Posts

Showing posts from March, 2023

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23. Ilipoishia...... Alipofika nje, alimkuta Elimina katahamaki sana tena anahasira sana.  "Umefanya nini Elvine? Elimina aliuliza kwa ukali sana tena hadi macho yalikuwa mekundu kama damu kwaajili ya kujaa hasira.... Swali; kwanini Elimina anahasira? Na Elimina huyu anasiri gani na nyumba iliyoungua moto? Kusoma sehemu ya 22 bonyeza hapa   Sasa inaendelea...... Elvine alikuwa anatetemeka  kwa hofu ya yale anayoyaona lakini alistaajabu kuona ni kama mkewe hajali sana kuhusu yeye. Alimtazama kwa makini sana mkewe akiwa anajaribu kutafakari kwanini anaonekana kuwa na hasira juu yake. Elimina akajishitukia "Hey, wewe! Nini sasa unanitazama hivyo?" "Nakutafakari sipati majibu!' "Nimefanyaje kwani?" "Hamna ila sijajua kama umenihofia mimi au hilo swali lako linamaana gani? "Elvine baba sina maana hiyo uliyoelewa wewe kabisa. Shida yangu mimi umefanya nini mpaka unataka kuhatarisha maisha Yako namna hii. Hujui namna ga

NJIA 7 LUKUKI ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

Image
  NJIA LUKUKI ZA KUOSHA UBONGO WAKO. Hivi ulisha wahi kwenda hospitali na kupata ushauri wa daktari juu ya afya ya mwili wako? Au basi ulisha wahi kumsikia mtu yeyoye pengine rafiki, ndugu, mke, kaka yako au mtu yeyote akisimulia kuhusu ushauri wa daktari katika kutunza na kuimarisha afya ya mwili wake? Bila shaka ulisha wahi na kama bado usihamaki, kwani utaelewa tu. Ukweli ni kwamba mara nyingi watu wamekuwa na utaratibu wa kwenda hospitali kwaajili ya afya za miili yao na hapo watapewa dawa za kutosha ili kujiponya na malazi yanayo wasibu. Na mara nyingi hupewa dawa za kutumia, wengine huchomwa   sindano, wengine kupewa masharti ya namna ya kutumia dawa hizo wengine huambiwa kula baadhi ya vyakula wengine mazoezi n.k Kwa kawaida mwanadamu ameundwa na sehemu kuu mbili, nazo ni utu wa nje na utu wa ndani . Utu wa nje ndio huu mwili ambao unashikika yaani, huu mwili wa damu na nyama. Ili kuuimarisha mwili huu wanadamu wamekuwa wakifanya vitu kama mazoezi, kula vizuzi na vitu vinavy

KANUNI MAKINI YA KUPAMBANIA NDOTO YAKO:

Image
                      KANUNI MAKINI YA KUPAMBANIA NDOTO YAKO: Kuna njia nyingi sana tumeambiwa na kufundishwa kwa namna tofautitofauti sana ilikupambana na maisha yetu hasa katika kuyafikia malengo na mafanikio yetu.na kwa bahati nzuri au mbaya njia hizo zimekuwa zikiwasaidia wengi na wengine kuwahalibia kabisa na wengine kuwaboresha huku wengine zikiwabomoa kabisa .kiuhalisia hakuna njia ambayo imethibitishwa na kutumika kuwa ni njia bora kwa 100% ambayo inaleta mafanikio kwa watu wote kwa kweli bado sijaona.kwasababu njia ambayo ilimfanikisha John akiitumia Anna kwa namna ileile inaweza kumfilisi na kumharibia kabisa,njia iliyo mfilisi Huyu ndiyo itakayo mfanikisha yule.Unaweza ukaambiwa   weka malengo,amka mapema ,weka vipa umbele,fanya kazi kwa bidii,fanya mambo kwa utofauti,fanya kwa ubora,jifunze vitu vipya kila siku ,ajabu ni kwamba unaweza kufanya yote hayo na ukapata matokeo tofauti kabisa na ulivyo tarajia sababu zipo nyingi sana naomba tutaelezana wakati mwingine   lakini

