HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31 Ilipoishia………. Elvine alipoteza amani kuliko hata mkewe maana kila alipomtazama mkewe basi moyo wake ni kama ulikuwa unachomwa na mwiba uliojishikiza huko kwenye mishipa ya moyo. Nafsi yake ilitaabika na ndipo alipoamua kutafuta muda mzuri, baada ya chakula cha jioni, azungumze na mkewe, maana ule ukimya wa siku mbili ulikuwa adhabu kubwa sana kwake. Kusoma sehemu ya 30 bonyeza hapa Sasa inaendelea………. Elimina mamy naomba kujua kwanini hutaki kuniuliza kuhusu sababu ya haya yote? Maana najua unajua kuwa kuna mahali mimi nilikosea, sasa unapokaa kimya hivyo… kiukweli unazidi kunichanganya maana ni kama hutaki kujua, sasa unadhani mimi roho yangu itatulia kweli?. Hata kama ungekuwa wewe lazima usingepata amani, ungekuwa hata unawaza hivi nakuwaziaje, nakuonaje na ninajisikiaje ninapokuona, sasa kwanini wewe umekaa kimya, sema neno tafadhali? (Elvine alikuwa akiongea bila kumtazama mkewe usoni maana moyo wake haukuwa katika hali ya utulivu). Pamoja na ...

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

 


HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

Ilipoishia……...

              Elvine alikumbuka kila kitu, akajitambua na akakumbuka kila kilichotokea akiwa kwenye Ile ardhi, akajiuliza kuhusu Elimina na akatambua ukweli kuwa yule aliyenaye hawezi kuwa Elimina maana kuna vitu vingi alivyofanyiwa vibaya ambavyo Elimina asingeweza kufanya....

Kusoma sehemu ya 26 bonyeza hapa

Sasa inaendelea…...

Elvine akiwa pale mtini alikuwa akiwaza ni jambo gani litakaloendelea baada ya pale maana hakuwa na cha kufanya kwa haraka kutokana na mazingira yalivyo magumu kwake. Alitulia kidogo huku hofu imemkamata kisawasawa. Akaanza kusikia sauti ya Elimina anaomba sana tena anaomba maombi ya kupambana,

Maombi; Mungu wa mbingu na nchi na ijulikane leo ya kuwa wewe ni Mungu wamiujiza. My husband Elvine has to come back no matter what. Namuombea nguvu mpya na ulinzi. Namuombea ujasiri katika hali anayopitia. Natuma moto kutoka mbinguni ukaangamize adui zake, natuma upanga ukatao kuwili ukaangamize uchawi na vitu vyao vyote. Bwana ulisema wewe, sisi ni washindi hivyo tunashinda na zaidi ya kushinda. Yote kwa yote natubu kwaajili ya mume wangu, natubu kwaajili ya makosa yake please dear GOD, msamehe mwanao huyu, I pray don’t give up on him. 

Kisha maombi yakakata, na Elvine hakusikia sauti ile tena. Akiwa pale ni kama alikuwa mahali salama sana ambapo hata Mungu angeweza kusikia sauti yake. Akatazama juu na kwa mara ya kwanza aliona nuru na upepo mzuri sana ukampiga. Akaona mawingu kama yupo duniani vile. Alitambua kabisa yawezekana pale ndipo pana njia ya yeye kutokea, na hapo ndipo alipojisemea “ama kweli Mungu anapompitisha mtu kwenye jaribu anaandaa na njia ya kutokea” lakini bado akawa na swali ni namna gani ataweza kutoka pale maana bado hali sio njema na wala akueleweki. 

Akaanza kumlilia Mungu kwa uchungu sana maana aliamini pale mtini ni mahali pekee ambapo pana connection ya yeye na Mungu hivyo aliamua kuitumia hiyo nafasi vizuri sana. Kwa machozi mengi alilia kuonesha kujuta na msamaha wa kweli. 

Pale chini ya mti Efraim hakuonesha kukata tamaa kuhusu Elvine, hivyo kwa kutumia uwezo wa kichawi alimuita Erijin(Erika). Erijini alipofika alikuwa tayari kashajua kinachoendelea kule, hivyo alifika pale akiwa amejaa hasira.

“nani karuhusu huu mti wa nuruni kuota kwenye ardhi yetu” alihoji erjini kwa hasira sana. 

“hata mimi sijui imekuwaje maana sijawahi uona hata siku moja mpaka umekuwa kiasi hiki”

“Naomba mlinzi wa mazingira aitwe” Erijini alimpa amri baba yake

Efraim alifumba macho kisha akafumbua na baada ya kufumbua tu macho walimuona nyoka mkubwa sana mbele yao, mwenye rangi ya bluu ambaye alikuwa kasimamisha kichwa chake kama mshumaa unataka kuwashwa.

