MAAJABU YA AKIBA

SIMULIZI
YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”.
SEHEMU YA NANE.
Ilipoishia....
Walipokumbuka
hili wote walicheka. Wakati huo kumbe mama alikuwa mbele yao. Akawauliza
"nyie maadui wawili mnafanya nini sasa hivi hapa nje na usiku wote
huu?"
Walishituka sana na wakawa wanawaza namna ya kujitetea..
Sasa inaendelea..
Kama hujasoma sehemu ya saba bonyeza hapa
"Mama
usituelewe vibaya tulikuwa tunaagana tu, kwahiyo nilipomkuta Elimina hapa
nikaona nimuage" Elvine alieleza.
"Na
wewe Elimina ulikuwa unafanya nini nje saizi usiku?"
"Nilikuwa na...."
"Alisema anajisikia vibaya
kidogo kwahiyo anapunga upepo"
"We Elvine vipi mbona
unamsemea kwani yeye hawezi kujieleza?"
"Kwanza nyie mmeanza lini
kuongea, nyie si mnatuigizia mmenuniana?"
"Mama samahani, umeelewa
vibaya, mimi naomba nikalale tu" Elimina alisimama kisha
akaingia ndani kulala.
Mama
alitabasamu tu kisha akamtazama Elvine. Wote wakatabasamu.
"Usijali
kijana wangu nilikuwa nawatania tu, napenda muwe na amani, lakini pia kwa
kipindi ulichokuwa hapa nimejikuta nakupenda sana mwanangu. Na ninakuombea sana
ukafanikiwe kumpata mama yako"
"Asante
sana mama."
Asubuhi Elvine alikuwa tayari kwa safari,
hivyo Elimina alimsindikiza stendi Elvine. Wakiwa wanasubiri gari, ghafla yule
baba anayefanana na Elvine alikuja na kusimamisha gari karibu yao.
"Hey Elvine unarudi
nyumbani China nini?"
"Hapana,
naenda apo Dar, father!"
"Waooh! Sio mbaya kama nitakupa
lifti maana pia naelekea huko."
Elvine alifurahi sana , kwasababu ya
ile furaha, alijikuta bila hata ya kuamuaga vizuri Elimina,
alichukua begi lake dogo alilokuwa amebeba na kuingia kwenye gari. Elimina
alijisikia vibaya sana. Hivyo naye akaondoka kwa hasira.
Wakati gari inaanza kuondoka Elvine
akakumbuka kuwa hajamuaga vizuri Elimina, hivyo aliomba kushuka kwenye mara moja. Alitegemea
kumuona Elimina lakini hakuweza, aliaangaza tena huku na huko lakini aligundua
kuwa Elimina amekwisha ondoka. Alijisikia vibaya pia lakini hakuwa na namna
zaidi ya kurudi kwenye gari na safari ikaanza.
Wakiwa kwenye gari Elvine alitamani sana
kujua jina la baba yule, hivyo akawa anamsumbua kwa maswali.
"Elvine kijana wangu,
kwanini unataka kujua jina langu?"
"Nothing, napenda tu!"
"Si
nilikwambia uniite pacha au baba? *
"Ni
kweli lakini ingekuwa vizuri kama ningejua pia."
"Sawa, naitwa Edu!"
"Ooh! Na ilikuwaje
akapoteana na huyo unayemtafuta."
"Ooh! Ni stori ndefu, ila
usijali nikimpata nitakwambia"
Waliendelea na stori mbalimbali za kuhusu
maisha. Walifika Dar es salaam mchana. Elvine alisema anakwenda kumuona
mama yake anayekaa maeneo ya "Mlimani city". Yule
baba alimpeleka Elvine Mlimani city kisha
wakaagana.
Elvine aliposhuka alitafuta hotel na
kwenda kupumzika. Aligundua amebakiwa na kiasi kidogo cha pesa. Hivyo alipokuwa
pale hotel alipiga simu kwa baba yake Mr. Ezhu yang wa China na kumueleza hatua
aliyofikia na kisha akamueleza shida yake. Ezhu yang alituma fedha haraka sana.
