MAAJABU YA AKIBA

>>SEHEMU
YA KWANZA<<
Moto mkubwa ulikua unawaka juu ya maji, Elvine alizidi kusogea pale huku akistaajabu sana, na aliogopa sana "haaa! hivi inawezekanaje Moto uwake ndani ya maji? au ndiyo ile muvi ya jana inajirudia ila huu ni mwendelezo wake?"
"Hapana, sioti Mimi jamani... au..... naota?".
Ghafla alishituka kutoka usingizini. Kumbe ilikuwa ni ndoto tu!,
alijiuliza sana lakini, kwakuwa alikua ni mtoto aliipotezea na asubuhi alikua ameisahau ndoto ile.
Elvine alikuwa mtoto mdogo mwenye miaka 10.
Na alikuwa akiishi na mama yake tu na hakuwahi kumfahamu baba yake, wala ndugu yeyote toka
aanze kujitambua. Maisha yao hayakuwa ya shida sana bali yalikuwa ya kawaida tu.
Asubuhi aliamka akamsalimu mama yake
ambaye alikuta kamuandalia chai ya maziwa mezani.
" Shikamoo mama! "
"Marhabaaaa El umeamkaje?"
" Kama kawaida yangu ni upande wa kulia
ndiyo nimeamkia" mama yake alicheka sana akasema,
"sawa nishakuzoea kasumbufu kangu"
Mama yake aliitwa Editrin alikuwa akimpenda
sana mtoto wake. Licha ya kuwa na mtoto, Editrin alionekana ni binti mrembo
sana, lakini hakutaka chochote ila mtoto wake awe salama muda wote. Alikua
akifanya kazi Kama secretary Katika kampuni moja ya kuuza maziwa ya unga.
Lakini, mara muda wa kazi ulipoisha tu, aliwahi shule kwenda kumchukua mwanaye
ili arudi nae nyumbani. Hakutaka mwanaye aguswe bila kosa, na pia alibahatika
sana. Maana, Elvine alipendwa na watu wengi sana. Alionekana kuwa mtii na
mwenye adabu kwa kila mtu. Hivyo, alipata kibali kwa watu wa mtaa wa Tosa
jijini Iringa.
Elvine hakwenda shule Siku hiyo kwakuwa ilikua
ni jumamosi. Editrin akamuuliza mtoto
wake
"hivi Elvine unataka nini ukiwa mkubwa?
"Mimii...
sitaki kitu!
(akafikiria kidogo huku anaangalia ukutani ambako kulikuwa na tv ambayo imezimwa)
enheee!!! Mama unakumbuka katuni ya jana? "
"Imefanyaje sasa"
"Anhaaaa! basi sawa kama hukumbuki
"
"Hivi unajielewa Elvine?"
"Naisi tu ila nishapata jibu"
"Enhee jibu gani sema
nisikie"
"Nataka nikulinde wewe tu mama yangu".
Baada ya jibu lile Editrin alicheka sana na akakumbuka kua
katuni ya jana kuna mtoto aliulizwa na baba
yake kuwa anataka nini akiwa mkubwa? Na akajibu kama alivyojibu Elvine.
"Sawa sasa unahisi unaweza basi?
"
"Naweza ndiyo"
"Kweli? "
Yeaaaaa!!!, Elvine alijibu kwa kelele
huku akimkumbatia mama yake.
Walikua na maisha ya furaha sana siku zote.
Editrin alimlea mtoto wake vizuri sana tena katika malezi ya kidini na mara nyingi alikuwa akimuita mwanae
Mtumishi wa Mungu.
Siku moja Elvine alienda kucheza kwa
rafiki yake aliyeitwa Efraimu huko alikutana na wenzake wengi sana. Michezo
iliendelea hadi usiku. Mama yake hakuwa na wasiwasi kwakuwa alijua kuwa mwanaye
yupo salama. Ilipofika saa 2:15 usiku Elvine alianza safari ya kurudi nyumbani hakuwa
na wasiwasi wowote maana watu walikuwa wengi sana njiani.
Alipokaribia nyumbani, alimuona baba mmoja
akitoka nyumbani kwao...
''Mmmmh huyu nani tena kwetu au mwizi? Ngoja
nimwoneshe. Huyu jamaa hawezi kuiba na mimi nipo namtazama. Yaani,
alichoiba lazima arudishe maana hii sura sijawai kuiona hapa mtaani wala
haonekani kama mtu mwema. Kwanza sura yake inatisha. Ngoja...ngoja...ngoja"
Elvine alijibanza ukutani karibu na
nyumba moja ya jirani, kisha akaokota jiwe kubwa
mithili ya kichwa chake. Kisha akatabasamu na kujisemea,
"Leo na Mimi nitakuwa Daudi,
namkamata Goriathi hapa siyo muda.."
