HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 30
HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 30
Ilipoishia……...
Kwa upande wa Elvine kilio chake kilitawaliwa na huzuni, hofu na woga wa kumpoteza mkewe, alitawaliwa na hasira dhidi yake mwenyewe kwa makosa aliyoyafanya maana aliona adhabu kubwa itaipata familia yake kwaajili yake, hali hii ya mkewe kupoteza, mtoto na kutopata mtoto ilizidisha maumivu na kila alipomkumbuka Eljini alihisi kupasuka. Kilio chake kiligubikwa na huruma kwa mateso aliyopitia mkewe wakati ambao yeye hakuwepo maana aliona kila tatizo la Elimina basi yeye ndio chanzo, hivyo alikuwa anaumia sana moyoni mwake…...
Kusoma sehemu ya 29 bonyeza hapa
Sasa inaendelea……...
Baada ya kulia sana madaktari waliamua kuwatuliza na kuwainua pale chini. Eliudi alimwita Elvine pembeni na kumwambia anajambo la kuongea nae. Hivyo waliamua kutoka nje na kumuacha Elimina pale ndani akiwa na madaktari wengine ambao dhahiri walionekana kushangazwa na jambo ambalo hata Elimina mwenyewe hakujua ni nini hasa.
Wakati Elvine na Eliudi wanatoka nje, Elimina alitamani sana kujua wanaenda kuzungumza kitu gani. Hivyo aliwaambia madaktari aliobaki nao kuwa anahitaji kwenda toilet na akaahidi kurejea baada ya dakika chache. Baada ya kutoka pale alianza kuwatafuta Elvine na daktari Eliudi walikoelekea.
Kwa bahati hawakuwa mbali sana hivyo aliwaona kwenye kona fulani ya hospitali lakini alimkuta Elvine akilia sana jambo ambalo moja kwa moja iliashiria kuwa kaambiwa jambo baya. Elimina alisogea kwa karibu na kisha akanyata na kujibanza kwenye ukuta ambao ilikuwa rahisi sana kwake kuwasikia wanachoongea japo wao wasingemuona kwa urahisi.
“Usilie sasa Elvine, unajua ukilia hivyo…. alafu we mtoto wa kiume, mkeo atafanyaje sasa si atatakiwa azimie kabisa. Ebu acha kuwa hivyo, au kuna jambo jingine zaidi ambalo unalijua na mimi silijui? Hebu niambie ukweli, au mlipigana siku moja kabla ya mkeo kuletwa hapa?” daktari Eliudi alisikika akimuhoji elvine
“Hapana, mimi na Elimina hatukugombana, lakini kuna mambo mengi sana ambayo kwa hali ya kawaida huwezi kunielewa Eliudi, ila wewe jua tu, hii dunia ina mambo mengi mazito. Kwa ufupi moyo wangu mimi…. moyo wangu umeshakuwa dhaifu” Elvine alijibu huku akiwa katika kilio cha kwichi kisicho na sauti.
“Ook sawa, but usijali, ila ushauri wangu ni kama nilivyokwambia, tafuta hata mganga rafiki yangu maana kuna jambo hapa halipo sawa, najua unasali ila hata sisi wengine mambo yakitukaba tunajongeza kidogo” Eliudi aliongea huku kamkazia macho Elvine
“Ushauri unaonipa wewe ni kama kunivutia kwenye mauti yangu ya mwisho, surely wakati huu, adui zangu wanasubilia maamuzi yangu. Eliudi mimi siwezi kufanya kosa jingine kama hilo maana kuna wakati nilijalibiwa kwa tamaa zangu na wema usio na mbele wala nyuma na sasa najutia. Mimi najua Mungu anahuruma sana atanihurumia tu, na mtoto nitapata tu one day” Elvine alijitia moyo na kufuta machozi yake
“We jikute wa Mungu sana, shauri yako. Mimi mwenyewe nasali tena kanisani kwetu mimi ni mzee wa kanisa, na pia mimi ni daktari kwahiyo sikushauri ujinga hapa, nataka kukusaidia”
“Hakuna msaada hapo! ila wewe unanipa ushauri wa kifo cha rohoni na mwilini, tayari naujua moto wa kuwa vuguvugu Eliudi, ila kwa wewe huwezi elewa. Ila naomba tu Mungu akupe na wewe funzo kidogo, maana sasa hivi nachukia sana watu ambao ndani yao tayari wanaikaribisha dhambi taratibu huku mbele za watu wanaficha aibu zao. Haya yote ni matokea ya kosa moja nililoliona labda ni dogo wakati huo”
“unamaana gani?”
