HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31
HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31
Ilipoishia……….
Elvine alipoteza amani kuliko hata mkewe maana kila alipomtazama mkewe basi moyo wake ni kama ulikuwa unachomwa na mwiba uliojishikiza huko kwenye mishipa ya moyo. Nafsi yake ilitaabika na ndipo alipoamua kutafuta muda mzuri, baada ya chakula cha jioni, azungumze na mkewe, maana ule ukimya wa siku mbili ulikuwa adhabu kubwa sana kwake.
Kusoma sehemu ya 30 bonyeza hapa
Sasa inaendelea……….
Elimina mamy naomba kujua kwanini hutaki kuniuliza kuhusu sababu ya haya yote? Maana najua unajua kuwa kuna mahali mimi nilikosea, sasa unapokaa kimya hivyo… kiukweli unazidi kunichanganya maana ni kama hutaki kujua, sasa unadhani mimi roho yangu itatulia kweli?. Hata kama ungekuwa wewe lazima usingepata amani, ungekuwa hata unawaza hivi nakuwaziaje, nakuonaje na ninajisikiaje ninapokuona, sasa kwanini wewe umekaa kimya, sema neno tafadhali? (Elvine alikuwa akiongea bila kumtazama mkewe usoni maana moyo wake haukuwa katika hali ya utulivu).
Pamoja na Elvine kuongea yote hayo. Elimina hakusema neno, ila alibaki akimtazama tu.
Elimina, please nakuomba sema neno. Basi hata kama unahasira nataka kujua kama unahasira au kama unatamani kunipiga basi fanya hivyo.
Elimina akatabasamu kisha akamuuliza “unamaanisha kweli”
Elvine alipomtazama mkewe usoni alikuta anatabasamu lakini bado aliweza kuona huzuni iliyokuwa imefichwa kwenye lile tabasamu. Alijua kuwa mkewe anauchungu moyoni, tena tabasamu lake halikumaanisha furaha ya kile alichosema bali inawezekana kabisa kuwa kama Elimina angekuwa na uwezo huo basi kweli angempiga.
Elimina sitanii maana kwangu mimi naona moto unawaka moyoni mwangu, natamani mtu aje anipige labda huu moto utazima maana nimekukosea sana mke wangu. Please ondoa hasira yako kwangu basi hata unilaumu kwa makosa yangu tu angalau nitajua kilichopo moyoni mwako.
Elimina alimtazama sana kwa muda alafu akatabasamu tena, kisha akasimama na kwenda kupanga nguo kwenye kabati la nguo. Wakati anapanga nguo akamuuliza swali mumewe “vipi kama nimeamua kupotezea ?”
Elvine akajibu “siwezi kukuamini kwa hilo”
Eliminia hakuendelea kuzungumza bali kimya kizito kikatawala baina yao. Elimina alimaliza kupanga nguo kisha akapanda kitandani bila kusema neno lolote. Jambo lile liliufanya usiku kwa Elvine kuwa mzito zaidi maana aliukosa usingizi kabisa. Usiku wa saa 9 aliamua kutoka na kwenda sebuleni. Na wakati anatoka chumbani alimfungia mkewe kule chumbani ili ikitokea mkewe akiamka basi asitoke nje.
Alikwenda sebuleni akawa anazungukazunguka tu, maana moyo wake ulikuwa unamwambia alie sana, tena alie kwa sauti labda uchungu na hasira itakwisha. Alielekea jikoni na alipofika huko aliona wakati wake wa kulia sasa unafaa, aliufungua mlango kisha akajibanza nyuma ya ule mlango, akakaa chini na kukiweka kichwa chake Katikati ya miguu yake, akalia sana. Mwanzo alizuia sauti yake kwa kulia kiume lakini kadri alipokuwa akilia alihisi moyo unataka kupasuka. Mwisho alipiga kelele ya uchungu sana.
