MAAJABU YA AKIBA

SEHEMU YA TISA.
Ilipoishia...
Niambie
basi unamaana gani, Elvine alipiga magoti na kuanza kulia.
kusoma sehemu iliyopita bonyeza hapa
Elvila hakujibu chochote bali alipotea
ghafla kama upepo. Elvine alishituka maana hakuelewa sehemu ambayo
Elvila kapotelea. Elvine alikaa kitandani kwa muda huku akiwaza cha kufanya.
Ilipofika jioni alitoka nje na kuanza kufanya kazi ya kutembelea nyumba za
jirani na ile hoteli huku akishuhudia watu habari za Yesu.
Alipofika kwenye nyumba moja alimkuta
mtoto mmoja amelala anaumwa sana. Na yule mtoto
alionekana naweza hata kuongea. Mama yake baada ya kugundua kuwa Elvine ni
mtumishi wa Mungu alianza kulia na akapiga magoti kwa Elvine huku akilia.
"Wewe si mtumishi wa Mungu mchungaji?
Tafadhari sana naomba msaidie mwanangu, najua nyie walokole mnaponyaga watu.
Mwanangu mimi kalogwa tena na mama yangu, yaani bibi yake baada ya mimi kukataa
kwenda kumfanyia matambiko mtoto wangu. Na sikutaka afanyiwe matambiko maana
sijui hayo matambiko yao yanamaana gani, niliogopa wasije
wakamfanya mwanangu mchawi. Sasa nilipokataa tu
mama alisema
atanikomesha, na tangu hapo mwanangu hajawahi amka hapo kitandani na anawiki
mbili sasa."
Maelekezo ya yule mama yalimfanya Elvine
amuonee huruma sana yule mtoto. Lakini
akawaza afanye nini. Aliwaza yule mama alikuja akamshika miguu na akasema hatoruhusu
Elvine atoke pale ndani kama mwanaye hajapona
maana ni mtoto wake wa pekee aliyenaye na mumewe alikwisha fariki.
"Mmmh! Huyu mama vipi tena mbona
ananitisha"Elvine aliwaza moyoni.
"Mama mimi sio mponyaji. Mponyaji
ni Mungu"
"Hapana mimi naimani unaweza
kumfanya mwanangu apone, naomba sana mchungaji, mwanangu hana hatia"
Elvine alihisi kuchanganyikiwa,
akamsogelea yule mtoto na kuanza kumuombea. Aliomba masaa mawili lakini hakuna
kilichotokea na mwisho akawa amechoka sana. Alitaka akimbie lakini yule mama
hakutoka hata dakika moja na alikuwa kamkazia macho ili muujiza unapotokea
asiwe wa mwisho kuona. Elvine alikuwa amevaa tai, lakini akaona ile tai
inamkaba sana akaitoa na kuiweka kwenye begi
lake dogo alilokuwa
amebeba. Alihisi anaonewa sana maana aliona hana msaada.
Baadaye akaona hawezi kabisa
kuendelea. Akatoka mbio mule ndani na kuanza kukimbia. Alipofika nje ya ile
nyumba alimsikia yula mama akilia sana. Ghafla alisikia sauti ikimwambia,
"Kwanini unakimbia, imani ya yule
mama inatosha sana kumponya kijana wake, tatizo lipo kwako, ongeza imani yako
na umthibitishe Yesu wako"
Elvine alisimama kama dakika tano pale
nje, kisha akarudi tena ndani. Na wakati huu alikuwa kajiweka tayari
kuhakikisha mtoto anapona ili shetani aaibike. Aliporudi alimkuta yule mama
amemkumbatia mtoto wake. Alimsogelea na kumwambia "Bwana atafanya".
Yale maneno yalimtia moyo sana yule mama
hivyo akafuta machozi na kusogea pembeni. Elvine alimshika mtoto yule kichwani
na akasema tu "walivyovituma kwako, vitawarudia, na Bwana atawanyamazisha
kimya wote wanaokuwazia mabaya. Amka mtoto mzuri ukawaoneshe kuwa yupo Mungu
mwenye mawazo tofauti na wanadamu"
Ghafla
yule mtoto aliamka pale kitandani, tena akiwa mzima kabisa. Hata Elvine hakuelewa vizuri
kilichotokea. Yule mama alifurahi sana. Elvine alipotaka kuondoka yule mama
akamwambia Elvine kuwa anataka kuokoka, Elvine alifurahi sana maana aliona kafanya
jambo ambalo hajawahi kulifanya la kamvua mtu mmoja kutoka
dhambini. Baadaye alipotaka kuondoka yule mama alimwambia Elvine kuwa yupo
tayari kumpa chochote anachotaka lakini Elvine alikataa. Yule mtoto alikuja na
kumkumbatia Elvine na akasema anaomba amuombee ili asilogwe tena. Elvine alimuombea
yule mtoto na akamtabiria baraka nyingi sana yule mtoto, kisha akaondoka kurudi
hotelini.