JINSI YA KUSEMA UKWELI NA KUWA MWAMINIFU

Siku Moja nilikuwa katika pitapita zangu nikasikia mtu akisema siku hizi kumpata mtu mkweli haiwezekani. Nilipouliza kinagaubaga akasema watu ni waongo sana, hakuna anayeweza kuongea ukweli wakati Wote na Uongo umekuwa ni sehemu ya Maisha yetu. Na akachimba zaidi akasema kama utachagua kuwa mkweli itakubidi utafute kadunia Kako ukaishi kivyako huko. Ni kama kuna kaukweli Fulani hivi ukiangalia kadiri siku zinavyozidi kwenda watu wanazidi kupoteza UKWELI na UAMINIFU. Utashangaa mtu unamuuliza umefika wapi nipo hapa corner nakuja chapu,unakaa saa za kutosha hata hatokei kumbe bado yupo nyumbani kabisa.Mwingine anakwambia tutakutana saa 4:00 afu haonekani kabisa, mwingine anaenda kutoa sadaka hewa ili aonekane ametoa, yaani uongo umetapakaa Kila mahali UAMINIFU umekuwa bidhaa adimu sana. UKWELI umefichika umekuwa wa kumlika na tochi. kuwaridhisha na kujionyesha kwa wengine ni moja ya kitu kinachopelekea kusambaa na kuenea kwa uongo kuliko UKWELI. Hiki kitu kimekuwa ni kilio Cha wengi sana

TATUA TATIZO LOLOTE UNALOPITIA KWA NJIA HIZI!

Image
  TATUA TATIZO LOLOTE KWA NJIA HIZI! Siku zote ukiishi katika dunia hii kila kukicha utakutanana na migogoro na matatizo ya kutosha.Yaani, ukikwepa upande huu utakutananayo tu upande wa pili. Kumbe matatizo katika dunia hii ni sehemu ya maisha. watu wengi hawakubaliani na ukweli huu matokeo yake matatizo yamekuwa yakiwashangaza kila leo. Nimewahi kukutana na usemi mmoja ambao sina budi kukujuza nawewe leo. Nao ni huu “ kuishi duniani huku ukitegemea kuishi bila matatizo ni chanzo cha matatizo yote. ”, kuna watu wana amini kuwa wao hawajaumbwa kukutana na matatizo yeyote hapa duniani, hapo utakuta mtu anasema  “ hivi kwanini mimi tu Mungu yanipate haya ”. Ajabu kweli yaani matatizo anataka yawapate watu wengine tu ila yeye hapana, ndugu ilihali unakaa kwa hii dunia hiki kitu ni ngumu kukikwepa asee . Ndugu yangu kama unakaa kwenye hii dunia matatizo yatakuja tu aidha upende au usipende, uwe mwema au mbaya kiasi gani ,mcha Mungu au muovu kiasi gani, uwe tajiri au uwe masikini, uwe mc

SAMEHE KWA FAIDA YAKO MWENYEWE!.

Image
    SAMEHE KWA FAIDA YAKO MWENYEWE. Mtu mmoja alisikika akisema nimekusamehe lakini sitakusahau katika maisha yangu kwa hichi ulicho nitendea! Kama utakuwa mfuatariaji na mdadsi wa mambo na watu utagundua kuwa suala la kusamehe limekuwa ni changamoto kubwa sana kwa watu wengi. Wengi wamebaki na vinyongo, visasi, machungu, na hasira kupita kiasi kuhusu ulio   wakosea au kutokuwasamehe. Mwalimu mmoja aliwaagiza wanafunzi wake kila mmoja aje na nyanya kulingana na idadi ya watu anaowachukia. Wanafunzi walikuja nazo siku iliyofuata, wengine walikuja na nyanya moja, wengine mbili, wengine tano, na wengine nyanya za kutosha   na walipo kuja nazo aliwaambia waandike  majina ya watu wanaowachukia ko, waziache kwenye mikoba yao na mwalimu aliwaambia watakuwa wanakuja nazo kila siku bila  kuzitupa au kuziacha. Baada ya siku kadhaa wanafunzi walianza kulalamika kuwa mzigo umekuwa mzito na umekuwa ni ngumu kuja nao kwani zilikuwa zimeshaanza kuoza na kunuka hivyo yalikuwa yanaharibu daftari

KWANINI UNATESEKA NA MADENI YASIYO KOMA?

