HUYU NDIYO MTU MUHIMU SANA KWENYE MAISHA YAKO.
HUYU NDIYO MTU MUHIMU SANA KWENYE MAISHA YAKO. Kila mtu anaweza kutaja watu kadhaa ambao ni muhimu sana katika maisha yake. Wengine watataja: wazazi, walezi, ndugu, marafiki, wenza, walimu, au washauri waliowahi kuwasaidia. Na ni kweli, watu hawa wana nafasi kubwa sana katika safari yetu. Wanaweza kutupa msaada, ushauri, upendo na kututia moyo tunapopitia changamoto katika maisha yetu. Lakini kuna mtu mmoja ambaye mara nyingi tunamsahau na huyu ndiye ninaye mzungumzia leo boss. Mtu ambaye nafasi yake haiwezi kuchukuliwa na mwingine awayeyote boss. Mtu ambaye maisha yako yanategemea sana maamuzi yake. Mtu ambaye tabia zake zinaathiri sana maisha yako boss. Huyo mtu si mwingine ni WEWE MWENYEWE. BOSS WEWE NDIYE MSINGI WA MAISHA YAKO Watu wengine wanaweza kukusaidia ndiyo. Wanaweza: kukufungulia milango, kukupa nafasi, kukushauri, kukutia moyo. Kukupa faraja na kukusindikiza boss. Lakini hakuna mtu anayeweza kuishi maisha yako kwa niaba yako ndugu yangu. Hakuna mtu anayew...