HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31 Ilipoishia………. Elvine alipoteza amani kuliko hata mkewe maana kila alipomtazama mkewe basi moyo wake ni kama ulikuwa unachomwa na mwiba uliojishikiza huko kwenye mishipa ya moyo. Nafsi yake ilitaabika na ndipo alipoamua kutafuta muda mzuri, baada ya chakula cha jioni, azungumze na mkewe, maana ule ukimya wa siku mbili ulikuwa adhabu kubwa sana kwake. Kusoma sehemu ya 30 bonyeza hapa Sasa inaendelea………. Elimina mamy naomba kujua kwanini hutaki kuniuliza kuhusu sababu ya haya yote? Maana najua unajua kuwa kuna mahali mimi nilikosea, sasa unapokaa kimya hivyo… kiukweli unazidi kunichanganya maana ni kama hutaki kujua, sasa unadhani mimi roho yangu itatulia kweli?. Hata kama ungekuwa wewe lazima usingepata amani, ungekuwa hata unawaza hivi nakuwaziaje, nakuonaje na ninajisikiaje ninapokuona, sasa kwanini wewe umekaa kimya, sema neno tafadhali? (Elvine alikuwa akiongea bila kumtazama mkewe usoni maana moyo wake haukuwa katika hali ya utulivu). Pamoja na ...

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

 

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

Ilipoishia……….

Jesus! Elvine alishtuka na mshale wa hatari ukagonga kichwani mwake. Alianza kuifuata ile damu ambayo ilimpeleka mpaka chumbani ambako alimkuta Elimina kalala chini huku ashika mtoto mkononi,mtoto kalala na Elimina kazimia. Damu zilikuwa zimemtoka nyingi sana Elimina hivyo hakuwa na nguvu tena.

Elvine alipaniki asijue afanye kitu gani.

Kusoma sehemu ya 28 bonyeza hapa.

Sasa inaendelea……….

Haraka alimchukua mtoto kutoka mikononi mwa Elimina kisha akachukua kitenge cha mkewe na kukitandika kitandani alafu akamlaza mtoto wake. Kijasho chembamba kilikuwa kikimtiririka, kwa woga alimsogelea Elimina na kuanza kumuamsha.

Alipiga simu kwa daktari mmoja aliyekuwa akiitwa Eliudi kisha akamtaarifu kuhusu mkewe kujifungulia nyumbani na hatari iliyomkuta. Daktari Eliudi haraka aliagiza usafiri wa dharura (ambulance) kuja nyumbani kwa Elvine na baada ya dakika chache Elimina na mtoto walichukuliwa mpaka hospitali ya “The Lion” ambako walipewa huduma ya matibabu ya haraka na baada ya muda mchache Elvine aliisikia tena sauti ya mtoto wake akilia, jambo ambalo lilimpa moyo na nguvu mpya ya kuwa mtoto yupo hai.

Kwa Elimina mambo hayakuwa mazuri kabisa maana hakuzinduka mapema na madaktari walimwambia Elvine aombe sana maana mkewe yupo kwenye hari ya hatari sana, maana kwa uchunguzi uliofanywa alionekana kapata madhara makubwa sana kutokana na kupoteza damu nyingi pia iiligundulika kuwa alipigwa na kitu Kizito maeneo ya tumboni masaa machache kabla ya kujifungua.

Siku nzima ilipita pasipo Elimina kujitambua, jambo ambalo lilimfanya Elvine kuogopa sana na ndipo sasa alipoikumbuka sauti ya Malaika wake “Nenda ukaipate furaha ya muda mfupi”.

Alihisi kuchanganyikiwa, chozi zito likaanza kumtoka na akashindwa kuivumilia hali ile, akaanza kulia kwa sauti pale nje ya chumba cha wagonjwa mahututi jambo ambalo liliwashangaza watu na wengine kuzani kafiwa.

Eliudi alipokuja alishangaa kumkuta Elvine kakaa chini analia, aliamua kumshika mkono na kumwinua kisha akaenda naye ofisi kwake.

