MAAJABU YA AKIBA

SIMULIZI YA
KUSISIMUA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”.
>>SEHEMU
YA PILI.
Alipotazama nje
kupitia dirisha aliona giza ambalo liliashiria kuwa ilikuwa ni usiku
umeingia tena sio mawio bali usiku wa manane.
"Mamaaaaaaa!" alipiga kelele na hakuna anayesikia na cha ajabu zaidi ni kwamba hata wale watoto watatu walionekana kuwa bize na kucheza kwa staili za midundo ambayo haikuwa inasikika.
Kama hujasoma sehemu ya kwanza bonyeza hapa.
Sasa
inaendelea......
Elvine alizidi kuchanganyikiwa maana hakujua
kama ni kweli anaona, anaota ama anaona maono. Alizidi kulia lakini hakuna aliyesikia
kilio chake. Mlango aliuona upo mbali sana na nje pia aliogopa kutoka kwa lile giza
nene. Aliamua kukimbilia mlangoni lakini hata nguvu za kufungua mlango hakuwa
nazo akajikuta amekaa chini huku akitetemeka na kuwashangaa wale mabinti
wageni.
"Eee Mungu nisaidie... eeh Mungu
nisaidie mwanao" alijikuta akitamka maneno hayo kwa woga na mtetemeko wa
hofu kubwa.
Wakati hajui cha kufanya, alishangaa
kumuona Elvila akimgeukia na kutabasamu. Hili lilimshangaza zaidi maana Elvila
alifanya hivi kila alipogongana nae macho, tangu wakiwa Sunday school hadi
kanisani.
"Huyu binti ananijua mimi? ananiona
eeeh!" alijiuliza mwenyewe pasipo kuwa na majibu maana alikwisha tambua kuwa
watu wengine hawamuoni yaani, Elimina na Ester.
Elvila alitoka pale alipokuwa amekaa na
kuanza kusogea pale mlangoni ambapo Elvine alikuwa amekaa chini akilia, tena
alikuwa na tabasamu lisilo hata na hofu.
"Elvine alijikuta anaanza kumuogopa
hadi yule mtoto mwenzake, na isitoshe alishangaa zaidi namna binti yule
alivyokuwa akimtazama na kutabasamu kana kwamba anamfahamu vizuri.
"Elvine!!!" binti yule alimwita.
Mapigo ya moyo wa mbio zaidi na akahisi kufa kufa hivi,
"We....we....wewe ni nani? Aliuliza kwa
hofu sana huku machozi yanatiririka kama maji yaliokosa leso.
"Usiogope, upo salama, wewe ni mtoto wa
Mungu uliyeugusa moyo wake, maana wewe ni mtu mkubwa sana. Usijifananishe na
wengine hata kidogo maana thamani yako sio sawa na unayejifananisha naye.
Mungu analo kusudi juu yako. We si, Mtumishi wa Mungu eeh!!" binti yule
alieleza na kumalizia na swali.
"Eee....ndi.. ndio" alijibu Elvine
kwa woga sana.
Alipotazama mbele alishangaa kuona kila kitu
kimerudi kama mwanzo. Na Sasa ilikuwwa ni wakati wa neno. Mchungaji Moses yupo
madhabahuni anatoa neno na nje pia kulionesha kuwa ni saa saba mchana.
Akageuka kumtazama Elvila ambaye bado alikuwa
pembeni yake anatabasamu. Elvine alipiga kelele "mchungajiiiiii!!!!!"
Lakini cha ajabu hakuna aliyekuwa anamsikia na watu walikuwa wametulia sana.
Alitaka kusimama lakini akagundua kuwa hata kusimama hawezi.
"Unataka nini?" alijikuta akimuuliza Elvila swali hili.
"Acha woga na ukafanye yalio mapenzi ya Mungu, na huu ndio ujumbe
niliotumwa kwako. Maana wewe ulikwisha ahidiwa kuwa mtoto wa nadhiri kwa Mungu
na hatima yako ni ya KIMUNGU."
"We ni nani?"
"Mtumwa tu wa ujumbe kuufikisha"
"Kwanini uje kwangu?"
"Ndiye uliyekusudiwa"
"Na wale wageni wengine ni wewe ndiyo umekuja nao?"
