HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26. Ilipoishia.......... Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti... Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa. Sasa inaendelea......, Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 22.

HATIMA YA KIMUNGUSEHEMU YA 22

Ilipoishia.....

"Kulia sio suluhu ila nenda kamlilie Mungu wako, usipende kutoa machozi kama hivi mwanadamu mbele ya asiyeweza kukusaidia, tuungane kumsaidia japo ni mtihani ila wewe kama mwanamke kaushinde....

Kusoma sehemu ya 21 bofya hapa.

Sasa inaendelea....

Elimina alilia sana na ndipo aliposhtuka na kujikuta yupo kanisani watu wanamuombea kwenye chumba cha maombi. Aliutazama mwili wake akahisi maumivu makali sana jambo hilo likamfanya agundue kuwa kanisa lilikuwa likimkemea mapepo. Aliwatazama na akajikuta kama anafikiria namna walivyopambana kumuombea Kwa muda mrefu huku wakimgeuzageuza ili kutoa mapepo yaliyomfanya kuzimia, aliwatazama sana watumishi wenzie na mwisho akajikuta anatabasamu maana kicheko kilikuwa kimembana lakini akajizuia kwa tabasamu.

Walipoona anatabasamu wakajua tayari sasa mapepo yamejidhihirisha wazi wazi baada ya kujificha muda mrefu kwa kujifanya hayaongei. Wakataka kuanza kukemea tena. Sasa wakati huu Elimina akaiona hatari inayoenda kutokea baada ya watu wale kupambana na kitu ambacho hakipo. 

"Hey! Wapendwa ni mimi Elimina, ni mimi kabisa tena Wala sina hata mapepo. Ila nilikuwa mahali" neno nilikuwa mahali likawa tatizo kulisikia mbele ya wainjilisti na wanamaombi wenye imani kali.

"Binti tuambie ulikuwa wapi na ulikuwa unafanya nini?"

" Kusema kweli sikumbuki nilikokuwa ila nachojua nilikuwa na binti mfano wa malaika"

Kijana mmoja akawaambia wenzie, hivi nyie mnapata wapi muda wakuongea na mapepo kwa namna kama hiyo. Usimpe adui nafasi hata bible inasema. Elimina tuambie ulikuwa wapi? Wewe ni ajenti?, jibu mara moja kabla hatujashusha moto wa Bwana ukuangamize" yule kijana akaongea kwa ukali kidogo ili kumtisha Elimina.

Sasa wakati huu Elimina akajikuta anashindwa kujizuia kicheko kilichoubana moyo wake. Akajikuta anasahau hata mazito yanayompata Elvine mumewe. Akaangua kicheko, kicheko kisicho na kizuizi. Sasa hapa wote wakamwamini yule mwinjilisti kuwa Elimina anamapepo makali tena sio wakuhojiana nae yaani wakemee tu mpaka kieleweke.

Wakaanza kumuombea, sasa Elimina akaona awaache tu maana hawawezi hata kumuelewa. Wakati wanamuombea pale kijana mmoja mdogo wa kiume akatoka kanisani akaja kwenye chumba cha maombi. Alipofika alitazama kinachoendelea kisha akasogea mpaka eneo la tukio kisha akampa mkono Elimina na kumwita tena kwa jina lake jambo ambalo lilimshangaza sana. Elimina alimshika mkono yule mtoto na akasimama pale chini na kusogea pembeni. Wale waliokuwa wanaomba walikuwa wanaendelea kukemea hewa pale na wala hakuona kilichotokea. Walipokuja kushtuka wakashangaa yuko wapi Elimina?. Walipotazama pembeni wakamuona Elimina kasimama pembeni anawashangaa na yupo na mtoto wa mzee wa kanisa kashikwa mkono. Wakastaajabu sana. 

Yule mtoto akasema " poleni maana mnapambana na kisichokuwepo! Hii ni mbaya sana kwakuwa nyote mmeshindwa kugundua, unajua kwanini Mungu hakuwafunulia mapema nyie kuhusu huyu binti?. Wengi wenu hampo sawa na Mungu yaani, mmemkosea sana Mungu lakini mmejaa mazoea katika kuombea watu, ipo siku mtakemea mapepo yawaingie nyinyi wenyewe"

"Wewe mtoto unamaana gani? Nani kakuambia mimi nimemkosea Mungu?" Kijana mmoja aliongea kwa hamaki sana.

