HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23. Ilipoishia...... Alipofika nje, alimkuta Elimina katahamaki sana tena anahasira sana.  "Umefanya nini Elvine? Elimina aliuliza kwa ukali sana tena hadi macho yalikuwa mekundu kama damu kwaajili ya kujaa hasira.... Swali; kwanini Elimina anahasira? Na Elimina huyu anasiri gani na nyumba iliyoungua moto? Kusoma sehemu ya 22 bonyeza hapa   Sasa inaendelea...... Elvine alikuwa anatetemeka  kwa hofu ya yale anayoyaona lakini alistaajabu kuona ni kama mkewe hajali sana kuhusu yeye. Alimtazama kwa makini sana mkewe akiwa anajaribu kutafakari kwanini anaonekana kuwa na hasira juu yake. Elimina akajishitukia "Hey, wewe! Nini sasa unanitazama hivyo?" "Nakutafakari sipati majibu!' "Nimefanyaje kwani?" "Hamna ila sijajua kama umenihofia mimi au hilo swali lako linamaana gani? "Elvine baba sina maana hiyo uliyoelewa wewe kabisa. Shida yangu mimi umefanya nini mpaka unataka kuhatarisha maisha Yako namna hii. Hujui namna ga

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

 

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

Katika dunia hii ambayo watu wanalaumu ya kwamba vyuma vimekaza, imekuwa ni hulka ya watu wengi kutamani sana kuajiriwa. Walau, mkono uende kinywani tu mengine yatajipa mbele kwa mbele. Ajira imekuwa kimbilio kwa walio wengi. Wasome mamia kwa maelfu wanatembea na bahasha mkononi wakisaka ajira. Wasio na elimu wanataka ajira, wakubwa kwa wadogo, wake kwa waume wanataka ajira, walioko ajirani hawataki kustaafu. Hali kama hii imefanya tatizo la ukosefu wa ajira kuongezeka. 

Nakumbuka kuna tangazo la ajira lilitoka, alikuwa anahitajika mtu mmoja lakini, walio omba maombi hayo walikuwa watu 824. Ikumbukwe hapo anahitajika mtu mmoja tu! Just to give you the pictureKatika hili nikwambie tu kuwa ajira ni chache kama wengi wanavyosema, lakini kazi zipo  nyingi sana kuliko unavyodhani. Sema watu hawataki kufanya kazi ila wanataka kuajiriwa. 

Hiki kitu tutakijadili wakati mwingine lakini, mimi kama mimi siyo kwamba napinga watu kuomba ajira au kuajiriwa hapana! Na wala sipo huko kabisa. Ninachotaka nikuambie  ni kwamba usikubali kuajiliwa kabla hujasoma na kuelewa mambo haya ambayo tutajifunza hapahapa. Hivyo soma kwa makini na uelewe usije ukafanya makosa ambayo watu wengi huyafanya .

Kabla hatujayatazama mambo hayo, napenda kukueleza kuwa unapaswa kujiuliza maswali kama, mimi ni nani? Ajira ni nini? Kwanini unaenda kuajiriwa? Kumbuka kuwa inakupasa kuwa na ndoto, na kwa kawaida kila mtu anayo ndoto lakini anaweza kuwa anaifahamu au haifahamu kabisa. Na kuifikia ndoto elewa kuwa utakutana na vizuizi na changamoto za kila namna. Na nyingi zitakuchelewesha sana. Lakini, pia ni muhimu kufahamu  mshahara ni ambao unaupata kwenye ajira hiyo ni nini?  Mtu mmoja alisikika akisema mshahara ni rushwa anayopewa mtu ilikusahau ndoto yake kwa muda. Lakini pia, ni muhimu kujua ni sababu gani inakupeleka ajirani. Hapa naenda kukupa sababu tatu ambazo zitakusukuma kuingia kwenye ajira na siyo kwenda ili kupata chochote kitu.

