhi ya watu ni kuanza kuamini kwamba wao ni muhimu kupita kiasi. Hapa ndo shida ilipo boss.

Utawaona tu wakipata: cheo, fedha, elimu, umaarufu, kuaminiwa au mafanikio fulani tu.
wanaanza kuwadharau wengine. Wanaaanza kujiona bila wao watu hawana ujanja. Wanasahau walikotoka na
Wanasahau kuwa kila walichonacho leo ni dhamana ya muda tu boss.

Kwasababu Sifa ni za muda. Utajiri ni wa muda. Cheo ni cha muda. Umaarufu ni wa muda. Yaani ni swala la muda tu.

Lakini tabia njema, alama na mchango wako kwa watu wengine vinaweza kubaki kwa muda mrefu zaidi boss wangu.

Boss just be humble, UWE MNYENYEKEVU ndugu.
Jua  kabisa mbadala wako yupo, na pengi lako linazibika sana tu.
Na kujua kwamba mbadala wako yupo mahali fulani hakupaswi kukukatisha tamaa boss.
Badala yake kunapaswa kukufundisha:
unyenyekevu, heshima kwa wengine, shukrani
na kutumia vizuri nafasi uliyopewa leo.

Kwa sababu nafasi uliyonayo leo ni fursa ya kuwasaidia wengine kuwa bora kuliko vile ulivyo wakuta, wala si umiliki wa milele boss.

Halafu jua kwamba boss, MUNGU ANA WATU WENGI SANA.
Mara nyingi tunafikiri: "Bila mimi hiki hakiwezi kwenda." Bila hapa hawafanikiwi. Siyo hivyo boss.
Kitu ambacho hukijui boss, ni kwamba:
Mungu ana watu wengi sana.
Kama wewe hukufanya, kuna mwingine atafanya.
Kama wewe huwezi, kuna mwingine ataweza.
Kama wewe utaondoka, kuna mwingine atasimama.
Hii ndiyo sababu hatupaswi kujivuna wala kuwadharau wengine Mungu anaweza akamwinua yeyote amtakaye na kwa wakati wowote. Tusitishane bana.

Goja nikupe hii  HEKIMA boss.
Usitumie mafanikio yako kuwafanya wengine wajione wadogo, dhaifu wala si lolote ila wewe.
Usitumie elimu yako kuwadharau wasio na elimu.
Usitumie cheo chako kuwakandamiza wengine.
Usitumie utajiri wako kujiona bora kuliko wengine.
Kwa sababu kesho mambo yanaweza kubadilika.
Na mtu unayemdharau leo anaweza kuwa msaada wako kesho yako. Sijui kama unanipata boss?

Nimalize kusema hivi, jitahidi kuwa bora.
Jitahidi kufanikiwa.
Jitahidi kuacha alama nzuri duniani.
Lakini usisahau:
Hakuna mtu asiye na mbadala wake.
Na hakuna pengo ambalo haliwezi kuzibwa.
Hivyo basi, ishi kwa unyenyekevu, waheshimu watu, tumia vizuri nafasi uliyopewa leo, na acha urithi wa tabia njema kuliko urithi wa majivuno boss.

Goja nikuulize boss,
Kama ungeondoka leo, watu wangekukumbuka kwa cheo chako au kwa namna ulivyowatendea?

Kwa sababu mwisho wa siku, si nafasi yako ndiyo itakayobaki kwenye mioyo ya watu bali athari uliyoacha katika maisha yao.

#SeeYouNextLevel

Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.

Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026/06/inuka-tena.html

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. 

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29