Eliudi alianza kumtia moyo Elvine na kumwambia kuwa Elimina hawezi kufa ni vile tu yupo kwenye hali mbaya kidogo ila wao kama madaktari watajitahidi kadri ya uwezo wao kuokoa maisha yake kwaiyo asilie bali amuombee.

“Hakuna unachoelewa Eliudi… we niache tu maana haya yote ni makosa yangu we niache please toka niache” Elvine alimfukuza Eliudi kana kwamba yeye ndiye mwenye ile ofisi.

Eliudi aligundua Elvine kachanganyikiwa sana hivyo akaamua kumuacha pale ofisini na kuondoka zake.

“Aya baba lia hasira iishe” aliongea Eliudi huku akitoka ofisini.

Elvine alipiga magoti na kuanza kuomba maombi ya uchungu na malalamiko.

“Please please…. ple…. please nakuomba, mke Wangu….. Mungu, please naomba jamani, usimchukue, makosa ni yangu na yeye hana hatia, kama unataka kutoa adhabu yoyote.. mi…mimi nipo tayari kuipokea hata kama ni kufa basi wacha nife mimi ila sio yeye nakomba. Elimina mbona mwema sana kwako daima na hajawahi kukukosea sana kama mimi sio? Mwachie yeye na uniadhibu mimi mwenye makosa naomba sana, help me please…. p…ple…please, kwani mimi sijawahi fanya jambo zuri kwako hata mara moja? Kwanini leo unaniadhibu vikali bila huruma, kwani huu si ndio ulikuwa muda wangu wapumziko? Kule nilikotoka nimeteseka na bado na huku ni…... ooh no”

Akiwa katikati ya kilio kizito ambacho kilijawa na hofu ya kumpoteza mkewe alihisi kaguswa begani na alipofumbua macho kweli alimuona Malaika Elvila.

“Kuna watu wanapata madhara kwa sababu ya makosa ya wengine na sio kwakua wamekosea, hivyo kwaajili yako uhai wa Elimina upo hatarini, ila hongera kwa sababu umeshtuka mapema endapo ungelala usiku wa leo basi asubuhi ya kesho Elimina angekuwa tayari katwaliwa. Na haya ni kweli ni makosa ya….” 

“Najua ni makosa yangu ndio, najua please niambie nifanye kitu gani kumrudisha mke wangu” Elvine alidakia huku akitetemeka kwa hofu.

Chagua kati ya mwanao na Elimina nani apewe adhabu yako.

Mtoto, mchukueni mtoto,

Kwanini mtoto? Kwasababu unahisi utapata mwingine?

Mchukueni bwana mimi mke wangu namuhitaji, kwanza huyo mtoto ni mgeni tu hata jina simjui (Elvine alikuwa anaongea hayo kwa hasira na uchungu mzito).

Ooh?

Ndio

Sawa mwanao kashakufa tayari na mkeo kashaamka sasa hivi. Elvine alitaka kutoka mbio aende kutazama lakini alipotaka kusimama alikosa nguvu kana kwamba kavaa vyuma miguuni. Alimtazama Elvila ambaye alikuwa tayari kachukizwa na tabia ya Elvine.

“mkeo ni muhimu kuliko maagizo unayopewa na Mungu?

Hapana samahani, ila naomba nikamuone kwanza mke wangu please.

Ooh kwahiyo mwanadamu unataka mimi ndio nikusubiri wewe umalize mambo yako? 

Hapana sina maana hiyo.

Pole sana Elvine, uhai wa mkeo na mwanao umebadilishwa tena, Elimina kafa tena na wewe ndiye uliyesababisha.

Hapa….hapana, please, Hapana, Samahani sirudii tena nipo tayari kufanya chochote ila naomba mumrejeshe Elimina please” Elvine aliongea akiwa tayari kasha paniki na alihisi kuchanganyikiwa tena

Sawa Elimina kapona ila hatopata mtoto tena kwa sasa, na mwanao pia kasha chukuliwa roho yake.

Ni sawa, ni sawa…. japo?…, ok sawa nimeridhia.

