Posts

Showing posts from April, 2024

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23. Ilipoishia...... Alipofika nje, alimkuta Elimina katahamaki sana tena anahasira sana.  "Umefanya nini Elvine? Elimina aliuliza kwa ukali sana tena hadi macho yalikuwa mekundu kama damu kwaajili ya kujaa hasira.... Swali; kwanini Elimina anahasira? Na Elimina huyu anasiri gani na nyumba iliyoungua moto? Kusoma sehemu ya 22 bonyeza hapa   Sasa inaendelea...... Elvine alikuwa anatetemeka  kwa hofu ya yale anayoyaona lakini alistaajabu kuona ni kama mkewe hajali sana kuhusu yeye. Alimtazama kwa makini sana mkewe akiwa anajaribu kutafakari kwanini anaonekana kuwa na hasira juu yake. Elimina akajishitukia "Hey, wewe! Nini sasa unanitazama hivyo?" "Nakutafakari sipati majibu!' "Nimefanyaje kwani?" "Hamna ila sijajua kama umenihofia mimi au hilo swali lako linamaana gani? "Elvine baba sina maana hiyo uliyoelewa wewe kabisa. Shida yangu mimi umefanya nini mpaka unataka kuhatarisha maisha Yako namna hii. Hujui namna ga

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23. Ilipoishia...... Alipofika nje, alimkuta Elimina katahamaki sana tena anahasira sana.  "Umefanya nini Elvine? Elimina aliuliza kwa ukali sana tena hadi macho yalikuwa mekundu kama damu kwaajili ya kujaa hasira.... Swali; kwanini Elimina anahasira? Na Elimina huyu anasiri gani na nyumba iliyoungua moto? Kusoma sehemu ya 22 bonyeza hapa   Sasa inaendelea...... Elvine alikuwa anatetemeka  kwa hofu ya yale anayoyaona lakini alistaajabu kuona ni kama mkewe hajali sana kuhusu yeye. Alimtazama kwa makini sana mkewe akiwa anajaribu kutafakari kwanini anaonekana kuwa na hasira juu yake. Elimina akajishitukia "Hey, wewe! Nini sasa unanitazama hivyo?" "Nakutafakari sipati majibu!' "Nimefanyaje kwani?" "Hamna ila sijajua kama umenihofia mimi au hilo swali lako linamaana gani? "Elvine baba sina maana hiyo uliyoelewa wewe kabisa. Shida yangu mimi umefanya nini mpaka unataka kuhatarisha maisha Yako namna hii. Hujui namna ga

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 22.

Image
HATIMA YA KIMUNGUSEHEMU YA 22 Ilipoishia..... "Kulia sio suluhu ila nenda kamlilie Mungu wako, usipende kutoa machozi kama hivi mwanadamu mbele ya asiyeweza kukusaidia, tuungane kumsaidia japo ni mtihani ila wewe kama mwanamke kaushinde.... Kusoma sehemu ya 21 bofya hapa. Sasa inaendelea.... Elimina alilia sana na ndipo aliposhtuka na kujikuta yupo kanisani watu wanamuombea kwenye chumba cha maombi. Aliutazama mwili wake akahisi maumivu makali sana jambo hilo likamfanya agundue kuwa kanisa lilikuwa likimkemea mapepo. Aliwatazama na akajikuta kama anafikiria namna walivyopambana kumuombea Kwa muda mrefu huku wakimgeuzageuza ili kutoa mapepo yaliyomfanya kuzimia, aliwatazama sana watumishi wenzie na mwisho akajikuta anatabasamu maana kicheko kilikuwa kimembana lakini akajizuia kwa tabasamu. Walipoona anatabasamu wakajua tayari sasa mapepo yamejidhihirisha wazi wazi baada ya kujificha muda mrefu kwa kujifanya hayaongei. Wakataka kuanza kukemea tena. Sasa wakati huu Elimina akaiona ha

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA21

Image
         HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 21. Ilipoishia...... Elvine baada ya kula alihisi kizunguzungu sana lakini badae alirudi kwenye hali yake ya kawaida. Yeye alijihisi labda kuzungumza kuhusu maji yaani hanywi maji mengi. Wakati kakaa pale kwenye kile kigoda alianza kuhisi usingizi na mwisho alijiona kashachukuliwa yupo mahali pengine asipopajua.,.... Kusoma sehemu ya 20 bofya hapa.  Sasa inaendelea.... Alijikuta yupo mtoni kwenye mtumbwi usiojulikana unaenda wapi ila unajiongoza wenyewe na maji ya mto yalikuwa machafu sana, pia hali ya hewa ni mbaya na baridi kali mno. Alitazama pande zote na asione mtu yoyote karibu yake, kulikuwa na ukungu na giza hafifu kama la jioni. Hakuweza kuona umbali mrefu kutoka alipokuwa na akawa anahisi kana kwamba macho ni mazito sana hayataki kuona yale yanayojiri pale.  Alipata hofu kidogo na akawa na maswali moyoni mwake. Alitamani angaliuliza mtu kuwa yu wapi na anakwenda wapi lakini hakuweza. Wakati anajiuliza akatahamaki baada ya kuona mamba wengi

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 20.

