HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26. Ilipoishia.......... Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti... Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa. Sasa inaendelea......, Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda

MFANO WA FAMILIA YA KUIGWA.

MFANO WA FAMILIA YA KUIGWA.
Ngazi ya familia ni ngazi muhimu sana kwa maendeleo ya Kila mtu. Pamoja na kuwepo ngazi nyingi na kubwa pengine kuliko hata familia, kwa  mfano tunazo ngazi kama Makundi au marafiki ,Shule /vyuo, jamii, Taifa n.k. ngazi ya familia bado ni ngazi muhimu sana katika kutengeneza malezi na mwongozo bora kwa mtoto ili kuyafikia malengo na maono yake. 

Lakini asilimia kubwa familia nyingi hazija litambua hili, kwani utajikuta baba yuko bize na kazi zake kweli kweli mama naye ndo kwanza ni yeye na vikoba  hata kaka na dada wanapo kuakua tu Kila mmoja anajua yake house gelo ndo mama, baba, dada na kaka wa watoto yeye ndo anajua wale nini wavaaje. Na wengine kuepuka taharuki zote hizo mtoto akifikisha miaka miwili tu anapelekwa boarding au nursery akajifunze kimombo ili kuja kuwakera wazazi na na wengine kwa kuwasemesha kingereza mwanzo mwisho akati hawakijui hata!, na kwa jeuri sasa nao wanatamba kweli mtaani kuwa mtoto ana mwaga ngeli balaa hahahaha!.

Sipingi kitu kama hichi lakini, ukweli ni kwamba kama familia, kuna mahali kuna muyumbo fulani, lazima tukubali yaani inafika wakati wazazi hawajui chochote kuhusu mtoto wao. Wanachojua ni kutoa hela ya twisheni, pipi na maandazi lakini, tukija kwa swala zima la kumfahamu mtoto wao kiundani bado ni kimbembe na matokeo yake wazazi wana walazimisha watoto wao kwenda kusoma na kusomea vitu vya ajabu kweli ambavyo hata wao wenyewe tu hawavijui kabisa.Tunapata kesi za  ajabu kweli yaani eti kisa mzazi anapenda kitu fulani na, alishindwa kikitimiza ndo anataka watoto wake waje wamtimizie,  hii inakubalika kweli jamani. Mimi nasema Hiki kitu hakikikubaliki kabisa Kwani "WATU HATUFANANI NA HATUWEZI KUFANANA". Ni muhimu kujua kwamba kila mtu ana ndoto yake na ipo tofauti kabisa na mtu mingine. Wazazi kuna mahala wana kwama kabisa imefika wakati Kila majukumu kuhusu watoto wao wamewaachia waalimu na watu wa mitaani kuwafahamu na kuamua, na kutengeneza hatima za wanao hili ni tatizo kubwa sana aseee. 

Sasa naandiki hivi mzazi wa  familia yenye KUIGWA kiujumla unayo kazi ya kushughulika na watoto wako in and out yaani, nje na ndani kwa sababu ipo sababu kubwa sana ya mtoto wako kupitia kwako hadi ukamzaa kuna watu wengi sana wanamlilia na kumwomba Mungu awape watoto lakini Mungu aliona kuwa wewe unafaa kumlea na kumsaidia mtoto huyo kutimiza kusudi la kuumbwa kwake. Kwani kuna uwezekano mkubwa sana kuwa angezaliwa kwingine na mtu mwingine kabisa .Goja nikuulize swali hivi wazazi wa Obama , Magufuli, Mesi na watu wengine mashuhuri walikuwa wanajua kuwa mtoto wao atakuja kuwa  raisi au mchezaji maarufu ulimwenguni???.na kama wangekuwa wanafahamu wangewalea kama wazazi wa leo wanavyo walea na kuwatwisha majukumu yao watu wengine??. 

Rafiki familia na wazazi wa KUIGWA ni wale ambao wanawasaidia watoto wao kujifahamu, kujitafuta, kujitambua, na kujua kusudi la kuumbwa kwao katika ulimwengu huu, mikakati na njia lukuki  za kuzifikia ndoto zao.

Wanafanya hivi kwa kuwajengea hofu ya mungunidhamu ya fedha, muda, Kujifunza maarifa mapya kila wakati, tabia ya kusomea nao vitabu hapa ndipo kuna siri kubwa goja tutalijadili siku nyingine hili. Pia wanahakikisha wanakuwa nao kwa ukaribu sana kwa kujua nini wanapenda na kipi hawapendelei yaani ukiwa mzazi wa namna hii utayafanya maisha yawe mepesi sana asee, si unajua hawajui wao ni akinanani na wapo hapa kwa Dunia kufanya nini hii issue imekuwa gumuzo mtaani na watu maisha hayaendeki kwa sababu watu hawajui ndoto na hatima zao na wazazi  wanaishi kama wanyama wengine  kwakweli wanachochea sana moto huu na hii ni shida sana tubadilike jamani.

Je ungependa kuwa mzazi wa familia yenye KUIGWA?? Fanya hayo mambo ya familia zenye kuigwa hufanya  na matokeo utayapata naamini utanipenda.

Mungu akubariki sana nakutakia familia yenye heri kwako.

GeT tO ThE nExT lEvEl!

Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa  mtandao wa addvaluetz  karibu sana ujiongezee thamani yako. 

Kwa mawasiliano;

Sim na Whatsapp >>+255783327456 / +255767653697.

Email>> eliasmigongo120@gmail.com.

Facebook>> MIGONGO ELIAS.

LinkedIn>>Migongoe. 

Pinterest>>eliasmigongo.

Kama umejifunza kitu,niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe


Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.