“Na kwa uhai wa mkeo unapaswa kuanza kutumika, maana muda umekwisha fika, kwanzia sasa wewe ni mchungaji nenda kalishe kondoo wa Bwana vyema yamkini neema ikarejea tena nyumbani mwako. Hivi Elvine unadhani Mungu ni mkatili sana kwako? La hasha kuna jambo anakufundisha kwa sasa hutaelewa ila baadae utanielewa vizuri”

“Sawa sawa sawa sawa nitafanya utakavyo, ila tafadhari nihakikishie uhai wa mke wangu”

Ok tuwekeane agano leo, kati ya wewe na Mungu wako; wewe sasa ni mchungaji wa kondoo wa BWANA” 

“Sawa sawa , mimi hapa Elvine nimekubali kuwa mchungaji na nitafanya kazi ya Mungu kama vile atakavyo”

Elvila alitoweka machoni pa Elvine baada ya mazungumzo na makubaliano hayo. Elvine alitoka mbio mpaka kwenye chumba cha wagonjwa mahututi lakini akaambiwa kuwa mkewe kashatolewa kule kwakuwa anaendelea vyema.

Alikwenda kwenye ofisi ya Eliudi ambako ndiko alikoelekezwa kuwa mkewe kapelekwa. Alipofika pale ofisini alikuta kuna madaktari watano ambao wanamshangaa Elimina, madaktari wote walikuwa kimya, hakuna aliyekuwa akitamka chochote bali walikuwa wakimtazama tu pasipo kuzungumza chochote.

Elvine alipoingia pale cha kwanza kilikuwa ni kumfuata mkewe na kumkumbatia, jambo ambalo Elimina lilimshangaza baada ya kugundua kuwa mumewe kasharudi, kwa furaha aliyokuwanayo Elimina alishindwa kujizuia kutoa machozi ya uchungu sana, kisha akapiga magoti na kuanza kumshukuru Mungu, Elvine alimkumbatia mkewe pale chini akiwa kapiga magoti pia huku akilia sana.

Tukio hili liliwafanya madaktari kutazamana na kisha wakasemezana “HAKIKA WATU HAWA WANAPENDANA SANA, sijui ingekuaje kama huyu binti angefariki siku ya leo huyu jamaa angekuwa kwenye hali gani”

Elvine alionekana kulia zaidi na akawa kama mtu ambaye akili yake haipo sawa maana kila muda alikuwa akimtazama mkewe na kumuuliza “upo salama kweli mama” na hali hii ilisababishwa na hofu aliyokuwa nayo. Machozi hayakukauka kwa haraka machoni mwake, maana alikuwa kajazwa na mengi sana moyoni mwake.

Kilio cha Elimina kilijazwa na shukrani na furaha ya kurudi kwa mtu aliyemsubiri kwa muda mrefu pasipo kujua ni lini angerejea maana imani ilipotaka kutindika aliamua kuishi na tumaini au matarajio mema kuwa yamkini Elvine atarejea. Kwahiyo hii ilikuwa ni zawadi na ‘surprise’ kubwa sana kwake maana hakuwa anajitambua wakati ambao Elvine alimchukua na kumpeleka hospitali.

Kwa upande wa Elvine kilio chake kilitawaliwa na huzuni, hofu na woga wa kumpoteza mkewe, alitawaliwa na hasira dhidi yake mwenyewe kwa makosa aliyokwisha kuyafanya maana aliona adhabu kubwa ambayo familia yake imepata kwaajili yake, hali hii ya mkewe kupoteza mtoto na kutopata mtoto tena hapo mbeleni ilizidisha maumivu na kila alipomkumbuka Eljini alihisi kupasuka. Kilio chake kiligubikwa na huruma kwa mateso aliyopitia mke wake wakati ambao yeye hakuwepo maana aliona kila tatizo la Elimina basi yeye ndio chanzo hivyo alikuwa anaumia sana moyoni mwake…...

Kusoma UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29 bonyeza hapa

Itaendelea………...

Kusoma sehemu ya 30 bonyeza hapa

Hadithi  hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            &, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255617653697.

Pamoja na;

ERICK MGAYA. Mhariri.

Mawasiliano :

Normal and WhatsApp no >>>>+255764032905

Tu follow kwenye.

Facebook page>>> Add Value Network.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.



Popular posts from this blog

MAAJABU YA AKIBA

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.