"Hapana wale ni watu wa kawaida tu, ila leo kwakuwa Mungu kamtuma
mjumbe wake kwako, ilitakiwa wageni waletwe wengi ili, malaika wake aingie
miongoni mwao. Kwahiyo, usiogope. Elvine hii ni habari njema ya hatima yako,
Mungu anakupenda sana. Utasimama kuwakomboa wanyonge na wenye shida utawapa
mahitaji yao". Maneno hayo halisemwa na Elvila huku akitabasamu. Elvila
alimtazama kwa muda Elvine kisha akaendelea,
"Najua hunielewi kwakuwa wewe bado mdogo. Lakini, kuna wakati
utaelewa, usiogope hata kidogo maana Mungu kaweka kitu ndani yako ambacho
kitakupa nguvu ya kutumika". Elvila alimaliza kuongea na kumgusa Elvine
kwenye paji la uso kwa mkono wake wa kuume, na baada ya kufanya vile mwanga
mkali ulitoka katikati ya mkono wa paji la uso. Elvine akajikuta akisema..
"Yesu nisaidie mimi nipo tayari kukutumikia ila naomba
unisaidie.." wakati anasema hivyo kwa mbali alimsikia Elvila akisema
"sasa umekili na ndicho kilichonileta kwako, na Bwana kakuapisha leo na
kukukubali wewe Elvine......"
Ghafla alishitushwa na mchungaji aliesema tusimame tufunge ibada.
"Heee! nilikua naota ama? Alitazama alipo na akagundua kuwa ni
palepele alipokuwa kakaa mwanzoni mwa ibada baada ya kutoka Sunday school, na
alikuwa kainamisha kichwa kama aliekuwa kasinzia.
Hapana hii sio kweli. Alijikuta kasema kwa sauti neno hilo hadi watoto
wenzie wakamshangaa.
Mwalimu hakuwa mbali akamsogelea na kumwambia "hivi unanini wewe
leo?. Maana umelala toka sifa hadi saizi na tumekuamsha hadi tumeshindwa. Halafu
saizi unaanza kelele tena?"
Elvine alishangaa zaidi na akawa haewi hata cha kusema au kujibu, alikaa
kwa kutulia hadi ibada ilipoisha kabisa na watu wakaanza kutawanyika. Alipotoka
nje alikwenda kumfuata Elvila na akamuuliza kama kuna kitu kimetokea ibadani.
"Kitu! Kitu gani?"
"Aaaa.... Ni... Au basi samahani"
Elvila hakujibu kitu bali alitabasamu tena kama anaejua kitu. Elvine
alitaka kumuuliza swali zaidi lakini kabla hajatamka neno alikuja mama mmoja na
kumwita Elvila na kuondoka naye jambo ambalo moja kwa moja lilionesha kuwa wale
walikuwa ni mama na binti yake au mtu wake wa karibu ambaye anakaa nae.
Elvine alikosa majibu ya maswali yake, na akabaki na maswali mengi
kichwa. Baada ya mda Editrin alikuja na kumwita Elvine hivyo safari ya kurudi
nyumbani ilianza.
Wakati wapo njiani Elvine aligeuka nyuma na akavutiwa na namna mchungaji
na mkewe walivyokuwa wanafurahi na mtoto wao Elimina huku wakiingia kwenye gari
lao aina ya 'prado' aliwatamani kidogo lakini moyoni akasikia ile sauti ya Elvila
ikimwambia usijifananishe na mtu, wewe ni mtu mkubwa.
Alitamani kumwambia mama yake lakini akaogopa, maana mama yake alisha
mkataza kulala kanisani hivyo hakujua namna ambavyo mama yake atalipokea jambo
lile, na tangu siku hiyo wale wageni wote hawakuja tena hata yule mtoto wa
mchungaji na rafiki yake nao walirudi china ambako ndiko walikokuwa wanasoma
maana walikuwa 'family friend' yaani Ester pia alikuwa ni mtoto wa mchungaji Joseph wa
mkoa wa mbeya sehemu iliyoitwa uyole ya kati. Lakini, taarifa za Elvila
hazikusikika tena tangu siku hiyo.
Hii ilimpa tabu sana Elvine
lakini akaamua kupotezea kwahiyo, hakumwambia mtu yeyote mpaka akaja kulisahau
kabisa jambo lile.
Siku moja akiwa anacheza na wenzake mtoto
mwenziye alimtania na kumwambia yeye ni mtoto asiye na
baba. Neno lile lilimuuma sana na akalitunza moyoni mwake mpaka aliporudi
nyumbani.
