HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31 Ilipoishia………. Elvine alipoteza amani kuliko hata mkewe maana kila alipomtazama mkewe basi moyo wake ni kama ulikuwa unachomwa na mwiba uliojishikiza huko kwenye mishipa ya moyo. Nafsi yake ilitaabika na ndipo alipoamua kutafuta muda mzuri, baada ya chakula cha jioni, azungumze na mkewe, maana ule ukimya wa siku mbili ulikuwa adhabu kubwa sana kwake. Kusoma sehemu ya 30 bonyeza hapa Sasa inaendelea………. Elimina mamy naomba kujua kwanini hutaki kuniuliza kuhusu sababu ya haya yote? Maana najua unajua kuwa kuna mahali mimi nilikosea, sasa unapokaa kimya hivyo… kiukweli unazidi kunichanganya maana ni kama hutaki kujua, sasa unadhani mimi roho yangu itatulia kweli?. Hata kama ungekuwa wewe lazima usingepata amani, ungekuwa hata unawaza hivi nakuwaziaje, nakuonaje na ninajisikiaje ninapokuona, sasa kwanini wewe umekaa kimya, sema neno tafadhali? (Elvine alikuwa akiongea bila kumtazama mkewe usoni maana moyo wake haukuwa katika hali ya utulivu). Pamoja na ...

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 28

 


HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 28

Ilipoishia………

Elimina alishikwa na uchungu wa ghafla mbele ya Edgar, lakini Edgar alianza kucheka kisha akasema “sasa Elimina mama, wacha mie niende nikanywe moja baridi huko kwa marafiki, alafu wewe liaaa liaaa ukichoka kufa na mwanao maana mlango nafunga dear…. Hospitali sio ya kwenda watu kama wewe. Au omba hata Mungu atume malaika waje wakusaidie” 

Ilikuwa ni saa 7 mchana siku ya jumamosi sikuhiyo. Na isingekuwa rahisi kwa majirani kujua kinachoendelea pale ndani. Edger alitoka pale ndani na akafunga milango yote kisha akaondoka zake.

Kusoma sehemu ya 27 bofya bapa.

Sasa inaendeleaa……..

Elimina alishagundua kuwa tayari Edgar kaingiliwa na roho ya kishetani, hivyo anatumiwa kufanya vitu asivyovielewa kwahiyo sio kosa lake.

Elimina alikosa nguvu na akawa anahangaika pekeyake pale ndani, wala hakuwa na msaada na tayari kiumbe cha Elvine kilikuwa kinabisha hodi duniani. Mbaya zaidi Elimina hakuwa na uzoefu wowote maana huyo ndiye alikuwa mwana wake wa kwanza (kifungua tumbo), Elimina aligalagala pale chini pasipo msaada. Aliita majina yote anayoyajua ya watu wa kwao, Elvine pia aliitwa japo hata mwitaji alijua wazi kuwa Elvine hasikii 

Elimina akiwa katika hali hiyo mbaya ghafla alipigwa na mwanga flani usoni ambao ulimfanya asahau kuwa yupo katika hali ya uchungu na ghafla tu akaanza kumuombea Elvine.

Maombi; mungu wa mbingu na nchi na ijulikane leo ya kuwa wewe ji mungu wamiujiza. My husband Elvine has to come back no matter what. Namuombea nguvu mpya na ulinzi. Namuombea ujasiri katika hali anayopitia. Natuma moto kutoka mbinguni ukaangamize adui zake, natuma upanga ukatao kuwili ukaangamize uchawi na vitu vyao vyote, Bwana ulisema wewe sisi ni washindi hivyo tunashinda na zaidi ya kushinda. Yote kwa yote natubu kwaajili ya mume wangu, natubu kwaajili ya makosa yake please dear God msamehe mwanao huyu I pray don’t give up on him. 

Alipomaliza kutamka maneno hayo uchungu wake ukarudi tena na mara hii ilirudi kwa kasi mpaka akahisi kukosa pumzi na mbaya zaidi ulikuwa ni ujauzito wake wa kwanza kwahiyo alikuwa kwenye hali mbaya mno.

Baada ya kuangahaika kwa muda wa kama dakika 20 baadae aligundua kuwa ile hali ingepelekea mambo yawe magumu kwa upande wake, aliamua kujipa nguvu na kujikongoja mpaka chumbani kwake. Ambako alichukua vitenge viwili na kitambaa kimoja kidogo.

Kitambaa kile alikitumia kuking’ata mdomoni mwake kwa nguvu ili maumivu yake ayapunguze kwa kung’ata kitambaa kwa nguvu. Halafu vile vitenge viwili aliviambatanisha na kuvitandika chini, kisha akajiandaa kujizalisha mwenyewe.

Alijikaza mpaka alipofanikiwa kutimiza lengo lake. Baada ya muda Elimina alifanikiwa kumleta mwana wa Elvine ambaye alitoa sauti sauti ya ng’aaaaaaaaa…… ng’aaaaaaaaa…………..ng’aaaaaaaa……..

Elimina lipomuona mwanae alifurahi sana mpaka alitoa chozi. Ila kwa namna alivyokuwa kachoka pale pale alipoteza fahamu akiwa na mwanae mikononi mwake.

*************

Elvine ghafla alisikia sauti ya mtoto ikilia na wote waliokuwa pale chini ya mti waliisikia na wakati huo pale chini kulikuwa na timu kubwa sana; mapepo, majini, wachawi na vinyamkera vyote wakihangaika na mti.