Lakini alimwambia kuwa Elvila analia sana maana anajihisi mpweke sana pindi
akitoka shuleni. Elvine aliuliza kwanini Elvila hajawahi kumtafuta yeye hata kwenye simu? na mara nyingi alipokuwa akimtafuta Elvila alikuwa
hapokei simu yake?, lakini Ezhu yang akamwambia Elvila hataki kusikia sauti bali
anahitaji kumuona Elvine kaka yake kwa macho,
na anasema Kama kweli Elvine anampenda basi aende kumuona. Elvine akaahidi kuwa
baada ya kumpata mama yake atakwenda China kuwasalimia.
Siku iliyofuata Elvine alianza kutafuta
nyumba ya Emiliano, lakini haikuwa rahisi sana. Alitafuta kwa muda wa
siku mbili bila mafanikio.
Siku ya tatu akiwa amesimama pembeni ya
nyumba moja ya kifahari sana akiwaza namna ya kuingia aliona gari inaingia
kwenye ile nyumba. Alipotazama ndani alimuona mama yake, Emiliano pamoja na
Emily mdogo wake Emiliano.
Kitendo cha kumuona mama yake,
Ilikuwa kama kapigwa ganzi na akashindwa hata kusogea,
aliishia
kushangaa. Gari ile iliingia ndani. Elvine alijikuta analia na akaogopa hata
kuingia ndani. Alibaki pale nje kwa muda huku akiwa hajui cha kufanya.
Aliamua kuondoka ili akajipange namna ya
kuingia kwenye ile nyumba na kujitambulisha. Alirejea kwenye hoteli aliyokuwa
anakaa huku akiwa na uchungu sana maana alijua kabisa kuwa sio rahisi mama yake
kumtambua yeye.
Kesho yake aliamka mapema sana na
akajiandaa vizuri, kisha akaelekea kwenye ile nyumba. Alipofika nje alibisha
hodi kupitia kengere ya hodi pale mlangoni. Geti lilijifungua lenyewe na mbele
yake alikutana na walinzi matano.
"Tukusaidie nini kijana?"
"Samahani mwenye nyumba
yupo?"
"Nani?"
"Madam Editrin"
"Unaahadi naye?"
"Hapana ila nahitaji
kumuona"
"Ondoka haraka usijeukabeba kesi"
"Kwanini?"
Akiwa haelewi kinachoendelea Emiliano
alitoka ndani akiwa na polisi wawili. Emiliano alipofika pale alimshangaa sana
Elvine, akamuuliza "we nani?" Elvine alianza alisema anahitaji
kuonana na Editrin kwakuwa anajambo la kumwambia.
Emiliano aliposikia hivyo aliwaambia wale polisi wamkamate Elvine maana atakuwa
anajua kitu. Elvine hakuelewa kwanini kakamatwa.
Alipofika polisi aliuliza kosa lake.
Ndipo alipoambiwa kuwa Emiliano kuchanganyikiwa baada ya mkewe kupotea usiku
ulipopita.
"Kapotea?
Kivipi yani? Jana si walikuwa pamoja? "
"Uliwaona
wapi?"
"Pale
kwao"
"We
ulikwenda kufanya nini. We ni mpelelezi wa maisha ya watu?"
Elvine
alikosa jibu. Yule afande akamwambia "maneno yako yatakufunga dogo, usije
ukatoa maelezo kama hayo polisi, sema mimi nakuona kama mtoto wa Mungu hivi,
yaani huna kosa lakini hiyo sentensi uliyoisema inautata kidogo. Ila usijali
mimi nimekupenda tu, kwahiyo nakutoa hapa halafu Emiliano nitamwambia kuwa
ushahidi unaonesha hauna kosa, ok?"
"Asante
sana... Asante sana aisee.."
Elvine aliachiliwa na kurudi zake hotel.
Alistaajabu sana, kwanini mama yake apotee wakati kama huu.
*. *
* * * * * * *
MASAA
18 YALIYOPITA
Editrin
baada ya kutoka kanisani na mumewe alikuwa kachoka sana, alikwenda chumbani
kupumzika. Mumewe aliaaga anakwenda mahali. Alichelewa sana kurudi. Aliporudi
alioga kisha akapanda kitandani
kulala. Baada ya Emiliano kulala, Editrin aliamka maana
usingizi ulipaa, alipoamka aliamua akafue nguo za mumewe jambo ambalo hajawahi
kulifanya hata siku moja, maana siku zote ni wafanyakazi tu ndiyo wafuaji wa
nguo, nao walikuwa wakifua kwa kutumia mashine za kufulia.