Elimina ule usiku hakuwa kalala pia, na alikuwa kageukia ukutani huku kajikunja kana kwamba amelala lakini haikuwa hivyo, alikuwa akilia sana muda wote huo, ila hakutaka Elvine ajue. Alipoona Elvine anatoka nje alitaka kumfuata ili ajue anakwenda wapi, lakini alishangaa kuona kafungiwa kwa nje. Hilo lilimshangaza sana na kumuogopesha mno. Alitamani kuvunja mlango lakini alishindwa kufanya hivyo.
Wakati kazubaa hajui afanye nini alishtuka baada ya kusikia sauti kali iliyosikika mara moja tu yakilio. Aliogopa zaidi na akahisi kuchanganyikiwa. Wakati hajui cha kufanya alichakata hicho kilio kwa akili yake na mwisho akapata majibu kuwa, yawezekana Elvine analia ila hakutaka kulia mbele yake.
Alitaabika sana kutoka na akaona haitawezekana kufanya hivyo. Akaamua kupiga kelele kana kwamba amevamiwa na watu au viumbe vya kutisha. Elvine aliposikia sauti ya mkewe alishtuka na kwa haraka alifuta machozi na kukimbia mpaka chumbani alikomfungia mkewe. Alipofika pale mlangoni aligundua kuwa ufunguo ulianguka maana hakuwa nao Wakati huo. Alitoka mbio hadi jikoni na akaukuta ufunguo alipokuwa amekaa. Haraka alichukua ufunguo na kuanza kurudi chumbani, kwa kuwa alikuwa na haraka, alijikuta katereza na kuangukia mkono, alipojikaza kuinuka aligundua kuwa damu ilikuwa inamtoka mdomoni. Hakujali hilo, haraka alienda kwenye mlango chumbani na kuanza kuhangaika kufungua mlango.
Kwakuwa alikuwa na haraka na alikuwa tayari kachanganyikiwa, akili yake ilikuwa haijatulia hivyo funguo ikamgomea kufungua mlango; si kwasababu haikuwa funguo sahihi ila yeye alikuwa na mawenge akawa anaizungusha hovyo hovyo funguo bila utaratibu unaotakiwa. Alihangaika kwa muda mwisho akaanza kulia maana kila alipojaribu Aliona funguo inagoma.
Elimina aligundua kuwa Elvine yupo pale mlangoni ila kashindwa kufungua mlango na badala yake yupo anahangaika tu. Aliamua kutulia na kuacha kupiga kelele kama mwanzo maana alijua kabisa kuwa anazidi kumchanganya Elvine.
Huku nje ya mlango baada ya Elvine kushindwa kabisa kufungua mlango na kusikia Elimina kaacha kupiga kelele za msaada akahisi tayari Elimina kakutwa na mazito kwahiyo hawezi tena kuongea hivyo alizidi kuchanganyikiwa zaidi ya mwanzo. Alijikuta akianza kuupiga mlango kana kwamba anataka kuuvunja, lakini haikuwa rahisi pia.
Elimina alipogundua kuwa hali ya Elvine inazidi kuwa mbaya pale nje aliamua kumuita kwa sauti ya upole sana.
“Elvine, mimi nipo salama”
“hapana Elimina, wewe tulia mimi sasa hivi nafungua mlango, japo…. Japoo… sijui nimekosea wapi mimi zaidi, kwanini kila kitu kwangu kinakuwa kigumu upande wangu.. why…?” Elvine alimjibu Elimina huku analia sana
“Hapana, Elvine, kweli mimi nipo sawa, tulia kwanza alafu nisikilize” elimina aliongea sauti ya utaratibu sana
Lakini Elvine hakuamini kabisa, maana akili yake iliitafsiri ile asauti ya Elimina kama mtu anayemtia moyo tu ila uhalisia yamkini kazidiwa huko anajikaza tu kuongea na ndiyo maana anaongea sauti ya utaratibu vile.