Image
  KWANINI UNATESEKA NA M ADENI YASIYO KOMA?  Kabla ya kwenda mbali Zaidi ni muhimu tujue maana ya maneno haya mawili nayo ni Mkopo na Deni. Mkopo ni aina ya fedha ambayo mtu au taasisi inachukua   kutoka kwenye chanzo kingine cha fedha kwa masharti fulani ya kurudisha fedha hizo kwa muda fulani na kwa kiwango cha riba. Mkopo unaweza kutolewa na benki au taasisi nyingine za kifedha, serikali, au hata mtu binafsi. Sasa pale mtu anaposhindwa kutimiza masharti na makubaliano ya mkopo huo. Hapo ndipo inageuka na kuwa deni   na kwa wingi ni madeni. Madeni si mabaya sana, kama yatakuwa yamefanyika kwa utaratibu maalum wa lengo la kuongeza thamani yake kila baada ya muda fulani. Lakini, kama si hivyo yatakuwa ni mabaya sana kuwahi kutokea. Pamoja na hayo zipo sababu nyingi sana zinazowapelekea watu wengi kuingia kwenye madeni yasiyoisha na mbaya zaidi wamefanya kila linalowezekana ili kuondokana na madeni hayo lakini imekuwa changamoto isiyoisha kwao. Hili nalo bado ni tatizo kubwa sana. L

MFANO WA FAMILIA YA KUIGWA.

Image
MFANO WA FAMILIA YA KUIGWA. Ngazi ya familia ni ngazi muhimu sana kwa maendeleo ya Kila mtu. Pamoja na kuwepo ngazi nyingi na kubwa pengine kuliko hata familia, kwa  mfano tunazo ngazi kama Makundi au marafiki ,Shule /vyuo, jamii, Taifa n.k. ngazi ya familia bado ni ngazi muhimu sana katika kutengeneza malezi na mwongozo bora kwa mtoto ili kuyafikia malengo na maono yake.  Lakini asilimia kubwa familia nyingi hazija litambua hili, kwani utajikuta baba yuko bize na kazi zake kweli kweli mama naye ndo kwanza ni yeye na vikoba  hata kaka na dada wanapo kuakua tu Kila mmoja anajua yake house gelo ndo mama, baba, dada na kaka wa watoto yeye ndo anajua wale nini wavaaje. Na wengine kuepuka taharuki zote hizo mtoto akifikisha miaka miwili tu anapelekwa boarding au nursery akajifunze kimombo ili kuja kuwakera wazazi na na wengine kwa kuwasemesha kingereza mwanzo mwisho akati hawakijui hata!, na kwa jeuri sasa nao wanatamba kweli mtaani kuwa mtoto ana mwaga ngeli balaa hahahaha!. Sipingi kitu k

SABABU ZA KUWEPO KWA MASIKINI WENGI KULIKO MATAJIRI;

TAMBUA KUWA ; Watu wengi sana wana malengo na wanatamani kuwa na mafanikio makubwa sana kuwahi kutokea hapa duniani yaani ukimuuliza mtu yeyote hata mtoto atakwambia ana ndoto ya kuwa dokta,mwalimu,nesi n.k wengine ma bilionea,  yani kiufupi hakuna asiyependa kufanikiwa sijaona kwakweli. Ingawa watu wote hutamani mafanikio makubwa sana swali moja limekuwa likinitesa na nimekuwa nikijiuliza kuwa kwanini kuna masikini wa kutosha kuliko hata matajiri na watu maarufu hapa dunian?. swali Hili ndilo ambalo limenifanya niandike Makala hii .na Makala hii itakwenda kulijibu swali hili vizuri kabisa  hivyo kaa kwa kutulia nikupatie madude. SABABU ZA KUWEPO KWA MASIKINI WENGI KULIKO MATAJIRI; Rafiki zipo sababu kede wa kede zinazo watofautisha masikini na matajiri hapa duniani lakin utofauti wao mkubwa unakuja kwenye tabia zao ndiyo maana Mwandishi wa vitabu, mkufunzi wa mambo ya Uongozi na mfanyabishara, Mike Murdock aliwahi kusema “Siri ya mafanikio yako imefichwa katika tabia zako za kila siku

Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.