"Tena wewe? Kwani ni nani anaemchukia mama yake mzazi kwa kuwa alimgombanisha na mkewe? Si wewe au?. Alafu kapatane na mama yako kwanza, mkeo kashamsamehe ila wewe bado unakinyongo, ukifanya hilo tu Mungu ataweza kusema na wewe tena maana biblia inasema :1 Yohana 2:9 Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa"

Yule kijana chozi likamtoka, akapiga magoti na kuanza kulia. "Wewe ni nani uliye ndani ya mtoto huyu, hakika ni mtumishi wa mbingu. Umeyasema yaliyo ya kweli kabisa, kweli nastahili toba Kwa hili jambo" yule mtoto akawatazama wengine waliobaki

" Nani ni Tomaso kati yenu nimwambie kosa lake. Mmmh! Wengine walipojitazama myoyoni mwao waliogopa sana maana makosa yao ni ya aibu kutajwa mbele ya watumishi wenzao. Kila mmoja alikaa kimya. Yule mtoto ghafla akarudi kwenye hali ya kawaida akashangaa kafikaje pale na akashangaa kashika mkono na Elimina ambaye hakuwa hata kamzoea, mtoto alishtuka, alafu akaogopa maana aliona watu wote wamemkazia macho sana.

Aliachia mkono wa Elimina kwa haraka. "Dada kuna nini?".

"Usijali nenda kanisani. Lakini nimejifunza kitu kwako leo " katika maisha yako, usije kujichanganya maana Mungu humtumia yeyote kama ilivyo kwako leo ila mpaka akuamini na aone utakatifu wako"

Yule mtoto hakujibu kitu maana alikuwa hata haelewi maana ya maneno yale. Aliamua kuondoka zake na kukimbia kuelekea kanisani. Elimina aliwatazama watumishi wale kisha akawaomba radhi kwa kilichotokea. Hakuna aliemjibu maana wote walimnunia na hakuna alietaka hata kumtazama kila mmoja akaanza kutoka pale ndani akiwa na jambo lake moyoni. 

Walipotoka wote Elimina akamkumbuka mumewe na alipotazama saa aliona ni 7:18 mchana. Machozi yalianza kumtoka, alipiga magoti na kuanza kuomba toba kwaajili ya Elvine. Aliomba maombi ya maombolezo mpaka machozi yakaweka mifereji ya kudumu mashavuni. Aliomba, aliomba, aliomba, akaomba!! Mpaka nguvu zikamuishia. Baadae akajitia nguvu na kuamka pale chini alipokuwa kalala wakati anaomboleza.

Alipanda gari na kuanza kuondoka kuelekea nyumbani. Alilia njia nzima. Alipofika nyumbani aliitazama nyumba Kwa huzuni kuu. Akashuka kwenye gari na kuingia ndani. Cha kushangaza alimkuta mumewe yupo sebuleni kakaa anakunywa chai.

Elvine! Aliita kwa mshangao. Ndani ya dakika moja alijikuta anakumbuka tukio zima kati yake na yule malaika. Akajiuliza maswali mengi mno kichwani (Elvine ndio karudi? Au ninaota? Au Ile ya kule kanisani ndio ilikuwa ndoto? Mmh! Lakini mbona.... Hapana! Hii mbona ajabu, yaani Elvine kumbe ni mzima kabisa! Jaman mwee! ).

Alimsogelea mumewe machozi yakishindwa kufunga milango kwa uchungu na furaha ya kumuona mumewe. Elvine akasimama pale alipokaa na kuanza kumshangaa mkewe kwanini analia. 

"Vipi wewe yapi yamekukuta?"

"Ulikuwa wapi leo?"

"Kwani nilikuaga naenda wapi?"

"Mmh! Uko sawa kabisa?"

"Ndio nipo sawa!"

