MAAJABU YA AKIBA

SIMULIZI
YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”.
SEHEMU
YA KUMI.
Ilipoishia....
Ile
nyumba haikuwa mbali na barabara hivyo akafika barabarani lakini kwa yale
maumivu aliyokuwa nayo hakuweza kukimbia zaidi, alidondoka katikati ya
barabara, akiwa pale alisikia sauti ya mama mmoja kwambali sana ikimwambia
"Kijana wangu nini shida amka! Nini kimekukuta? Haa! Mungu wangu. Mwanasheria!! hebu tumbebe huyu tumuwahishe hospitali kwanza, maana nahisi kavamiwa na vibaka wa mji wetu huu...."
kusoma sehemu ya tisa bonyeza hapa
Sasa
inaendelea....
Editrin hakujua kwanini kijana yule
alikuwa akilia, hivyo akahisi labda ni kwasababu ya maumivu aliyokuwa nayo.
"Vipi kijana, unaendeaje? Na nini
kimekukuta" aliuliza Editrin kwa huonyesha kuhuzunika sana kwa kile
kilichotokea kwa Elvine
"Mama!!!" Elvine aliita akiwa
bado anahisi yupo ndotoni.
"Usijali kijana wangu, utakuwa
salama tu", nitakuchukua hapa baada ya matibabu halafu twende kwangu
ukaniambie kilichokukuta."
Elvine hakuwa anaongea chochote zaidi
ya kulia kwa sababu ya uchungu aliokuwa nao. Editrin aliendelea kumuongelesha
lakini hakujibiwa. Daktari alikuja na kukamilisha matibabu. Baadaye Editrin
alimchukua Elvine mpaka kwao ambako alikuwa akiishi na wazazi wake.
Elvine Alishangaa sana baada ya kuiona
nyumba ambayo mama yake alikuwa akiishi na hapo ndipo akagundua kuwa haoti bali
ni uhalisia kabisa kuwa yule ni mama yake.
Alikaribishwa vizuri na bibi yake
Eliana. Alikupofika mule ndani alikuwa akishangaa tu kama haelewi
kinachoendelea.
Walikaa sebuleni, baada ya dakika
chache alikuja Mr. Edward naye akakaa sebuleni.
"Baba! huyu ndiye kijana
niliyemuokota jana njiani muda ule nilipokuwa nakuja na mwanasheria ofisini
kwako." Aliongea Editrin kwa kufungua maongezi
"Anhaaaa! Nini kimetokea kwako
kijana wangu? Maana nasikia kuna majanga yalikukuta"
"O..o.. ndi.. ndiyo"
"Ni nini?"
"Nilikuwa nimevamiwa"
"Na nani?, Je, hao watu
unawajua?"
"Ndio"
"Basi subiri kidogo mwanasheria
wetu anakuja sio muda, ili tujue namna ya kukusaidia, maana hata uyo mama yako
hapo anakesi anataka kuifungua, kwahiyo nazani mwanasheria akija tutakusaidia
pia sawa eeh?" Aliongea Mr. Edward kwa tabasamu pana la ukarimu.
Baada ya muda mfupi mwanasheria
alikuja.
"Karibu sana Mr. Ebrania"
Mr. Edward alimkaribisha mwanasheria yule
"Asante sana, za hapa?"
Njema sana
Vipi kijana wangu unaendeaje sasa
maana jana ulikuwa hali mbaya sana, aliongea Mr. Ebrania kumwambia Elvine
Naendea vizuri sasa.
Basi vizuri
Baada ya kukaa kutulia, Editrin
alimwambia mwanasheria amsikilize kwanza Elvine
Elvine alianza kueleza kuwa alitekwa
na mtu mmoja ambaye anamfahamu lakini hakutaja jina. Baada ya kueleza kilichotokea
aliamua kujitambulisha vizuri kwa mama yake.
Editrin hakuamini baada ya Elvine
kusema yeye ni kijana wake aliyepotea miaka mingi iliyopita. Kila mtu
alishangaa. Editrin alisimama na kwenda kumkumbatia mwanaye lakini kwa furaha
aliyokuwa nayo alilia sana mpaka akapoteza fahamu.
Elvine alilala pale ndani tena
akapokelewa vizuri sana na babu na bibi yake. Hakutaka kukaa mbali na mama yake
tena kwahiyo, alilala kwenye kiti karibu na kitanda ambacho mama yake alikuwa
amelazwa na alilala akiwa kashikilia mkono wa mama yake.
Asubuhi Editrin alirudisha fahamu na
alipoamka tu alitaja Elvine kwakuwa hakumuona pale chumbani; Elvine alikuwa
kaamka mapema sana na akaenda kuandaa maziwa jikoni kwaajili ya mama yake.
Editrin aliogopa sana maana alihisi
Elvine kaondoka. Alitoka haraka sebuleni huku akiita Elvine. Sebuleni alikutana
na mama yake Eliana.
"Usijali Elvine yupo jiokoni
kasema anataka akuchemshie maziwa"
Editrin pasipo kujibu neno haraka
alikwenda jikoni kuhakikisha.
Mwanangu jamani, umerudi kweli?.
Alimkumbuka mwanaye kwa nguvu sana huku machozi yakimtoka. Elvine naye
alipomtazama mama yake alitokwa na machozi; wakalia kwa muda mrefu sana.