Alipofika hoteli aliingia chumbani kwake
na akashangilia sana, aliweka muziki wa nyimbo za dini na kucheza sana maana
hakuamini kama Mungu kamtumia yeye kumponya mtu, alicheza na akaimba sana
mule ndani: ukweli hakuwa anajua kucheza lakini alikuwa akirukaruka tu.
Asubuhi alipoamka akajikuta amechoka
sana, na kichwa kikawa kinamuuma sana. Aliamka na kijianda vizuri, baada ya
kunywa chai ya pale hotelini alitoka na kuanza kumtafuta mama yake mtaani kwa
kutumia picha aliyokuwa nayo kwenye simu yake. Alitafuta
sana lakini hakufanikiwa.
Taarifa zilimfika Emiliano kuwa kuna mtu mwingine
anamtafuta Editrin. Alituma watu wakaja kumteka Elvine; Elvine alishangaa
ghafla wakati anaendelea kuzunguka mtaani mida ya saa 1:30 usiku gari
lilisimama pembeni yake na wakatoka vijana wenye nguvu wakamshika na kumuingiza
kwenye gari.
Alichukuliwa na kupelekwa sehemu ambayo
hakuwa anaijua. Alipelekwa kwenye nyumba moja nzuri sana lakini mule ndani
kulikuwa kunatisha sana. Kulikuwa na giza, taa zilipowashwa zilikuwa zikitoa
mwanga hafifu sana. Aliogopa sana maana hakuwa anajua kama anaweza kuwa na ugomvi
na mtu, alihisi labda wale watu wamemfananisha. Alifikishwa kwenye
chumba fulani na kufungwa kamba akiwa kakalishwa kwenye kiti.
Alikaa pale kwa muda mrefu hadi
ilipofika saa 5 usiku ndipo Emiliano alipokuja. Elvine
Alishangaa sana kumuona baba yake wa kambo pale. Emiliano alipofika kabla ya
kuuliza chochote alishika mbao pana sana iliyokuwepo
pale pembeni na
kuanza kumpiga nayo Elvine. Elvine alilia kwa maumivu makali hakujua sababu ya
kupigwa. Baada ya Emiliano kuridhika ndipo akamsogelea na kumuuliza
"wewe ni nani? Na kwanini unamtafuta
mke wangu?"
"Mimi ni mtoto wa Editrin"
"What?"
. "Ndio"
Emiliano alicheka sana na akaanza upya
kumpiga mpaka alipoona Elvine kazimia ndipo aliporidhika na kuondoka.
Elvine alirudisha fahamu siku iliyofuata
baada ya kumwagiwa maji ya barafu. Alipotazama alikutana na sura ya Emiliano
tena mbele yake. Akiwa amekaa kwenye kiti pia
wametazamana.
Alikuwa anaogopa sana.
"Kwahiyo kumbe haukufa?" Emiliano aliuliza.
"Sikudanganyi mheshimiwa Editrin
ni mama yangu, japo tulipotezana muda sana."
Elvine aliongea kwa hofu sana.
"Najua hudanganyi. Siku
zile ulipopotea nikajua ulikufa maana nakuchukia sana"
"Unanijua Mimi toka
zamani"
Emiliano alicheka sana na akaanza kumsimulia
mambo yaliyotokea wakati Elvine
hajazaliwa na wakati akiwa mtoto.
......