Alizibeba zile nguo hadi sehemu ya kufulia,
kabla hajaanza kuzifua alizikagua mifukoni kuona kama kuna chochote ambacho
kipo kwenye mifuko. Hakuona chochote. Lakini wakati mkono wake upo kwenye mfuko
wa mwisho alihisi mfuko ule umeloa na akagusa kitu mule mfukoni.
"Mmh! Emiliano naye anawekaje vitu
mfukoni hadi mfuko unalo......" Kabla hajamaliza alipigwa na mshtuko baada
ya kutoa ule mkono na kugundua kuwa ni kidole cha mtu
chenye damu mbichi kabisa.
Alitupa lile koti pembeni yake, aliogopa
mno, akajiziba mdomo ili asitoe sauti, alijiuliza
maswali mengi mno moyoni kwa dakika chache tu. Alitoa machozi, akajuta,
akashangaa, anajilaumu, akajing'ata vidole kwa uchungu mkubwa. Aliona
pale ndani sio sehemu salama kwake. Akiwa anawaza kukimbia aligundua kuwa
haitokuwa rahisi sana maana ni usiku wa saa 6:30, kwahiyo walinzi wangemzuia.
Alikwenda kwenye store na kujifungia huko.
Usiku wa saa 8 Emiliano alishituka kutoka
usingizini, alishangaa baada ya kugundua kuwa Editrin hayupo. Alitoka sebuleni
huku akiita, hakuna aliyejibu. Aliita sana lakini kulikuwa kimya, alipofika
kwenye chumba cha kufulia nguo alishangaa kuziona nguo zake zimetupwa pale
chini hivyo akagundua kuwa Editrin kaona kile kidole kwenye suti yake.
Alishituka sana, akaondoka mpaka kwenye
chumba cha mfanyakazi mmoja aliyeitwa Ekhi. Ekhi alikuwa ni mfanyakazi wa muda
mrefu sana mule ndani na ndiye aliyekuwa mfuaji wa nguo zake siku zote. Ekhi
alikuwa anajua siri nyingi za bosi kwahiyo alikwisha zoea kuna vitu vya ajabu
sana.
Wakati huo Emiliano anakwenda kwa Ekhi,
Editrin pia aliamua kutoka kwenye kile chumba ili aende kwa Ekhi kumuuliza
vizuri kuhusu alichokiona kama kimewahi jitokeza
kabla.
Alipotoka tu kwenye kile chumba alimuona Emiliano anaingia kwenye chumba cha
Ekhi. Alinyata na kusimama mlangoni kusikiliza.
Alisikia
Emiliano akimfokea Ekhi maana alikwisha mwambia kuwa akirudi tu kutoka kazini,
Ekhi anatakiwa kuchukuwa nguo na kwenda kuzifua haijalishi saa ngapi wala muda gani.
Ekhi alijitetea kuwa siku hiyo alipitiwa na usingizini mapema sana, kwahiyo hakujua kama bosi karudi. Mwisho Editrin alisikia Emiliano akisema
"usinilaumu mimi, haya ni makosa yako na hii ndiyo adhabu yako". Ekhi
alipiga kelele lakini hazikuwa zinafika mbali kutokana na uwepo wa 'singbord'.
Editrin alisikia mlio wa lisasi akiwa pale mlangoni, na ndipo alipogundua kuwa
mumewe ni mkatili kama mnyama. Hakutegemea wala kuwaza
hata siku moja. Alikuwa akimuamini sana Emiliano kwa namna alivyokuwa mpole na
mkarimu.
Alitoka mbio pale mlangoni na akawahi
getini ambako aliwakuta walinzi wamelala. Alimshukuru sana Mungu maana ilikuwa
rahisi sana kutoroka. Alifanikiwa kukimbia pale ndani na kwenda kusikojulikana.
Emiliano alituma walinzi wamtafute kila
mahali lakini hawakumpata usiku ule. Emiliano alichanganyikiwa maana aliwaza
mambo mengi sana hasa juu ya hatari inayokuja baada ya Editrin kukimbia.