Godius Rweyongeza katika kitabu chake cha jinsi ya kufikia ndoto zako. Ameandika sababu tatu ambazo mtu anayetaka kuajiriwa inampasa azitumie . Na, hapa tuna kwenda kuzifahamu sababu hizi kabla hujazama kwenye ajira na kufanya makosa ambayo wengine hufanya. Yaani, nachotaka kusema usiende kutafuta ajira kichwa kichwa na bila sababu yeyote bali tumia hizi kama sababu za wewe kuajiriwa, ambazo ni;

SABABU YA KWANZA: ILI KUPATA UZOEFU NA UJUZI KATIKA ENEO LAKO,

Kwa kawaida mtu anapoajiriwa katika eneo fulani, kadri anavyofanya kazi na kukutana na changamoto tofauti tofauti kazini, anavyofanya na kutatua changamoto hizo, ndivyo anavyo zidi kupata uzoefu na kuongeza ujuzi. Mfano mtu akiajiriwa kama mwalimu, IT, Afisa masoko, mhasibu n.k na akafanya kazi kwa uaminifu na kujituma atapata uzoefu na kuongeza ujuzi wake. Ambapo hatakuwa sawa na mtu ambaye amekaa tu bila kuufanyia kazi ujuzi wake. Hivyo hii inaweza kuwa ni sababu ya mtu kumfanya aaajiriwe ili kuongeza ujuzi na uzoefu katika eneo lake.

SABABU YA PILI:  ILI KUPATA KONEKISHENI.

Kwa kweli tunaishi katika dunia yenye kujuana kwingi. Yaani, connection na, huu ndiyo uhalisia si unajua mafanikio yako yamefungwa kwa watu! Hivyo kadiri unavyo jamiiana na watu wengi hata kufanikiwa kwako itakuwa vyepesi. Hivyo hata katika ajira mtu akiajiriwa bila shaka atakuwa na watu tofauti tofauti, yaweza kuwa wakurugenzi, mameneja, polisi wanasheria, wabunge na wengine kibao. Akifahamiana nao itakuwa ni rahisi sana kwake kuja kuwatumia kuifikia ndoto yake kwa wepesi. Si unajua your network is your networthy! Hata wewe unapoenda kwenye ajira au kama upo kwenye ajira jitahidi kuishi vizuri na watu fahamiana nao, watakuja kukusaidia siku moja katika kufanikisha ndoto zako.

SABABU YA TATU:  ILI KUPATA FEDHA.

Pesa ni muhimu sana katika kufanikisha mambo mengi. Pamoja na hayo kuna watu wana ndoto na malengo makubwa sana, na kuanza kuyafanyia kazi  imekuwa ni changamoto kwai pesa kwao bado ni tatizo. Ingawa unaweza kuanza biashara na kitu chochote kile kihusuyo ndoto yako pasipo hata na pesa. Kwani pesa zitakuja zenyewe tu. Lakini, pesa inarahisiya mambo kama itatumiwa vyema.hivyo hata wewe unaweza kuajiriwa ili kupata walau kiasi kitakacho kusukuma kwenda mbele, pengine kama mtaji, kama. Watu wengi wmeitumia hii nia kupata mtaji na wengine kunogewa na ajira hadi leo wana kula keki ya taifa. Sema ndoto zao ndo hivyo, wamezi terekeza kabisa kwa rushwa ya mshahara. Wewe usiwe mmoja wao. 

Sababu hizi ni muhimu sana ambazo mtu anaweza kuzitumia kwenda kutafuta ajira yaani uzoefu, connection na fedha. Wengi wana enda kuajiriwa kwa sababu ya pesa pekee na hawa ndio huuza ndoto zako mapema sana. Na, wengine huenda na sababu hizi zote lakini wanaishia kunogewa na mshahara. Yatupasa kutambua kuwa ajira zipo kwa wote li kuwa saidia. Na nikushauri unaweza kuzitumia hizi sababu kuajiriwa. Kisha, ondoka kafanyie kazi mipango na malengo yako. Na hapa ukiona umefanya kazi na kukaa kwa muda mrefu sana ajirani tambua kuwa unawazibia watu wengine nafasi. Hivyo ni muhimu kulitambua hili na kwenda kufanya hivyo. Lakini, siyo lazima uajiriwe wewe kama unavyo vitu  hivi vyote yaani, una connection, uzoefu na fedha, huna haja ya kwenda kuajiriwa waweza kuendelea kupambana mdogo mdogo hadi kuufikia ukuu unao utaka katika maisha yako.

Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.

na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.

GeT tO ThE nExT lEvEl!

Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz. Karibu sana ujiongezee thamani yako. 

Kwa mawasiliano;

Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456

Email>> eliasmigongo120@gmail.com.

Facebook>> MIGONGO ELIAS.

LinkedIn>>Migongoe. 

Pinterest>>eliasmigongo.

Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe. 

 

Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.