*Emiliano alikuwa akimpenda sana
Editrin toka wakiwa shule. Baada ya kurudi kutoka marekani masomoni alikuta
Editrin kaolewa. Hakuwa tayari kukubali kirahisi kumpoteza Editrin hivyo
aliwatuma watu wakaenda kumteka Edwin mume wa Editrin. Alipomteka alimwambia
achaguwe kati ya kumuacha Editrin au kufa. Edwin alikataa kumuacha mkewe hivyo
Emiliano aliagiza Edwin akatupwe kwenye maji akiwa mzima. Walimfunga kamba na
wakamfungia na jiwe kubwa mwilini. Wakati wanaenda kumtupa walichukua
simu ya Edwin na walimvua saa, kisha wakaenda kumtupa
baharini. Baadaye taarifa za kupotea kwa Edwin zilisambaa
sana, na Editrin alimtafuta mumewe sana. Baada ya kusikia kuwa Editrin anamtafuta
mumewake. Emiliano alimteka mtu mwingine na kumchoma moto na akamvalisha saa ya
Edwin na kumtegeshea ile simu ya Edwin mfukoni ili polisi waweze
kumpata.
Emiliano alifanya hivyo ili kumfanya
Editrin ajue kuwa mumewe amekwisha fariki, hivyo aache kumtafuta Edwin. Baada
ya Editrin kumzika mtu ambaye alidhania kuwa ni Edwin, alirudi kukaa kwa baba
yake Mr. Edward. Akiwa pale Emiliano alimfuata Mr. Edward na kumwambia kuwa
yupo tayari kumuoa Editrin kwa gharama yoyote. Na kwakuwa baba yake alikuwa
kashuka kidogo kiuchumi baada ya familia ya Esau kujiondoa ushirika kwenye
kampuni yake baada ya Editrin kuolewa na mtu mwingine, Edward akaona ni jambo
jema kumfanya Editrin aolewe na Emiliano, lakini Editrin hakuwa tayari kuolewa
kwaajili ya mtoto wake yaani Elvine, na kwakuwa alihisi kuwa baba yake
atamuozesha kwa Esau aliamua kutoroka.
Emiliano alichukia sana baada ya kupata
taarifa za kutoroka kwa Editrin lakini hakuwa na namna ya kufanya. Alimtafuta
lakini hakumpata.
Baada ya miaka kama 14, alifanikiwa kufahamu
kuwa Editrin yupo Iringa, na aliweza
kujua suala hilo baada ya kumfatilia Edger kwa muda
mrefu. Hivyo siku ambayo Edger alipafahamu nyumbani kwa
Editrin naye pia aliweza kupafahamu. Alipofanikiwa kupajua mahali wanapoishi Editrin
na mwanaye. Alipanga kumuua Elvine ili apate nafasi ya kumuoa Editrin lakini alikuja kupata
taarifa kuwa Elvine kapotea kwahiyo akawatuma watumishi wake wazidi kumfatilia
Editrin na pindi wakipata taarifa za muonekana kwa Elvine wahakikishe wanamuua
mtoto huyo.
Baada ya siku kadhaa kupita alikwenda
Iringa. Siku aliyokwenda yeye, Eliana pia mama wa Editrin
alikuwa kapata taarifa za binti kuchanganyikiwa hivyo Eliana alitangulia
kufika. Wakati Emiliano anafika sehemu ambayo Editrin alikuwa kahifadhiwa
alimuona mtoto Efraim akiwa kamkumbatia Editrin, akajua ndiyo Elvine kapatikana
kumbe Efraim alikuwa akimuaga Editrin kama mama wa rafiki yake kipenzi Elvine alikuwa akilia kwa uchungu maana alimkumbuka sana
Elvine.
Emiliano aliiwaagiza wafanyakazi kazi wake
wamuue yule mtoto. Siku iliyofuata walimvizia Efraim akiwa anatoka dukani na
kumgonga na gari hivyo Efraim alipoteza maisha. Lakini baada ya Editrin
kuja Dar es salaam ndipo alipogundua kuwa yule mtoto waliomuua sio sahihi.
Na mara hii baada ya Editrin kuja tena
Dar es salaam aliamua kuja kama kijana mwema sana, na haikumgharimu sana hivyo
akatimiza lengo lake kirahisi sana.
Emiliano alieleza kuwa akiwa marekani
alimchumbia binti mmoja wa kizungu, lakini kwakuwa hakuwa anampenda alimuua
baada tu ya yule binti kupata ujauzito wake.
Na pia Esau alimuua maana aliona
anamsumbua mkewake maana Esau pia alikuwa akimpenda Editrin. Esau alikuwa mkorofi sana
lakini alikuwa muoga sana kuua.*
.....