Ile sauti ya mtoto iliwapiga masikioni wale watu wa ufalme wa giza pale chini kiasi cha kuanza kuwapasua vichwa. Walishangaa kuona mchawi mmoja kichwa kinapasuka na ubongo ukamwagika, wakiwa wanashangaana na mwingine akapasuka na ndipo walipoona pale hapafai tena wao kuwepo, kila mmoja akaanza kukimbia na kwenda kusiko julikana. Maana kila mmoja alikimbia kuokoa uhai wake hivyo walikuwa kama vichaa wakigongana gongana.

Wakiwa katika hali hiyo ya kukimbiakimbia ghafla wote walichanganyikiwa baada ya kumuona na Erijini kiongozi wao akipasuka kichwa pia maana alijifanya mbishi akabaki pale eti azuie ile sauti. Tena kwa Erijini alikufa vibaya sana maana alipasuka kichwa na baada ya kichwa kupasuka na kiungo kimoja kimoja kikawa kinazidi kupasuka.

Elvine alishindwa kuvumilia kutazama kinachoendelea pale chini. Aliamua kufumba macho na maskio yake maana sauti ya mtoto ilikuwa kali na sauti ya mipasuko ilikuwa kama mabomu kwahiyo ile sehemu ilikuwa sio ya kufurahisha.

Elvine alipofumbuwa macho yake baada ya dakika kama 5 aliona utulivu na ukimya wa ajabu ambao ulimfanya akaogopa zaidi

“Mungu wangu nisamehe mimi, kweli nimeona na naapa ntafanya chochote utakacho taka nifanye, naahidi, please nahitaji kurudi nyumbani nikawe kijana mwema” Elvine alitamka maneno hayo akiwa hata haelewi anaongea nini bali uoga na hofu ilitawala ndio ilikuwa ikizungumza

Alipotazama pembeni yake alimuona mtoto Elvila (Malaika). Alishtuka kiasi kwamba angeweza hata kudondoka lakini yule Malaika alimzuia asianguke.

“usiogope, unaniogopa hata mimi?” Elvila alimuuliza Elvine kwa tabasamu

Oooohhhh!!!! Elvine alishusha pumzi ndefu kwanza.

Asante….. asante umekuja, kwanini ulinitelekeza Elvila kwanini?

Kwakuwa ulistahili

Aty nini? Oky fine lakini si ungenisamehe tu.

Ooh, mungu ni mungu mwenye wivu, pia lazima akupe adhabu ili ukirudi usimsaliti tena. Ila bado hajakukatia tamaa, kakupa nafasi nyingine. Amini Elvine nakwambia kama usingelipitia hili yaliyo mbele yako yangekushinda. Lakini hasira ya Mungu ipo juu yako hivyo kuna pigo litakuja kwako hivi karibuni jiandae….

But kosa langu nini hasa

Wewe ulimsaliti mkeo, maana ulikokuwa unaelekea ilikuwa ni katika njia ya uzinzi Elvine, kama uliweza kuacha ibada kwaajili ya Erika na ukaongeza na uongo juu, kwa Mungu hilo sio jambo dogo kwa mtu ulieaminika kama wewe.

Nakili makosa kweli, nilidanganya, nikamsaliti Mungu na mke wangu na pia niliacha kumwabudu mungu, please samahani.

Ufunguo umeshapatikana Elvine, nao ni mtoto wako

Mtoto wangu!?

Yeah!!

“Nenda ukaipate furaha ya muda mfupi” Elvila alimaliza kwa kutabasamu sana

Elvine wala hakujali aliruka kutoka juu ya mti kwa furaha aliyokuwa nayo, na aliporuka tu alijikuta kakaa kwenya kiti cha miguu mtatu palepale alipopoteleaga. Hakutaka kujiuliza chochote kuhusu kilichotokea, pembeni aliliona gari lake palepale alipoliacha lipo vilevile halina hata vumbi

Hapo yote hayakumzubaisha Elvine kuyashangaa. Moja kwa moja kama kimbunga alizama ndani ya gari na kuendesha gari lake mpaka nyumbani. Alipofika nyumbani alishangaa kuona mlango umefungwa.

Akahisi labda mkewe atakuwa hospitali hivyo akageuza gari mpaka hospitali ya ‘the lion hospital” ambayo haikuwa mbali na kwao na ndio hospitali waliyozoea Kwenda yeye na mkewe mara nyingi. Alifika mapokezi na kuulizia kama mkewe karipoti pale lakini aliambiwa mkewe hayupo.Alijaribu kupiga simu lakini haikupokelewa.

Baadaye aliamua kurudi nyumbani tena. Kwa vile alikuwa na funguo nyingine aliweza kuingia ndani. Alipoingia alishangaa kuona damu nyingi kwenye sebule ya kulia chakula.

Jesus! Elvine alishtuka na mshale wa hatari ukagonga kichwani mwake. Alianza kuifuata ile damu ambayo ilimpeleka mpaka chumbani ambako alimkuta Elimina amelala chini huku ameshika mtoto mkononi. Mtoto kalala na Elimina kazimia. Damu zilikuwa zimemtoka nyingi sana, hakuwa hata na nguvu.

Elvine alipaniki asijue kitu gani afanye.

Itaendelea……………. 

Kusoma UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 28 bonyeza hapa

Kusoma sehemu ya 29 bonyeza hapa.

Hadithi  hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            &, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255617653697.

Tu follow kwenye.

Facebook page>>> Add Value Network.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.



Popular posts from this blog

MAAJABU YA AKIBA

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.