“Elimina najua unapitia hali ngumu huko ndani, usijali sio muda mlango utafunguka, hakuna kitakacho kukuta kibaya, kwanza wewe huna kosa hata moja kwa Mungu, yote yalikuwa makosa yangu, yaani yule binti Erijini ndio kasababisha yote… ila… ila…. Usijali kila kitu kitaisha sawa mamaa… hakuna kitakachokukuta kabisa…”
Elimina alipoona Elvine hamuelewi akaamua kuongea kwa sauti ya ukali
“Elvine mbona haunielewi nimesema nipo sawa!!! Tulia acha presha.”
“sauti hii kidogo ilimshtua Elvine na akajikuta anaweza kuufungua mlango. Kwa haraka aliusukuma mlango na kuingia ndani. Alimkuta mkewe kasimama tu pembeni ya mlango akimtazama. Alimshika mkono na kuanza kumuuliza tatizo lilikua nini mpaka akawa anapiga kelele? Lakini mkewe hakujibu ila akamkumbatia na kumwambia asijali hakuna kilichotokea.
Elvine baada ya kugundua mkewe alikuwa kafanya makusudi, alichukia sana, alimsukuma na akaanza kumfokea
“hivi wewe unawezaje kuleta utani kwenye wakati kama huu? Kila kitu kwangu kinaenda vibaya na wewe bado unaona raha kunichanganya eeh? Mwanamke gani wewe hupendi kuona mimi napata furaha?”
“Hapana Elvine, samahani sana, sikuwa na maana ya kukuchanganya, ila nilitaka uache kile ulichokuwa unakifanya huko nje” Elimina aliongea huku akimshika Elvine mabega
“niache!! Unanishikashika nini, wewe unajua mimi nilikuwa nafanya nini mpaka utake niache, au unahisi mimi nimekuwa muuwaji siku hizi, ndiyo maana hutaki kuniuliza kuhusu mwanao? Nakuuliza wewe mwanamke? Nijibu” Elvine alikuwa akiongea kwa hasira sana lakini alikuwa akitetemeka mno kwaajili ya uchungu uliokuwa umejaa ndani yake hadi meno yakawa yanagongana wakati anaongea.
“naomba unisamehe najua nimekosea, please naomba unisamehe” Elimina alijikuta naye akianza kulia na kujutia kile alichokifanya japo lengo lake lilikuwa ni kumfanya Elvine aache kulia kule nje peke yake ili amtulize, lakini kwa bahati mbaya mambo hayakuwa kama alivyotarajia”
Elvine aliwaka kama moto na akawa hataki kutulia. Wakati mkewe anajishusha ili kujaribu kumaliza ugomvi yeye akawa anazidi kupandisha hasira zake kwahiyo hakutaka hata kumsikiliza mkewe maana aliamini mkewe aliamua tu kucheza na akili yake bila kutumia akili.
Wakati ugomvi unaendelea Elimina alijikuta kapokea kofi la uso bila kutegemea. Elvine mwenyewe hakuamini kama ni yeye ndiye aliyemshushia kofi zito vile mkewe. Elvine alishtuka sana na kuanza kumuomba mkewe msamaha “Elimina samahani, yaani kweli haikuwa dhamira yangu, please! ”
Wakati Elvine anautafuta msamaha huo, Elimina alikuwa kainama tu, kashika shavu lake huku machozi yakimtiririka pas
ipo kutoa sauti.
Itaendelea…..
Hadithi hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.
Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .
Mawasiliano:
Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.
&,
Imehaririwa na
MIGONGO ELIAS. Mhariri.
Mawasiliano:
Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255617653697.
Pamoja na;
ERICK MGAYA. Mhariri.
Mawasiliano :
Normal and WhatsApp no >>>>+255764032905
Tu follow kwenye.
Facebook page>>> Add Value Network.
GeT tO tHe NeXt LeVeL!
Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.
.jpeg)