Image
HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 20. Ilipoishia.....  Lakini Elvine alikuwa anaipenda kazi yake, anapenda kuitwa meneja, anapenda kuonekana bosi, sasa akiwaza kuhusu kuwa mchungaji anaona kama hailipi kabisa japo zamani alikuwa anapenda sana kuwa mchungaji. Alijiwazia mwenyewe kisha akaamua kuondoka pale sebuleni maana aliona anazidi kuchanganywa na maneno ya mkewe. Aliingia chumbani kwake ambako alishangazwa baada ya kumkuta mtoto mchanga analia kitandani kwake...... Kusoma sehemu ya 18 bonyeza hapa. Sasa inaendelea.... "Mmmh!" Elvine alisikika akiguna kwa umakini sana alianza kumsogelea yule mtoto aliyemkuta kalazwa kitandani. Alikuwa ni mtoto mchanga sana ambaye anakadiliwa kuwa na miezi kama mitatu au minne hivi. Alikuwa na wasiwasi maana alitamani kujua mtoto kafikaje fikaje pale ndani wakati anamsogelea akiwa katika hali ya umakini sana alishtuka sana baada ya kuguswa bega Kwa nyumba na mtu.  "Yesu kristo! Kwa jina la Yesu toka pepo!!!" Elvine alikemea kwa kulalami

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 19

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 19 Ilipoishia.... Katikati ya ule moshi walionekana watu wawili wanatembea kuingia ndani ambao walikuwa mwanaume na mwanamke, wenye sura za tabasamu zilizojaa chuki, mateso pasipo huruma na furaha Kwa wengine. Lakini ni ajabu maana walipoingia walikuwa   watu wanaofahamika sana na ni ajabu kuwafahamu.... kusoma sehemu ya 18 bonyeza hapa Inaendelea.... Alionekana binti mmoja mrembo kapendeza mno kwa mavazi yake mekundu kwanzia juu mpaka chini. Yaani, gauni refu jekundu lililokuwa likitambaa mpaka chini renye maua ya kuvutia sana, viatu vyake virefu vyekundu ambavyo kama hujawahi vaa viatu virefu basi viatu vile huwezi kuvitumia kwa majaribio kabisa, kichwani alibana nywele zake ndefu kwa kibanio chekundu na mikononi alivaa bangili mbili za rangi nyekundu pia, ni wazi kusema kwamba alipendeza mno na hakuvaa kimaskini hata kidogo maana mavazi yake kwa makadirio ya haraka labda yalikadriwa laki tano au sita ili mtu kuyamiliki. Alikuwa kashikwa mkono

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA 18.

Image
HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA KUMI NA NANE. Ilipoishia.......  Siku moja wakiwa nyumbani Elvine alihisi nafsi yake kama ipo kwenye shida sana. Yaani inahangaika, na akakosa amani kabisa. Hakuweza kumweleza pertnar wake maana hakuwepo. Kwani alikuwa  dukani. Aliona bora akalale, ili atulize akili. Akiwa  mbioni kuusaka usingizi pale kitandani aliona popo kaingia chumbani na kuanza kurukaruka huku na huko. Alipata hasira maana aliona kapoteza usingizi wote. Aliamka na kutafuta mbao moja pana ambayo alitaka kuitumia kumchapa yule popo.  "Yaani wewe kamnyama umenikosea sana maana mimi nimechoka halafu wewe unataka kunisumbua, Sasa subiri uone kazi....  Kusoma sehemu ya 17 bofya hapa. Sasa inaendelea ....... Alimuongelesha popo kana kwamba anamsikia. Alipotaka kumpiga popo yule alikwepa. Wakaanza kufukuzana pale chumbani maana popo alikuwa mjanja sana. Elvine alijitahidi sana kumpiga lakini alishindwa mpaka akachoka. Alipochoka yule popo aliondoka kwa kupita dilishani kana kwamba alikuwa

Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.