HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31
.jpeg)
Nilichosoma katika sehemu hii, simulizi imeendelea kwa mvuto mkubwa sana – linaonyesha mapambano ya ndani ya Elvine kati ya imani yake, hofu yakuwaza kumpoteza mkewe Elimina, na hatia ya makosa ya zamani. Kuna mambo yafuatayo nimeona yaliyobeba msingi wa sehemu hii:
1. Mgongano wa nafsi ya Elvine
👉Anapokuwa mbele ya Malaika Elvila, anatakiwa kufanya maamuzi magumu: kati ya mke na mtoto.
👉Uamuzi wake unaonyesha upungufu wa mwanadamu, uchungu, na jinsi maumivu yanavyoweza kuathiri fikra na maamuzi.
2. Adhabu na Neema
👉Kupotea kwa mtoto na kutozaa tena kwa Elimina ni matokeo ya makosa ya Elvine, lakini bado neema ya Mungu inaonekana kwa kumrejesha mkewe.
👉Malaika anamkumbusha kuwa Mungu si mkatili, bali anamfundisha kupitia mateso na changamoto.
3. Ugeuzi wa Maisha (Turning Point)
👉Elvine sasa anaitwa kuwa mchungaji wa kondoo wa Bwana, ishara kwamba maisha yake yamepata mwelekeo mpya.
👉Huu ni mwanzo wa safari yake ya kiroho, kutoka katika hatia na huzuni kuelekea huduma ya kiungu.
4. Upendo wa ndoa
👉Muunganiko wa Elvine na Elimina unaelezwa kwa hisia kali sana – kilio chao, kumbatio lao, na maneno ya madaktari yanasisitiza kuwa wanapendana kwa dhati.
👉Hii inafundisha kuwa mapenzi ya kweli hupimwa kwenye majaribu makubwa.
Kwa mtazamo wa kifasihi na kimaana , sehemu hii imejaa:
Ustadi wa kusisimua Kwa msomaji (suspense) , Cha kutaka kujua nini kitatokea baada ya Elvine kufanya maamuzi yasiyo na uhakika.
Maswali ya kimaadili na imani ,kati ya upendo wa familia na mapenzi ya Mungu.
Mafundisho ya kiimani , kuwa Mungu huruhusu mateso kwa ajili ya kutufundisha na kutuandaa kwa jukumu kubwa aidha LA kiroho au kimwili.
🙏Mr. MIGONGO ELIAS & JACQUELINE JOHN🙏
Here I have written a message in both literary work and spiritual matter, woven together with the eternal Word of God, so that it may carry the weight of the heart and the power of impact upon the reader and the listener.
🙏Mwanadamu usicheze na Mungu 🙏
Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?(Hesabu 23:19).
Anaposema, hufanyika; anapotoa ahadi, haina budi kutimia.
Njia zake ni za ajabu mno, hazichunguziki wala hazielezeki, kwa
macho ya mwili hayawezi kuyafikia, na akili za wanadamu haziwezi kuyafasiri.
Isaya 55:8-9 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.
Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
Yamkini leo unapita katika kivuli cha mauti, katika giza la huzuni, katika majaribu yasiyoelezeka. Yamkini machozi yamekuwa mkate wako mchana na usiku, na moyo wako umejaa maswali yasiyo na majibu. Lakini kumbuka: Mungu halali na pia, Mungu hajakuacha, Mungu hajanyamaza bure Katika pitapita zako yupo NAWE Kila saa.
“Zaburi 23:4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Amini, hakika ipo siku moja, kutakuwa vyema tu.
Kwani macho ya Mungu yameelekezwa juu yako, na rehema zake hazikomi.
Mapito yako ni darasa, mateso yako ni maandalizi, na machozi yako ni mbegu ya furaha ijayo.
Kwa hiyo mwanadamu, usidanganyike kwa kuichezea neema ya Mungu.
Ukihesabu magumu yako kama adhabu, kumbuka ni daraja la neema.
Ukiona giza mbele yako, jua ni kivuli cha mwanga unaokuja.
Kwa maana Mungu ni mwaminifu, na hajawahi kudanganya.
Anakuangalia, anakushika, na mwisho wake utashangilia.
In conclusion ;This part of Hatima ya Kimungu (Section 29) has deeply touched me. The blend of pain, love, faith, and sacrifice shows how fragile human life is, and how God uses trials to shape our destiny.
As a writer and a believer, I see in Elvine’s struggle the reflection of many of us when faced with impossible choices torn between love, responsibility, and God’s will. His tears represent the weakness of humanity, but his new covenant with God reveals that redemption and transformation are always possible.
I truly admire the way this story reminds us that marriage, faith, and commitment to God can carry us through the darkest valleys.
DANIEL EMANUEL NGASA
CONTACT;+255 683 227 7.
Kusoma sehemu ya 29 bonyeza hapa
Hadithi hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.
Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .
Mawasiliano:
Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.
&,
Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.
Mawasiliano:
Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255617653697.
Pamoja na;
ERICK MGAYA. Mhariri.
Mawasiliano :
Normal and WhatsApp no >>>>+255764032905
Tu follow kwenye.
Facebook page>>> Add Value Network.
GeT tO tHe NeXt LeVeL!
Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.