“huwezi nielewa kwa sasa ila soon utaelewa Eliudi”
“utajikuta unakufa bila urithi nakwambia, maana kama nilivyo kwambia, mkeo yupo kwenye hatari ya kutopata mtoto tena na isitoshe inatakiwa afanyiwe operesheni ya haraka atolewe kizazi kabisa bila hivyo anaweza kupata madhara makubwa zaidi maana kwanzia sasa tumbo litaanza kumsumbua, na pia we unadhani ni hali ya kawaida ee? Nadhani hili sijakwambia, unadhani kwanini madaktari walijaa pale ofisini kwangu? Mkeo alikuwa anazima alafu mtoto anaamka, mtoto akizima mkeo anafumbua macho, unadhani ni hali ya kawaida hiyo? na haijajitokeza mara moja hiyo hali, mimi nakwambia kuna mtu anakuchezea unaniona mimi mbulula aya!” Eliudi aliongea kwa hasira
“hayo yote nayajua hata kama sikuwepo hapo” Elvine alijibu kwa mkato huku chozi likimdondoka.
Wakati hayo yote yanaendelea Elimina alikuwa anasikia kila kitu, na aliposikia hataweza kupata mtoto tena, alihisi kuzunguzungu. Alitoka pale mbio na kusogea mbali kidogo maana tayari alihisi kama anakabwa na nguo aliyoivaa, hakufika mbali alidondoka na kupoteza fahamu. Madaktari waliokuwa karibu na eneo hilo, walimuwahisha kwenye chumba cha dharura ili kumpatia huduma ya haraka maana hawakujua sababu ya binti huyo kuzimia.
Elvine na Eliudi, majadiliano yao yalikatishwa na simu ya Eliudi kuita na kupewa taarifa za mgonjwa wake kukutwa kazimia. Haraka waliwahi alipolazwa Elimina. Kwa bahati walipofika walikuta tayari kazinduka, hivyo Elimina na Elvine walipewa ruhusa ya kurejea nyumbani. Lakini njiani Elvine alishangaa kuona Elimina yupo kimya na wala hajauliza kuhusu mtoto wake.
Walifika nyumbani, Elimina bila kusema neno alielekea chumbani na kulala. Elvine usingizi ulimkataa kabisa. Elimina aliigiza kutojali lakini haikuwa kweli, Elvine aliweza kugundua hilo. Lakini swali lililomtesa Elvine ni kwanini Elimina haulizi chochote kuhusu mambo yaliyotokea?
Zilipita kama siku mbili pasipo Elimina kusema chochote kabisa. Na kwa upande wake Elvine alikuwa anakosa namna nzuri ya kuanza kuyazungumzia yale mambo, kwahiyo alitamani Elimina aanzishe kwa kuongea jambo ili naye apate nguvu za kujieleza.
Itaendeea………
Hadithi hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.
Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .
Mawasiliano:
Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.
&,
Imehaririwa na
MIGONGO ELIAS. Mhariri.
Mawasiliano:
Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255617653697.
Pamoja na;
ERICK MGAYA. Mhariri.
Mawasiliano :
Normal and WhatsApp no >>>>+255764032905
Tu follow kwenye.
Facebook page>>> Add Value Network.
GeT tO tHe NeXt LeVeL!
Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.