Emiliano alimaliza kusimulia hadithi yake kwa kujitapa kuwa yeye ni mkatili na hana huruma japo watu hawawezi kumgundua
kwakuwa anasura nzuri ya kitumishi.
"Kwani unachotaka kwetu ni
nini?"
"Hakuna chochote, nampenda mke wangu
Editrin, lakini wewe lazima nikuue kabla Editrin hajakupata maana najua
atabadilisha mawazo na atakuwa tayari kuniweka hatari mimi"
"Vipi kama baba yangu
akawa ajafa"
"Nini wewe? Baba yako
nani?"
"Natamani baba yangu angekuwa hajafa ili uje uaibike"
"Haiwezi
tokea"
"Sawa! lakini mimi sina hatia naomba niondoke"
"Leo
hutoki hapa"
"kwanini?"
"Hutakiwi kuishi wewe Mr pastor, maana mama yako alikuwa anasema
mtumishi wake umepotea, hahahhah!"
"Natoka hapa leo baba mdogo"
"Hutoki
Elvine"
"Natoka,
na nikitoka nitahakikisha nakufunga wewe"
"Hivi
unajiamini nini wewe kijana"
"Mungu
hawezi kuruhusu nife wakati kazi yake sijaitimiza, hata kama iwaje hapa
nitatoka tu",
Emiliano
alipata hasira sana, hivyo akawagiza watu wake wampige sana Elvine. Elvine
alipigwa hadi akazimia tena, Emiliano aliwaachia maagizo watu wake kuwa wasimuue
kwanza mpaka kesho atakapokuja tena, kisha akaondoka.
Usiku
Elvine alishituka na akasikia mtu akimwambia "haya ondoka sasa".
Alishangaa maana alijikuta kasimama mlangoni na hana kamba, hakujua hata
kafikaje pale mlangoni. Alifungua mlango akataka kutoka lakini ghafla wale
majambazi wakamsikia,
"Simama hapo, unaenda wapi? Na kwanza umejifunguaje?" Wale
walinzi walishangaa kidogo naye akawa anawashangaa maana walikua na siraha za
moto hivyo akaogopa kukimbia maana alijua atashambuliwa. Ghafla wakatokea watu
wanne warefu sana waliovaa mavazi ya rangi nyeupe iliyong'aa sana pia walikuwa
na mapanga ya moto, wakamzunguka Elvine.
Wale watu
waliogopa sana mmoja akapiga risasi lakini cha ajabu ni kuwa ile risasi ilibadilika
na kuwa ua jeupe kwahiyo lilipofika kwa Elvine lilimpiga lakini kwakuwa ni ua
hakuumia. Wale watu walikimbia kwa kupitia madirisha huku wakipiga kelele za
hofu. Elvine hakuwaona wale malaika hivyo hakujua kwanini wale watu wamekimbia
ma wala ile risasi hakuiona bali alisikia mlio tu, alipoona wale watu
wamekimbia na yeye akaanza kukimbia.
Ile nyumba haikuwa mbali na barabara hivyo akafika barabarani lakini kwa
yale maumivu aliyokuwa nayo hakuweza kukimbia zaidi, alidondoka katikati ya
barabara, akiwa pale alisikia sauti ya mama mmoja kwambali sana ikimwambia
"Kijana wangu nini shida amka! Nini kimekukuta? Haa! Mungu wangu.
Mwanasheria!! hebu tumbebe huyu tumuwaishe hospitali kwanza, maana nahisi
kavamiwa na vibaka wa mji wetu huu...."
Sehemu ya kumi itaendelea >>>>>.
Usikose kufuatilia.
kupata mwendelezo wake bonyeza hapa
Hadithi
hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.
Mwimbaji
na mtunzi wa nyimbo, mashairi, Hadithi (simulizi) na ngonjera.
Mawasiliano:
Whatsapno.
>>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.
Na,
Imehaririwa
na MIGONGO ELIAS. Mhariri.
Mawasiliano:
Whatsapno.
>>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.
GeT tO tHe NeXt LeVeL!
Kama
umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kujifunza na
kuboresha zaidi.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Pearson Mzunde · 91 weeks ago
Mara ghafla Mwanasheria aiseee
Nasubiri sehemu ya 10😋😋😋😋😋
Erick Eliah · 89 weeks ago
Elias Migongo · 89 weeks ago
Migongo · 89 weeks ago