NGUVU YA TATHMINI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAKO.
NGUVU YA TATHMINI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAKO.
Kuna jambo moja muhimu sana katika safari ya mafanikio ambalo watu wengi hulipuuzia, lakini lina uwezo mkubwa wa kubadilisha kabisa mwelekeo wa maisha ya mtu yeyote.
Jambo hilo si lingine bali ni TATHMINI. Ndiyo tathmini boss.
Boss in short tathmini ni uwezo wa kusimama kwa muda, kuangalia ulipotoka, ulipo sasa hivi, na kule unakoelekea.
Yaani ni sawa na kujiuliza hivi;
Je, njia ninayotumia inanifikisha ninapotaka kwenda?
Nimefanikiwa kwa kiwango gani?
Nimekosea wapi?
Nini kimefanya mambo yasiende kama nilivyopanga?
Nifanye nini tofauti ili kupata matokeo bora zaidi?
Kwa sababu huwezi kuboresha kitu ambacho hukijui wala hujakipima boss.
Ndugu, TATHMINI SI KUSHINDWA HII NI HEKIMA
Watu wengi wakiona mipango yao haijafanikiwa haraka huamua kuiacha na kuibwaga ghafla tu.
Kibaya zaidi wengine huanza kulaumu: mazingira, watu wengine, bahati, hali ya maisha au kujilaumu wao wenyewe.
Lakini mtu mwenye hekima hufanya kitu cha tofauti kabisa. Kwanza anakaa chini na kujiuliza:
"Tatizo liko wapi?"
Pengine shida siyo kwamba ndoto yako ni mbaya laa hasha.
Labda ukute ni: njia uliyotumia,
muda ulioweka, maarifa uliyokuwa nayo kipindi iko, watu ulioshirikiana nao au mikakati uliyoifuata boss mambo ni mengi ani.
Sikia boss, wakati mwingine huhitaji kuacha safari yako, bali unahitaji kubadilisha namna unavyosafiri ndugu. Sijui kama unanipata boss?
HATA HIVYO, WATU WANAOKUA HUJITATHMINI MARA KWA MARA.
Mtu anayepiga hatua maishani si yule asiyefanya makosa kama tunavyodhania ndugu.
Bali ni yule anayejifunza kutokana na makosa yake. Na mtu mwenye hekima mara nyingi hujifunza kutokana na makosa ya wengine. Tofauti ni kubwa hapo boss.
Siku zote boss baada ya kila hatua, jiulize hivi:
Nimefanya vizuri wapi?
Nimejifunza nini?
Nini kinahitaji kubadilika?
Nitawezaje kufanya vizuri zaidi mara nyingine?
Hapo ndipo ukuaji wa kweli huanzia boss.
HEBU, ACHA KUTAFUTA MCHAWI, TAFUTA SULUHISHO BOSS.
Ni rahisi sana kusema: "Tatizo ni fulani."
Lakini swali la muhimu zaidi ni:
"Mimi ninaweza kubadilisha nini?"
Kwa sababu nguvu yako ipo kwenye vitu unavyoweza kuviongoza.
Tathmini inakurudisha kwenye uwezo wako wa kuongoza maisha yako badala ya kuishi kwa lawama na majuto.
Elewa kuwa, KILA MAFANIKIO MAKUBWA YANA MLANGO WA TATHMINI NYUMA YAKE.
Makampuni makubwa, viongozi wakubwa, wanamichezo, watu wanaofanikiwa, biashara kubwa na ngome imara hujifunza jambo hili muhimu mapema sana.
Yaàna, wenyewe ushindi siyo shida zao na hawaangalii tu ushindi.
Badala yake wanaangalia: nini kilifanya washinde, nini kilichelewesha maendeleo,
na nini kifanyike kuboresha zaidi.
Kwa sababu mafanikio ya leo hayatoshi bila maandalizi ya kesho leo. Rudia kusoma uelewe boss.
Nimalize kusema, Kujitathmini si udhaifu.
Si kukubali kushindwa. Ni ishara ya mtu mwenye akili inayokua na kukomaa.
Mtu mwenye busara hasemi:
"Nimeshindwa, basi basi tena."
Anasema: "Nimejifunza, sasa narudi nikiwa bora zaidi." Hata wewe ndugu yangu, hebu;
Simama. Pima safari yako. Rekebisha makosa.
Endelea mbele ukiwa na nguvu mpya zaidi.
Kwa sababu: Mtu anayejitathmini leo, anajijengea nafasi ya kufanikiwa zaidi kesho.
Labda nikuulize boss. Ni jambo gani katika maisha yako linahitaji tathmini na marekebisho?
#SeeYouNextLevel
Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.
Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026/06/huyu-ndiyo-mtu-muhimu-sana-kwenye.html
#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork.
+255767653697.