Akajiweka tayari kwa mashambulizi. Yule mtu
pasipo kujua lolote alizidi kukaribia mahali alipojificha
Elvine.
'Paaaaah!!!!.' mlio ulisikika.
"Mwiziiiiii,,. jamani
mwizi kanishambulia ..... nakufaaaa..."Alitimua
mbio yule baba kwenda kusiko julikana na hata Kama angeulizwa asingejua anaenda
wapi na wala hakujua aliyempiga jiwe lile
la kichwa ni nani?
Huku nyuma Elvine alicheka hadi akakaa
chini.
"Haaaa!! kumbe
na wababa wakubwa wanaliaga. Hahahaha! Sitaki kuamini hili. Hahahaaha!"
Ghafla wababa wawili na
vijana wanne walikuja pale wakamkuta Elvine ndiyo anasimama kutoka chini
alipokua kakaa akicheka.
"Mtoto mzuri umemuona mwizi maeneo
haya akikimbia?" Aliulizwa Elvine na kijana mmoja, Elvine alitaka kucheka
akajizuia.
"
Mwi? " Akawaza kidogo,
"anhaaaa ee ndiyo nimemuona"
Wakauliza
kwa jazba zaidi wale vijana wakiwa wameshikilia mawe na malungu
"
Kapita wapi?"
"
Kapita..... Ilaaa hapana mi nadhani sio mwizi yule maana yeye ndiyo kaita
mwizi. Kwahiyo nadhanii sijamuona."
"Aaaa
tuondoke hapa huyu mtoto hajui kitu hebu twende mbele" walisemezana wale
watu na kuondoka zao
Elvine alizidi kucheka hadi nyumbani kwao.
Akamkuta mama yake sebuleni
"Elvine
ulikua wapi?"
"Si
kwakina Efraimu" Elvine alijibu huku alicheka.
"Mpaka
saizi? Alafu Mimi naongea wewe unacheka.!?"
"Hapana
mama nisamehe. Ni kwamba nimefurahishwa huko nilikotoka"
"Na
nini?"
"Kwanza
upo salama mama?"
"Mimi mzima tu"
"Njiani
nilimuona Daudi na Goliath wakiwa katika vita kali
wakati huo Daudi alikuwa akitetea Israel iwe salama pamoja na waliomo"
"Mmmh!! umeanza hadithi za vikatuni"
"Lakini
wewe si ulisema ni hadithi za kweli na ipo kwenye
biblia au?"
"Sawa
basi. Ndiyo ni ya kweli. Sasa wewe umewaona wapi? Na unamaana gani?"
Akacheka huku akielekea chumbani kwake
" Ni maono mama usijali"
"
We mtoto hebu rudi hapa ule"
"
Mweee samahani nishakula kwa watu maana, niliona chakula kinanukia vile
nilishindwa kukataa. Ila kwakua ni wewe umepika na unajua
kupika zaidi ya mama Efraimu ntakuja kula kidogo tena"
"Duuuh
hapa mtoto Sina kwa kweli"alijisemea mama Elvine huku akitabasamu.
Baada ya muda walikula chakula kisha, wakasoma
biblia kama ilivyo ada yao. mama Elvine akamsomea biblia mwanaye Kisha
wakaomba kwa pamoja na kila mmoja akaelekea kulala.
Wakati Elvine akienda chumbani kwake kulala
aligeuka na kumwita mama yake halafu akamuuliza kama kuna
mgeni yoyote aliekuja kwao jioni ile
" Mgeni? nani kakwambia mbona hakuna
aliekuja?" Mama alijibu kwa jazba kidogo
"Anhaa sawa mama usiku mwema" Elvine
akaingia kulala lakini alishangaa kwanini mama yake alijibu Kama hakupenda lile
swali. Lakini kwakuwa ni mtoto aliipotezea na
kuona kawaida tu. Akaingia kulala....
Siku iliyofuata ilikuwa siku ya jumapili. Hivyo,
waliamka na kujiandaa kuelekea kanisani. Asubuhi hiyo
ilikuwa ni njema sana kwa Elvine maana kati ya siku alizokuwa anazipenda
sana ni siku ya jumapili.
Walipofika kanisani aliowaona wageni wengi
sana siku hiyo. Japo kanisani hapo kulikuwa
na watu wengi lakini Elvine aliweza kufahamiana na watu wote wa pale kanisani
hii ni kutokana na ujanja wake. Alishangaa sana hivyo akamuuliza mama yake
kabla hawajatengana kuelekea kwenye madarasa yao ya jumapili.