Editrin alikuwa na maswali mengi sana
ya kumuuliza mwanaye lakini kabla hajauliza jambo, geti liligongwa, Editrin
alikuwa bado anawasiwasi asije akawa Emiliano ndiye aliyekuja kumtafuta hivyo
akamwambia mwanaye waende chumbani kwake ili wakajifiche huko. Elvine naye
alipata maswali mengi sana ambayo alitamani mama yake akamjibu.
Walikwenda chumbani na wakajifungia kwa
ndani ili kama Emiliano atakuja Basi pale chumbani ashindwe kuingia.
Walipofika chumbani, Editrin
alimkumbatia mwanaye tena kama mtu ambaye katendewa muujiza wa ajabu.
"Hivi ni kweli wewe ni Elvine? Ulikuwa
wapi siku zote? Na kwanini uliniacha mwanangu?"
"Nisamehe mama yangu mpendwa,
nilipotea mama yangu" Elvine aliongea vile huku alilia sana. Ghafla meseji
iliingia kwenye simu ya Elvine kutoka kwa Elimina mtoto wa mchungaji Moses
"Elvine kwahiyo ndiyo umeamua hivyo
eeh! Sawa bwana, kweli shukurani za punda mateke tena ya tumbo"
Elvine alisikia mlio wa simu yake lakini
hakujali wala kutazama kuwa ni nani aliyemtumia ujumbe.
"Editrin!!!!" Editrin aliitwa
na mama yake.
"Mmh! Kuna nini huko?" Editrin
alimuuliza Elvine kana kwamba Elvine anajua kinachoendelea sebuleni.
"Sijui, lakini mama, kumbe hapa ni
kwenu? Mbona haujawahi kuniambia kuwa tuna ndugu? Na Nini kimetokea mpaka umekimbia
kwa Emiliano baba mdogo? Vipi kuhusu baba yangu pia? Natamani sana kujua
kwanini ulinificha habari za baba na ndugu zako"
Elvine alikuwa kamkazia macho sana mama
yake kuonesha umakini wa kusikiliza.
"Editrin!!!!!!! Njoo haraka
mwanangu". Eliana alibisha hodi pale mlangoni.
"Nadhani sio Emiliano, maana
mama asinge niita hivyo. Twende kwanza sebuleni, halafu maswali yako yote
nitayajibu badae." Editrin aliongea huku alisogea mlangoni kisha akafungua
mlango.
Walitoka pale chumbani na kuelekea
sebuleni. Walipofika walimkuta baba mmoja ambaye alikuwa kavaa suti nzuri ya
rangi nyeupe akiwa amepiga magoti tena akiwa kainamisha kichwa chini.
"Kulikoni hapa tena?
Editrin alimuuliza mama yake".
"Unamjua huyo? Eliana naye alimuuliza binti yake"
"Mmmh!! Ngoja nimtazame".
Wakati Editrin anasogea kwa yule baba. Elvine alimtambua yule baba kuwa ni yule
Mr. Edu ambaye ndiye alimwambia kuwa amuite pacha.
"Haaa ni wewe baba yangu?"
Yule baba alipoisikia sauti ya Elvine aliinua kichwa haraka na kusimama pale
alipokuwa amepiga magoti. Na kuwasogelea Editrin na Elvine.
"What? E... E.. edwi....
Edwin??" Editrin alishangaa na kumrukia Edwin mwilini kwa kumkumbatia.
"Edwin ni nani tena?"
"Elvine huyu ni baba yako"
"What!? Baba yangu, hakufa? Ooh
no! Kumbe wewe ni baba yangu?. Elvine naye alistaajabu sana uweza wa Mungu."
"Nimewatafuta sana nyie
watu, kumbe siku zote nilikuwa naonana na wewe halafu nikashindwa kukujua,
nisamehe sana Elvine mwanangu, maana nilikupenda zaidi baada ya kuona jina lako
linafanana na jina la mwanangu na kumbe ni wewe?" Edwin alimtazama Elvine
na kumkumbatia pia. Wote wakakubaliana kwa furaha yenye machozi ndani yake.
Wakiwa pale ghafla mlango ulifunguliwa
na aliyeingia alikuwa ni Emiliano. Editrin hakutaraajia kwasababu Emiliano siku
hiyo hakuja na gari Kama siku zote hivyo walijisahau. Na pia walinzi
hawakumzuia Emiliano kuingia kwakuwa walikuwa wakijua kuwa Emiliano ni mkwe wa
ile familia na hawakuambiwa chochote kuhusu kutoroka kwa Editrin kwa mume wake.
"Editrin mke wangu" Emiliano
aliita na wakati Editrin kashangaa pale. Emiliano akimkimbilia na kumkumbatia.
Huku alionesha kufurahi sana kumuona.
Kupata meendelezo bonyeza hapa
Hadithi hii imendaliwa na
kuandikwa na JACQUELINE
JOHN.
Mwimbaji
na mtunzi wa nyimbo, mashairi, Hadithi (simulizi) na ngonjera.
Mawasiliano:
Whatsapno.
>>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.
Na,
Imehaririwa
na MIGONGO ELIAS. Mhariri.
Mawasiliano:
Whatsapno.
>>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.
GeT tO tHe NeXt LeVeL!
Kama
umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kujifunza na kuboresha
zaidi.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Chey · 90 weeks ago
Elias Migongo · 90 weeks ago
Pearson Mzunde · 89 weeks ago
Editrini kazi anayo
Atamwambia nn Edwini mumewe....
Nawakubali sana mtunzi na mhariri wetu
Njooni mchukue Pepsi big 😋🍷🍷
Migongo · 89 weeks ago