Elimina akakumbuka maneno ya yule malaika aliejitambulisha kwake kama Elvila. Akatulia Kwa dakika chache akiwaza, Kisha akafuta machozi na kumkazia macho Elvine vizuri. Alafu akamuuliza..

"We ni nani?"

"Unamaana gani mke wangu?"

"We shindwa pepo! Nani mkeo? Unadhani simjui mumewangu?, labda tu nikuambie: wewe sio Elvine, Elvine anatabia hata akichukia hawezi kunishangaa nikiwa nalia, lazima angenikumbatia na kutaka kujua zaidi kwanini nalia, alafu pia Elvine anapoongea na mimi huwa anani tazama machoni, ila wewe...., na tena Elvine mumewangu mimi hana tabasamu kama lakwako, wala macho makali kama yakwako!"

Yule mtu aliyemfanana sana Elvine akajua kashtukiwa, akataka ampige Elimina kofi moja zito, lakini Elimina alikwepa na kukimbilia chumbani na kujifungia huko. Yule mtu aliejifanya Elvine alikuwa ni Efraim na baada ya kuona kashindwa kudanganya Elimina kuwa yeye ni Elvine akachukia sana, akataka amfate kule kule chumbani kwa uwezo wake wa ajabu lakini alipotazama vizuri kwenye pembe za mlango wa kile chumba aliona mwanga mkali sana unatoka nje akagundua kuwa Elimina analindwa na malaika wengi mno kwahiyo hawezi kuingia pale, hivyo akaamua kuondoka.

Elimina alikaa chumbani kwa muda mrefu sana akiwa na woga na hofu kubwa. Baadae akajikaza akaamua atoke nje. Alipofika sebuleni hakukuta mtu. Alitazama kila mahali lakini hakuona mtu. Akaamua kurudi chumbani ambako alianza kuomba Kwa uchungu kwaajili ya mumewe. Aliomba mpaka saa 9 za usiku bila kuchoka. Ilipofika muda huo roho wa Bwana akamjilia juu yake ili amsaidie kuomba maana alikuwa anaomba toba kwa malalamiko bila hata point ya msingi. Alianza kunena kwa lugha mpaka saa 5:30 siku inayofuata ndipo akarudi kwenye hali ya kawaida.

*.     *.     *.      *.    *.    *

Elvine akiwa usingizini ndani ya ile nyumba waliyokaribishwa akaanza kuota ndoto za ajabu ajabu. Akashtuka usingizini, alipotazama pembeni hakumuona Elimina akashangaa sana. Alijikaza kuamka lakini mwili ulikuwa mzito sana na nguvu zilikuwa zinazidi kumtoka. Akajiuliza kwanini hali ile inamkuta. Akajikaza sana na akaweza kuamka, pembeni aliona mshumaa mwekundu unawaka, alipokuwa anashuka kitandani kwakuwa hakuwa na nguvu akayumba na kuukanyaga ule mshumaa pasipo kukusudia. Mshumaa ukaangukia kwenye kitanda alafu ukazima. Lakini kitanda kikashika moto. 

Moto mkali ukawaka kitandani, na ndani ya dakika moja moto ulisambaa kama petrol. Katikati ya moto Elvine alimuona mke wake anaomba tena yupo nyumbani. Elvine akaanza kukimbia kujiaokoa na ule moto maana nyumba yote ilikuwa inawaka moto, alishangaa sana kwani, alikuwa haungui wala hahisi joto la moto ule na alikuwa na nguvu sana. Akaona ajijaribu kwa kushika nguzo moja ya moto lakini nayo haikumuunguza ila Kila kitu pale ndani kulikuwa kinateketea. 

Alipofika nje, alimkuta Elimina katahamaki sana tena anahasira sana. 

"Umefanya nini Elvine? Elimina aliuliza kwa ukali sana tena hadi macho yalikuwa mekundu kama damu kwaajili ya kujaa hasira....

Swali; kwanini Elimina anahasira? Na Elimina huyu anasiri gani na nyumba iliyoungua moto?

Kusoma mwendelezo wake bonyeza hapa

Simulizi  hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            &, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.

Tu follow kwenye.

Facebook page>>> Add Value Network.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.




Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.