Tofauti na siku nyingine mama yake alimshangaa
sana Elvine kwani hakuwa na raha kabisa siku hiyo.
Jambo ambalo lilimshangaza sana Editrin aliyekuwa kakaa sebuleni
akitazama runinga.
Editrin alishitushwa
na mlio wa mlango uliobamizwa kiasi cha kulipuka moyo.
"We Elvine
nini shida
mbona unabamiza mlango hivyo?." Editrin alihoji kwa
kufoka
kidogo. Ilikuwa rahisi sana kwa Editrin kujua kuwa Elvine
hayuko sawa
maana ndiyo ilikuwa tabia yake kubamiza milango pindi anapokuwa na hasira au
huzuni.
" Hamna kitu mama ila ninausingizi
sana naomba niende kulala kwanza" alijibu Elvine
kwa huzuni sana, kisha akaondoka kuelekea chumbani kwake ambako
alijifungia na kulia sana. Mwanzo hakuwahi kujali kuhusu baba lakini siku hii
ilikuwa ya huzuni sana kwake maana ndiyo siku ya kwanza kujiona tofauti na
wenziye na akajikuta akitamani sana kama angekua na baba pia,
lakini aliwaza anaanzaje kumweleza mama yake kuhusu hili? hapo
ndio alichanganyikiwa sana.
Aliogopa kumuhoji mama yake maana katika kusoma kwake alishawahi kusoma na kusikia taarifa na hadithi mbalimbali zilizoelezea namna ambavyo wanawake wengi wanavyotelekezwa na waume zao. Kwahiyo, alihisi yamkini ndicho kilichotokea kwa mama yake. Pia, aliwaza pengine angemfanya mama yake ahuzunike zaidi.
Usiku alitoka chumbani na kwenda hadi nje
kabisa na nyumba ambako alipofika huko alitazama juu na akaanza kujisemea
mwenyewe
"Mungu, baba yangu
yuko wapi? Nimuulize mama au....? Aaaa mi sijui cha kufanya kwa kweli.
Lakini natamani na mimi kumjua baba japo jina. Maana mimi naitwa Elvine
Editrin, kwanini na mimi nisiwe kama wengine, kwani mama yangu
alifanya kosa gani hadi ukaruhusu afanyiwe hivi Mungu?" Aliendelea
kijihoji huku akilia. Ghafla radi ikapiga na mvua
ikaanza kunyesha alipotaka kurudi ndani haraka akajikuta anaona kizunguzungu na
akaanguka chini, akapoteza fahamu.
Editrin alishtuka saa 7 usiku akiwa na wimbi
la usingizi na akajikuta anawiwa kwenda kumwangalia mwanaye maana alikuwa kaota
ndoto mbaya juu ya mwanaye lakini aliposhituka kutoka usingizini
hakuwa anaikumbuka ile ndoto, ila akakumbuka kuwa Elvine hakuwa
sawa wakati anarudi shule.
"
Hivi huyu mtoto anashida gani? Atakuwa aliamka kuja kula kweli? "
Alijihoji bila kuwa na jibu.
Alijivutavuta mpaka
chumbani kwa
Eliasi ambako hakumkuta mwanae kitandani. Alishituka sana na usingizi
wote ulikata ghafla na akatoka mbio hadi
sebuleni lakina
bado hakumkuta Elvine, akakimbia zaidi hadi
bafuni, chooni, na jikoni lakini Elvine hakuwepo. Aliogopa sana
akatoka nje huku katahamaki na machozi yakiwa yameanza kumlenga
machoni mwake.
Alishangaa kuona alichokuwa amekiona.
Alikuta kuna maua mekundu na viatu vya Elvine, lakini Elvine
hakuwepo.
"Elvine
mwananguuu!!! Alijikuta kapiga yowe iliyowaamsha majirani zake wote.
Kufikia saa 11 alfajiri watu wengi
walikuwa wamejaa pale nyumbani kwa Editrin. Taarifa zile zilisisimua watu wengi
mjini pale ambapo kila mmoja alitamani kujua ni nini kimetokea kwa Elvine,
hii ni kwa namna mtoto yule alivyokuwa akipendwa na watu.
Editrin alikuwa hana ndugu mjini pale
lakini, alikua na marafiki wengi sana ambao ndio waliokuwa wafariji wake na
majirani zake walijitahidi kutafuta huku na huko kama wanaweza kumwona
Elvine lakini jitihada zote hazigonga mwamba.
