TABIA 10 NDOGO ZINAZOFICHUA AKILI NA HADHI YA MTU.
TABIA 10 NDOGO ZINAZOFICHUA AKILI NA HADHI YA MTU.
1. USIMPIGIE MTU SIMU ZAIDI YA MARA MBILI MFULULIZO.
Saikolojia inasema, Simu moja ni ujumbe. Simu mbili ni heshima. Simu tatu na zaidi ni shinikizo. Ukishapiga mara mbili na hakujibu, ujumbe umeshafika. Amechagua kutokujibu kwa sababu zake. Pengine yuko mbali na simu, mazingira siyo rafiki, au yuko bize. Usi assume na kujipa majibu ya moja kwa moja huwezi jua boss. Hivyo, subiri hadi Mtu mwenye akitafute boss. Ukiona kimya baada ya siku kadhaa kama unaissue muhimu mrudie tena ikiwezekana mtumie ujumbe wa maneno texts.
2. REJESHA ULICHOKOPA/KUAZIMA, BILA KUKUMBUSHWA.
Boss vitu kama, Pesa, kalamu, kitabu, mwamvuri, ukubwa wake hauhusiki. Kinachohusika ni tabia yako boss. Mtu anayekukumbusha deni anakuonyesha kitu kimoja tu, hukustahili KUAMINIWA basi tu ni vile mistake ilifanyika.
Kuepuka hayo. Rejesha mapema, rejesha kwa hiari, rejesha ukiwa bado unakumbuka. Hapo ndipo uadilifu na uaminifu wako unaonekana tajiri. Sijui unanipata?
3. USITUMIE UKARIMU WA MTU KWAKO KUJILISHA BILA AIBU.
Unapotolewa out ai kualikwa na mtu, hata kama menyu iko mbele yako fikiri kwanza boss. Usiagize kile ambacho hununui mwenyewe siku za kawaida au kile ambacho ungekuwa wewe na pesa zako usingenunua kabisa. Ukarimu si fursa ya kujifurahisha bali ni fursa ya kuonyesha tabia yako. Chakula cha bei nafuu ulichokula kwa heshima kitakukumbukwa zaidi kuliko mlo wa kifahari uliomlazimu mtu. Kitu hiki kiliwahi nikuta siku za nyuma baada ya kujifunza nilichange mara moja. Dear boss hata kama aliyekutoa out ni big fish jitahidi uwe casual tu. Kabla ya kuagiza ikibidi muulize au shauriana naye kwanza.
4. USIULIZE MASWALI YENYE UKAKASI, MAISHA YA MTU SI MJADALA WAKO.
Insue kama "Hee tu Bado hujaoa/kuolewa?" "Hamjapata mtoto?" "Mwee bado mnaishi kwa kukodi?", mbona umenenpa sana , umekonda sana. Maswali haya hayana nia njema ndani yake, yana sindano. Kila mtu ana safari yake, mzigo wake, na wakati wake. Ukitaka kujua, subiri akuambie mwenyewe. Ukipenda uhusiano linda faragha yake. Kwasababu unaweza muuliza mtu kwa habari ya unene wake kumbe hicho kitu anakichukia na amekuwa akipambana nayo siku zote.
So kitu kizuri cha kumwambia ni kwamba umependeza, uko vizuri siku hizi n.k
Lakini kama muhusika atapenda yeye mwenyewe mshiriki hayo poa.
5. MSHIKIE MLANGO MTU ANAYEKUJA NYUMA YAKO.
Boss hiki nacho kikushinde? Kama mtu anakuja nyuma yako, shika mlango apite. Usifikirie umri wake, jinsia yake, au hadhi yake. Kitendo hicho kidogo kinasema mengi kuhusu moyo wako. Watu wanakukumbuka si kwa sababu ulikuwa mkubwa bali kwa sababu ulikuwa mwema. Boss hapa namaanisha kuwasaidia wengine kadiri unavyoweza bila kujali jina, jinsi, kabila rangi wala umri na watu watakumbuka.
