KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA.

Image
  KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA. Boss! Siyo  kila mara, kusahau ni ishara ya Ubongo dhaifu, mara nyingi ni namna tunavyojifunza ndugu. Nimekutana na watu wengi wakisema: "Mimi sina akili kubwa." Wengine "Kumbukumbu yangu ni mbaya." Mara "Ubongo wangu hauhifadhi vitu." Lakini ukweli ni kwamba, mara nyingi tatizo si ukubwa wa akili yako wala uwezo wa ubongo wako. Tatizo ni kwamba watu wengi hawajawahi kufundishwa jinsi kumbukumbu (memory) inavyofanya kazi boss. Sikia ndugu; Ubongo wa binadamu umeumbwa kwa ustadi mkubwa. Kazi yake si kuhifadhi kila kitu unachokiona au kukisikia, bali ni kuchagua filtering taarifa muhimu na kuacha zisizo muhimu wala matumizi. Kwa hiyo, kusahau si kasoro ya ubongo ni sehemu ya kawaida ya jinsi unavyofanya kazi. Hebu tuangalie sababu kuu zinazowafanya watu kusahau mara kwa mara. 1. Kukariri Bila Kuelewa (memorising without understanding). Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo wanafunzi na hata watu wazima...

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

 


UKILIFAHAMU HILI KUHUSU WATU  UTAISHI VYEMA SANA MAISHANI.


Kuna ujuzi mwingi muhimu ambao kila mtu anapaswa kujifunza ili kufanikiwa maishani: mauzo, masoko, fedha, utatuzi wa matatizo, mawasiliano, majadiliano, na mengine mengi.
Lakini kuna ujuzi mmoja ambao ni zaidi ya hazina—ukiupata, unafungua milango mingi bila hata kugonga.

πŸ‘‰ Ujuzi huo ni KUWAFAHAMU WATU.
Ukifanikiwa kuwafahamu watu—saikolojia yao, hisia zao, na namna wanavyotaka kutendewa—hakuna mahali utakwamia.
Kwa nini?
Kwa sababu kila kitu unachokitaka kipo mikononi mwa watu: fedha, ardhi, bidhaa, mitaji, fursa, ushirikiano, na huduma zote.
Kwa kifupi:

πŸ‘‰ Mahusiano mazuri na watu ni bidhaa ADIMU yenye thamani kubwa sana.
Na kama ni bidhaa, basi lazima ujifunze namna ya kuitengeneza, kuikuza na kuitunza.
Katika sanaa hii ya kuishi na watu, kuna sheria mbili kuu zinazokuongoza.

SHERIA YA KWANZA: THE GOLDEN RULE
Kanuni hii inasema:
“Watendee wengine kama unavyotaka kutendewa wewe.”
Hii ni kanuni nzuri sana. Ina nia njema, ina maadili, na ina heshima.
Lakini…
πŸ‘‰ Ina udhaifu mmoja mkubwa.
Watu HAWAFANANI.

Unachokipenda wewe, si lazima kipendwe na mwingine.
Unaweza kupenda utani, mwingine akauchukia,
Unaweza kupenda ukali, mwingine anahitaji upole,
Unaweza kupenda uhuru, mwingine anapenda mwongozo
Unaweza kupenda haraka, mwingine anahitaji muda kidogo.
Kwa hiyo ukisema “nitanitendea kama unavyojitendea wewe”, unaweza kujifurahisha wewe—lakini ukamuumiza au kumkera mwingine bila hata kujua.

Hapo ndipo Golden Rule inapokwama.

SHERIA YA PILI: THE CHAMELEON RULE
Hii ndiyo sheria ya juu na bora zaidi.
πŸ‘‰ Ni kanuni ya Kinyonga.
Kama kinyonga hubadilika kulingana na mazingira, basi na wewe jifunze kubadilika kulingana na watu na mazingira.

Sheria hii inasema:
“Watendee watu kama wanavyotaka wao kutendewa.”
Si unajua kila mtu ana:
Mahitaji yake,
Mapendeleo yake,
Viwango vyake,
Hisia zake, na
Mipaka yake.

Kazi yako si kuwafanya watu wawe kama wewe.
Kazi yako ni kuwafahamu walivyo, kisha uwasiliane nao kwa lugha wanayoielewa wao na siyo kama wewe unavyoelewa.

Hapa ndipo ustadi wa kweli wa mahusiano ulipo.
Kwa mfano;
Unaweza kukutana na mtu:
Hapendi matusi,
Hapendi utani mwingi,
Hapendi kejeli,
Anathamini heshima na utulivu.
Lakini wewe unapenda:
Mizaha,
Maneno ya utani,
Urafiki wa kufunguka sana,
Ukilazimisha mfumo wako kwake…
πŸ‘‰ Unakaribia kumpoteza mtu huyo—hata kama ni wamuhimu sana kwenye maisha yako.

Je, Kufanya hii ni sawa na kuwaridhisha watu?
Hapana.
Hii siyo kujipendekeza, siyo kuwaridhisha watu,
Hii siyo kujishusha.
Hii siyo kupoteza utu wako.
πŸ‘‰ Hii ni hekima ya kijamii (social intelligence).
Ni uwezo wa:
Kusoma mazingira
Kutambua aina ya mtu
Kubadilisha namna ya mawasiliano
Kutoa heshima kwa tofauti za kibinadamu
Huu ndio USTAARABU wa akili ya juu katika dunia.
Sasa uondoke na kipi?

Ondoka na kanuni kuu ya kuishi na watu. Yaani,
πŸ‘‰ Tafsiri maisha kupitia watu na mazingira.
Badilika kulingana na:
Mahali ulipo,
Aina ya watu uliokutana nao,
Lengo la mahusiano hayo.
Kwa lugha rahisi:
Kuwa kama kinyonga, lakini ukiwa na malengo yako.
Hebu tafakari kwa kina kidogo,
Ni watu gani niliwahi kuwakwaza bila kujua?
Ni wapi nililazimisha watu wawe kama mimi?
Ni wapi sikujifunza tabia za watu kabla ya kuwa nao karibu?
Kisha…
πŸ‘‰ Amua kubadilika kuanzia sasa.
Huku ukijua:
Kusoma watu,
Kuwaheshimu walivyo, na
Kuwatendea kulingana na mahitaji yao.

Basi kufanya hivyo utakuwa umejenga MTAJI mkubwa kuliko FEDHA.
Hii ni kwa sababu:
Watu sahihi, wakikuamini na kukupenda, watakusupport na watakusaidia kubeba NDOTO zako.

Sasa chukua hatua leo
Anza na watu watatu wa karibu na wewe:
Angalia na ujifunze wanapenda nini,
Jifunze wanachokichukia,
Badilisha namna unavyowasiliana nao
Kisha utaona mabadiliko yatakayotokea
πŸ‘‰ Lakini kumbuka:
Mafanikio siyo tu unachojua katika maisha yako.
Lakini pia ni nani anakujua, anakuheshimu, anakusaport  na yuko tayari kushirikiana na wewe katika hatua zote za maisha yako.

Na hilo linaanza na KUWAFAHAMU WATU.

Hii ni HAZINA, ni zaidi ya UTAJIRI, Huu ni Ufunguo wa kufanikiwa katika maisha.

Si unajua ukitaka kwenda haraka nenda pekee yako, na kukitaka kwenda mbali nenda na watu.

Imeandaliwa na kuandikwa na;
Migongo Elias
□Add Value Network.
□ See You Next Level.
□ Knowledge is power
□0767653697


Popular posts from this blog

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31