Siku zilipita, wiki , miezi na hatimaye
mwaka Elvine hakuonekana. Hali hii ilikuwa ngumu sana kwa Editrin na akawa kama
kichaa maana mda wote alikumbatia viatu vya mtoto wake na hakutaka viguswe na
mtu yeyote.
Stori ya Editrin na kupotea kwa Elvine ilienea kila
mahali.
Siku moja Kuna mama mmoja alikuja kwa mama Efraimu ambako ndiyo Editrin
alikokuwa kahifadhiwa huku akiwa kama hayuko sawa. Mama yule alikuwa wa makamo
sana na kwa muonekano tu alionekana kuwa
ni mtu mwenye pesa sana. Alijitambulisha kuwa yeye ni mama wa Editrin.
Na akaeleza kuwa Editrin alitoweka nyumbani kwa miaka mingi baada ya mgogoro
uliowahi kutokea kati ya baba yake na Editrin, hivyo yeye kaweza kufika pale
kwa msaada wa taarifa za habari.
Mama Efraimu alimruhusu yule mama kuingia kumwona Editrin. Yule mama
baada ya kumwona Editrin alianza kulia na akaanza kuimba wimbo..
"Editrin for editing the world... Mama for all mothers in the world
but Eliana mama is only one for you kids....oooh for you kids..."
Mama yule aliuimba ule wimbo huku akilia na kumsogelea Editrin ambaye
alionesha kurudisha ufahamu baada ya kumtazama yule mama kwa mda mrefu.
''Mama!!" Editrin aliita na kumkumbatia mama yule aliyeitwa Eliana.
"My
daughter" mama yule alilia zaidi.
Walikumbatiana kwa nguvu kama ruba kwenye ngozi ya binadamu. Walilia kwa
mda mrefu sana na baadae walianza kuuimba ule wimbo wote huku bado
wamekumbatiana
"Editrin for editing the world... Mama
for all mothers in the world but Eliana mama is only one for you kids....oooh
for you kids..."
Editrin alikumbuka wakati akiwa mdogo namna
mama yao alivyokuwa akiwaimbia yeye na Edgar kaka yake. Na palepele aligeuza
wimbo na akaimba tena,
"Edgar for changing the world...
Mama for all mothers in the world but Eliana mama is only one for you
kids....oooh for you kids..." Wote walirudia wimbo na kulia sana.
Baadae Editrin akajikuta sasa anajitambua tena
maana ni kama alikuwa amechanganyikiwa.
"Mama mwanangu wamemuiba"
"Don't cry (usilie)"
"How mama how.....(Kivipi mama
kivipi?)"
"Mama kwanini huyu mtoto hana bahati
jamani?. Aaaa mama. Editrin alilia kwa uchungu zaidi,"
(Tangu kupotea kwa Elvine ilikua ni mwaka mmoja
na miezi miwili sasa. Hivyo watu walikwisha kata tamaa kuhusu Elvine.)
Mimi mwanangu najua atarudi tu japo sijui yupo
kwenye hali gani. Alisema Editrin huku akizidi kulia.
Editrin baada ya kutulia alimsimulia kisa kizima tangu alipotoroka kwao hadi kufikia hapa alipo na namna ambavyo Elvine kapotea. Eliana alionesha kuumia sana kwani kwa namna nyingine tunaweza kusema yeye ndiye aliekuwa bibi wa mtoto yule. Wakiwa wanaendelea na mazungumzo yale Editrin akaanza kukumbuka kisa chote kilichomkuta kwenye maisha yake hata kupelekea yeye kutoroka kwao Dar es salaam na kuamua kwenda kuishi Iringa.......
Sehemu ya tatu>>>>>Itaendelea ijumaa. Usikose kufuatilia
Bonyeza hapa kupata mwendelezo wake.
Hadithi hii imeandaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.
Mwimbaji
na mtunzi wa nyimbo, mashairi, Hadithi (simulizi) na ngonjera.
Whatsapno. >>>>>
+255789523850. Normal >>>>>+255747313148.
Mawasiliano:
Whatsapno. >>>>> +255767653697.
Normal >>>>>+255783327456.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Abel Banene · 95 weeks ago
Elias Migongo · 95 weeks ago
Mhitaji · 95 weeks ago
Migongo Elias · 95 weeks ago
Pephias · 95 weeks ago
Elias Migongo · 95 weeks ago
Judith ndumbaro · 94 weeks ago
Elias · 93 weeks ago