Asubuhi alipiga simu kwa mama yake mkwe
Eliana, lakini aliambiwa kuwa Editrin hajafika nyumbani. Alitoa taarifa
polisi, hivyo polisi walikuja pale nyumbani asubuhi kuchukua maelezo. Aliwaambia
polisi kuwa mkewe amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha kwahiyo anaomba
msaada wa kumtafuta.
* * * * * * * * * *
Elvine baada ya kutoka polisi alifika hoteli
na akaanza kumuomba Mungu kwa uchungu sana. Akiwa anaomba alisikia
sauti ikimwambia kuwa mama atamuona, lakini kwanza kuna jambo anatakiwa
kulifanya kwanza.
Alijiuliza ni jambo gani hilo. Aliambiwa
aondoke pale ndani na akazunguke kwenye nyumba za karibu kushudia. Hakuamini na
alihisi kaanza kuwa kichaa.
"Hivi ni sauti ya Mungu kweli? Yaani
mama yangu kapotea halafu mimi nikawashuhudie watu! Naenda kuongea nini kwanza?
Kwanza mimi mwenyewe ni mchanga kiroho, nimeokoka hata mwezi sijamaliza"
alijiongelesha sana baadaye akasema "mimi siwezi kutofautisha sauti ya
Mungu na mapepo kama huyu ni Mungu kweli, basi amshushe malaika hapa ndipo
nitaamini vinginevyo siendi mahali mimi"
Akiwa katika kusema maneno hayo ghafla
alihisi kaguswa na mtu begani na mtu aliyekuwa nyuma
yake. Alianza
kuogopa na akaanza kujisemea kimoyo moyo "eeh, Mungu mimi nilikuwa natania
tu! Nani huyu sasa!". Aliwaza sana, kwanza
yupo hoteli, chumbani anakaa peke yake, hana mwenyeji, hajaagiza chochote, na
mlango kafunga na funguo.
Elvine alikuwa anaogopa hata kugeuka nyuma,
japo ulikuwa ni mchana lakini yeye alihisi kama ni usiku na yupo pekeyake
kwahiyo hana msaada.
"Geuka na unitazame"
"We...
Ni... nani?
"Usiogope,
Ukigeuka
utanijua"
Kwa woga aligeuka, alishangaa kumuona
Elvila wa utotoni tena akiwa bado mtoto vilevile.
"Wewe......!!"
"Nimekuja tena
kwako, si umehitaji kuniona?"
"Nani? Mimi? Akha!"
"Mungu anakupenda sana
Elvine"
"Najua"
"Kwanini sasa unakuwa mkaidi?"
"Aaa
hapana, kwani nimesema siendi sasa? Naenda mbona. naenda mimi tena sasa
hivi."
"Kaokoe
maisha ya mtu kwanza, kuhusu yakwako Mungu atayasumbukia. Mama yupo sehemu
salama."
"Niahidi kitu"
"Sawa, najua unachotaka kusema, baada ya kazi hii, basi utampata
mama yako, lakini..."
"Lakini nini?"
"Hutokaa naye mapema hivyo"
"Kwanini?"
"Kwasababu wewe ni mkaidi na hiyo ndiyo itakuwa adhabu yako"
Kwamba, mnataka kumuua mama yangu au? Niambie vizuri, sijaelewa hapo!,
Kama anakufa basi na mimi sitowasikiliza tena, kweli nawaambia na wala sitosali
tena.
"Mawazo unayoyawaza wewe, sio Bwana anayokuwazia wewe" Elvila
alisema huku kamkazia macho Elvine
Niambie basi unamaana gani, Elvine alipiga magoti na kuanza kulia
Sehemu ya tisa itaendelea ijumaa
>>>>>. Usikose kufuatilia.
kusoma mwendelezo wake bonyeza hapa
Hadithi
hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.
Mwimbaji
na mtunzi wa nyimbo, mashairi, Hadithi (simulizi) na ngonjera.
Mawasiliano:
Whatsapno.
>>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.
Na,
Imehaririwa
na MIGONGO ELIAS. Mhariri.
Mawasiliano:
Whatsapno.
>>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.
GeT tO tHe NeXt LeVeL!
Kama
umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kujifunza na
kuboresha zaidi.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Cheyo · 93 weeks ago
Migongo Elias · 93 weeks ago
Pearson Mzunde · 93 weeks ago
Elvine anatakiwa kumuomba msamaha Elimina 😃
Migongo Elias · 91 weeks ago