"Mama
mbona watu wengi wanaoingia kanisani ni wageni au tumepotea kanisa ninii.....?". Wote
wakacheka
hadi waliokuwa jirani yao walisikia na kucheka pia. Elvine alipendwa sana na
watu wengi kutokana na ucheshi wake na maneno ya mzaha, hivyo alikuwa na kibali
sana kila alipokwenda.
Alipoingia kwenye darasa lao la Sunday
school (shule ya jumapili kwa watoto). Alishangaa pia maana, kulikuwa na watoto
wakike watatu ambao wailikuwa wageni. Alistaajabu kimoyomoyo akajisemea "mmmmh! leo
siku ya ajabu sana,". Alipo watazama wale wageni
mmoja aligeuka na kumtazama kisha nae akatabasamu. Elvine
alishangaa kidogo nae akatabasamu tena.
Alishangaa sana maana wageni wale
walionekana kama wenyeji kuliko hata yeye. Maana kila sekta walikua wepesi
kufanya jambo. Mwalimu aliposema nani anawimbo wa sifa mmoja wao aliiongoza
sifa. Maswali yote ya siku hiyo wale watoto waliyajibu kwa wepesi sana, neno la
siku hiyo mtoto mmoja kati yao ndiye Aliyetoa neno. Na neno hilo lilihusu
"IMANI" Katika yote Elvine alibeba sentensi moja ya binti yule
ambayo ilisema
"ukiwa na imani unaweza kubadili
dunia yako"
Mwisho wa ibada watoto wale
walijitambulisha nao walikua ni Elimina, Ester na Elvila.
Baada ya ibada ile watoto wote walitakiwa
kuingia kwenye ibada ya pamoja na watu wazima. Kabla ya kuingia Elvine alimfuata
Mwalimu akamuhoji kidogo kuhusu hawa wageni imekuwaje wametoa hadi neno ilihali ni wageni? Mwalimu alimwambia kuwa watoto hawa ni wageni wenyeji,
na Elimina ni mtoto wa mchungaji wao 'Moses' ambaye anasoma nje ya nchi (ndie aliyetoa
neno)
"Anasoma?.."alihoji
kama hajasikia kilichosemwa na mwalimu.
"Anasoma
nje huko"
"Wapi
huko?"
"Nasikia
ni China"
"Mmmmmh
sawa"
Elvine aliingia kanisani na akajikuta
kaumia sana kwa kupata wivu moyoni mwake.
Ndani ya kanisa ibada ya sifa ilikuwa
ikiendelea na Elvine alipoingia kanisani alienda kukaa ukutani kabisa na akawa
amejibanza kwa huzuni. Siku hiyo hakucheza wala kusimama wakati sifa ilikuwa
imepamba moto, jambo ambalo halijawahi tokea. Alimfikiria na kumtamania
mtoto wa mchungaji na alipata wivu sana. Muda wote wa ibada macho yake yalikuwa
kwa mabinti wale watatu kwani aliwaona Kama watoto wa matajiri na akapata wivu
mkubwa juu yao.
Watoto wale walikuwa bize na sifa na hata
hawakujua kama wanatazamwa na Elvine. Na isitoshe Ester na Elimina walikuwa
pamoja lakini, hawakuwa wanafahamiana na Elvila. Hivyo, kila mmoja alikuwa bize
na sifa japo walikaa viti vinavyofuatana. Wakati Elvine akiwa kazama katika
wimbi la mawazo huku akiwa anawatafakari wale watoto.
Ghafla alishtuka baada ya kuona
ukimya wa ajabu mle kanisani. Akili ilirudi haraka na akageuka kutazama
madhabahu. Lakini cha ajabu,
mle kanisani
alishangaa kuona hakuna mtu yeyote isipokuwa yeye na wale watoto watatu wageni.
Alipata hofu zaidi maana aliona kana kwamba Kuna mwanga uliongezeka mle
kanisani ambao haukutokana tu na taa zilizokuwa zinawaka. Bali, kulikuwa ni
mwanga mkali na ukungu kwa mbali. Alipotazama nje kupitia dirisha aliona giza
ambalo liliashiria usiku ulikuwa umeingia,
tena sio
mawio bali usiku wa manane.
"Mamaaaaaaa" alipiga kelele na hakuna
anaesikia na cha ajabu zaidi ni kwamba,
hata wale watoto watatu walioonekana kuwa bize na kucheza kwa staili za midundo
ambayo haikuwa inasikika.
Sehemu ya pili itaendelea juma tano>>>>>usikose kufuatilia
Bonyeza hapa kupata mwendelezo wake
Hadithi hii imeandaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN. Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo, mashairi, Hadithi (simulizi) na ngonjera.
Whatsapno. >>>>>
+255789523850. Normal >>>>>+255747313148.
Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.
Mawasiliano:
Whatsapno. >>>>> +255767653697.
Normal >>>>>+255783327456.
GeT tO tHe NeXt LeVeL!.