DAMU KWA DAMU, MOTO KWA MOTO” yule nyoka aliwasalimu

Erijini akatabasamu na kumshika yule nyoka shingoni na kuanza kumnyonga. Yule nyoka alipiga kelele za maumivu sana lakini Erijini hakujali mpaka Efraimu alipoamua kuingilia kati kwa kumvuta bintie ili amwachie yule nyoka maana alikwisha tambua kuwa Erijini alitaka kumuua yule nyoka kwababu ya hasira zake.

Yule nyoka baada ya kuachiwa alikuwa kashachubuka shingo kana kwamba kaunguzwa na moto au kachubuliwa na kisu. Na hapo hapo akabadirika na kuwa mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka kama 12. Yule mtoto alionekana kutetemeka sana na alikuwa kaumia sana sana lakini hakuwa nachakufanya maana hata kukimbia alishindwa alibaki tu kasimama huki kashikiria shingo yake iliyokuwa ikitoa damu.

“Unalijua kosa lako?” 

“Hapana mkuu”

“Aty nini?” Erijini alimkazia macho yule mtoto

Efrahimu akaamua kumuuliza yule mtoto.

“Wewe…. Huu mti unaujua?”

“Ndio mkuu”.. yule mtoto alijibu kwa hofu

“Ushawahi kuupanda juu yake hapo kabla?” 

“Ndi…ndio”

“Ushawahi kuyala maembe yake?”

“Hapana”

“Kwanini?”

“Kwasababu huu mti haujawahi zaa matunda na ulikuwa mti mkavu sana siku zote, hata siku chache zilizopita nilipita hapa sikuona tunda lolote na majani yote yalikuwa yamepukutika. Hata mimi leo nashangaa kuuona umestawi hivi, na unamaembe yaliyoiva, sijui imekuwaje kweli nasema ukweli”

“Kwahiyo unataka kutuaminisha kuwa ni mti wa miujiza huu sio?”

“Kama niishivyo mkuu, nahisi hivyo”

“Aya ondoka. Efrahim alimruhusu yule mtoto kuondoka pale”

Baada ya yule mtoto kuondoka, Erijini alijaribu pia kupanda mtini lakini haikuwa rahisi kwake pia. Na wakati wanahangaika pale chini, Elvine alikuwa akiwatazama tu.

********

Elimina na mjomba wa Elvine waliendelea kuishi pale lakini ajabu ni kuwa Edgar aliacha kabisa kuulizia habari za Elvine na wala hata hakuonesha kujali tena. Elimina aliamini huu ni muujiza tu wa Mungu lakini ki ukweli haikuwa hivyo. 

Siku moja wakiwa wanakula chakula cha jioni Edgar aliaanza kumwambia Elimina kuwa anampenda. Jambo hili lilimshangaza Elimina sana na alidhani labda mjomba anatania lakini kilichomshangaza zaidi ni pale ambapo Edgar alisema “acha kumuwaza Elvine maana hatorudi tena huyo”

“Uncle unajua alipo elvine sio?”

“kwaiyo kama najua? Ok, ndio najua, Elvine alikufa kisa tamaa maana alimpenda binti wa kuzimu”

Elimina akiwa na ujauzito ambao ulikua ukionesha kuhitaji kuleta kiumbe kingine duniani muda wowote maana miezi tisa ilikwishatimia, alishangazwa na maneno ya Edgar mpaka tumbo likashtuka.

Alijikuta akikosa nguvu na kudondoka chini ya kiti huku tumbo likiuma. Edgar pasipo huruma alimsogelea na kumpiga ngumi nzito tumboni. Ngumi ile iliongeza maumivu ya tumbo la Elimina. 

Elimina alishikwa na uchungu wa ghafra mbele ya Edgar, lakini Edgar alianza kucheka kisha akasema “sasa Elimina mama wacha mie niende nikanywe moja baridi huko kwa marafiki, halafu wewe liaaa liaaa ukichoka kufa na mwanao maana mlango nafunga dear…. Hospitali sio ya kwenda watu kama wewe. Au omba hata Mungu atume Malaika waje wakusaidie” 

Ilikuwa ni saa 7 mchana siku ya jumamosi sikuhiyo. Na isingekuwa rahisi kwa majirai kujua kinachoendelea pale ndani. Edgar alitoka pale ndani na akafunga milango yote

 kisha akaondoka zake.

Itaendelea………….

Kusoma sehemu ya 28 bonyeza hapa


Kusoma UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27 bonyeza hapa

Hadithi  hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            &, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255617653697.

Tu follow kwenye.

Facebook page>>> Add Value Network.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.


Popular posts from this blog

MAAJABU YA AKIBA

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.