Posts

Showing posts from June, 2023

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23. Ilipoishia...... Alipofika nje, alimkuta Elimina katahamaki sana tena anahasira sana.  "Umefanya nini Elvine? Elimina aliuliza kwa ukali sana tena hadi macho yalikuwa mekundu kama damu kwaajili ya kujaa hasira.... Swali; kwanini Elimina anahasira? Na Elimina huyu anasiri gani na nyumba iliyoungua moto? Kusoma sehemu ya 22 bonyeza hapa   Sasa inaendelea...... Elvine alikuwa anatetemeka  kwa hofu ya yale anayoyaona lakini alistaajabu kuona ni kama mkewe hajali sana kuhusu yeye. Alimtazama kwa makini sana mkewe akiwa anajaribu kutafakari kwanini anaonekana kuwa na hasira juu yake. Elimina akajishitukia "Hey, wewe! Nini sasa unanitazama hivyo?" "Nakutafakari sipati majibu!' "Nimefanyaje kwani?" "Hamna ila sijajua kama umenihofia mimi au hilo swali lako linamaana gani? "Elvine baba sina maana hiyo uliyoelewa wewe kabisa. Shida yangu mimi umefanya nini mpaka unataka kuhatarisha maisha Yako namna hii. Hujui namna ga

SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU “HATIMA YA KIMUNGU”. >>SEHEMU YA TATU.

Image
  SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU “HATIMA YA KIMUNGU”. >>SEHEMU YA TATU.   Ilipoishia....,.. Editrin baada ya kutulia alimsimulia kisa kizima mama yake tangu alipotoroka kwao, hadi kufikia hapa alipo na namna amba v yo El vine alivyopotea. Eliana alionesha kuumia sana kwani kwa namna nyingine tunaweza kusema yeye ndi y e aliyekuwa bibi wa mtoto yule. Wakiwa wanaendelea na mazung u mzo y ale Editrin akaanza kukumbuka kisa chote kilichomkuta kwenye maisha yake hata kupelekea yeye kutoroka kwao Dar es salaam na kuamua kuja kuishi Iringa.......   Kama hujasoma sehemu ya kwanza na ya pili bonyeza hapa. Sasa inaendelea...,.... Editrin alizaliwa Katika familia ya kitajiri sana. Baba yake alikuwa akiitwa Mr. Edward na mama yake aliitwa Eliana . Katika familia yao walizaliwa watoto wawili tu! ambao ni Editrin na Edger. T angu utoto wao walipendwa sana na wazazi wao wote wawili. Editrin na k aka yake Edger hawakuwahi kuyajua maisha ya shida ma an a baba yako alikuwa na pesa s

JIFUNZE KUJIFUNZA (PART 1)

Image
JIFUNZE KUJIFUNZA (PART 1) Siku moja nikawa nimetulia natafakari   nikawaza na kuwazua kuhusu binadamu. Nikaona kuwa ni kawaida kabisa kwa binadamu yeyote kuzaliwa, kulelewa, kwenda shule au kutokwenda kabisa, kuoa/kuolewa wakati mwingine kutokuoa/kuolewa kabisa, kufanya kazi, kuzeeka na hata kufa. Lakini unaweza kufa hata kabla ya wakati wa kuzeeka kwako. Nikagundua kuwa katikati ya utoto na uzee/ kifo. Mwanadamu huyu atajikuta amefahamu vitu vingi sana. Aidha kwa kujifunza mwenyewe kwa kuona kusikia au kwa njia yeyote ile, au kwa kufundishwa na watu wengine nyumbani au kwa kwenda shule. Kwa kifupi   tumejifunza au tumefundishwa mambo kemkemu. Ukienda shule za St. Kayumba utafundishwa habari ya 3K   yaani, kusoma, kuandika, na kuhesabu. Na, ukibahatika ukapanda magari ya njano utafundishwa kuhusu, 3R s yaani, Reading, wRiting, and aRithmetic. Hata kwa wale hawakukanyaga kabisa umande wa asubuhi nao wamejikuta wamejifunza vitu vingi sana huko nyumbani na mtaani pia. Kwahiyo utaon

Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.