Nakumbuka siku moja nilipata ajari nikianguka kwenye chombo cha moto. Kulikuwa na watu wengi tu kwa pemben wanacheza bao. Ajabu ni kwmaba Wengi wao walianza kucheka, kushangaa ajari ilivyotokea na wengine kuchukua video.
Lakini suprise alitokea bwana mmoja miongoni mwao akanisaidia, tukaotoa usafiri kwenye shimo kishq akanishauri nifanye nini.
Kusema ukweli yule bwana simjui jina na wala hanijui pia, lakini sijawahi msahau hadi kesho, na huwa natamani nionane naye kabisa. Nadhani umenipata nini namaanisha eeh.
6. UKIENDA MAHAKI NA RAFIKI YAKO JITAHIDI ULIPIE ZAMU YAKO, BILA KUKUMBUSHWA.
Kamw rafiki yako alikulipia safari ya kwenda — wewe lipia ya kurudi. Alinunua chai, wewe nunua chapati. Urafiki unaodumu ni ule ambao mzigo wake unabebwa pande zote mbili. Mtu anayepokea daima bila kutoa si rafiki, ni mzigo unaotembea. Wakati mwingine ujitahidi usiwe kama kupe kuconsume tu muda wote.
Hata kama hali yako bado ni ya chini sana jitahidi utoe chochote katika urafiki wenu, hata kama ni ushauri you hust give wewe ni boss ujue.
7. MTAZAMO TOFAUTI SI UADUI, JIFUNZE KUKUBALIANA NAYO.
Boss Namba 6 kwako ni namba 9 kwa aliyekaa upande wa pili, na wote mnasoma namba sahihi. Kabla hujakataa mawazo ya mtu, simama mahali alipokaa. Ukweli mara nyingi hauko kwa mmoja, uko katikati, ukingoja wote wawili wafike. Hivyo kabla hujayapinga au kuyakataa mawazo ya wengine fikiria na uyapime kwanza huenda kuna njia na ukweli ndani yake boss.
8. OMBA RUHUSA KWANZA KABLA HUJAINGILIA MAZUNGUMZO YA WATU.
Watu wawili wanapoongea pembeni huo si mwaliko wako. Ukitaka kuingia, simama kidogo, subiri pengo, kisha sema "samahani" kwanza kwa kuwakatizq jaman nina shida 1,2 n.k. Kujiingiza bila kukaribishwa si ujasiri, ni ukosefu wa ufahamu wa hali ya kijamii boss. Sijui kama ilishawahi kukutokea boss.
9. UKIMTANIA/KUMKEJELI MTU UKAONA AMCHUKIA/AMEUMIA , ACHA MARA MOJA.
Kuwa na mzaha ni vizuri lakini ukiona uso wake umebadilika, acha mara moja. Kuendelea kumtania mtu baada ya kuonyesha kutofurahia si ucheshi, ni ukatili uliojificha kwa tabasamu. Mzaha unaodumu una mipaka inayoheshimiwa boss.
10. SEMA AHSANTE, KILA WAKATI, KWA KILA KITU.
Neno hili halichoshi, halipunguzi hadhi yako, halichukui muda. Lakini linajenga, linaunganisha, na linakukumbusha kwamba hukufika hapa peke yako. Mtu aliyekusaidia, hata kidogo anastahili kusikia kwamba uliona alichofanya, Paul Clement anasema kushukuru ni kuomba tena.
Boss nimalize kwa kusema kwamba, "Adabu ndogo zinazoonekana kila siku ndizo zinazojenga mtu mkubwa wa kweli."
Vipi namba ngapi imekugusa sana boss?
#SeeYouNextLevel
Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.
Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026/05/ukidhibiti-maneno-yako-utaanza.html
#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork.
+255767653697.
