MAAJABU YA AKIBA

Image
MAAJABU YA AKIBA Akiba (saving) ni kiasi cha fedha au rasilimali ambacho kimewekwa kwa matumizi ya baadaye, hata sasa kingeweza kutumika lakini umuhimu wake kwa kutumika baadaye ni mkubwa kuliko matumizi yake ya sasa. Hata katika biblia ``Mwanzo 41:35-36`` kama umewahi soma utaona Farao baada ya kutafsiriwa ndoto yake na kufahamu kuwa, imempasa kuweka akiba alilifanya hilo kwa uharaka ili kuhakikisha linaendelea vizuri ndio akamweka Yusufu kama msimamizi wa hili. Farao aliona kabisa kuwa nidhamu yake ya kujiwekea akiba haipo sawa hivo alihitaji msaidizi wa kumsaidia kama yeye alivyokuwa ndivyo tulivyo baadhi yetu siku za leo hatuwezi kujiwekea akiba ya vile tulivyo navyo. yaani huwa tunapenda kusema kesho itajisumbukia yenyewe,  Hata hivyo tangu zamani hata leo mataifa mbalimbali yamekuwa yakijiwekea akiba kwa manufaa na matumizi ya baadaye. Ukiangalia nabii Samweli alikuwa akijiwekea akiba na aliitoa pale Sauli alipomtembelea wakaila ile akiba ya chakula. Ni muhimu kujiw...

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

 


HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Ilipoishia..........

Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti...

Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa.

Sasa inaendelea......,

Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda kidogo alijikuta hana hata dalili ya maumivu wala ajali yaani kama kaponywa kwa namna fulani. Alijitazama vizuri ili kuhakiki kama yupo sawa hata woga ukaisha kabisa yaani akawa na ujasiri wa ajabu.

Edger alitabasamu na kisha akagonga geti. Elimina alishangaa baada ya kutazama kwenye CCTV camera na kuona Edger hajaja na gari wakati alimwambia yupo na gari lake. Haraka aliruhusu geti kufunguka kwa kutumia remote control ambayo iliunganishwa kwenye simu yake. Edger aliingia pale getini na kutazama mazingira kwa muda kidogo kisha akaingia ndani..

Alipoingia alikuta Elimina anamuandalia chakula. Akamtazama sana Elimina kisha akatabasamu na kusogea mezani kwaajili ya kuanza kula.

"Wooh! Naona binti yangu umefunzwa ukafunzika mama, chakula kinaita hata kabla sijala jamaniii"

"Asante sana mjomba"

"We ni mrembo sana aisee! Yaani Elvine huyu kijana alikuwahi sana, pengine asingekuwahi ningekuoa mimi wee binti mrembo"

"Hahaha sawa bwana mjomba nawe utani wako mmh!"

"Unadhani utani basi, kweli maana mabinti wazuri kama nyie ni wachache sana hapa Tanzania "

"Sasa wewe si unajua, mabinti wazuri wapo kwa yesu!. Halafu hata mkeo si binti wa kiringa?"

"Ndio binti yangu, ni kabinti tu fulani ka kiringa"

"Mmmh! Mjomba mbona mkeo unamdogosha sana hivyo?"

"Aah, michosho tu yule binti hana hata jipya?

"Hee makubwa!" Elimina alibaki kushangaa namna ambavyo Edger alikuwa akimsema mkewe kwa namna  ile maana alishawahi kusikia jinsi Edger anavyompenda mkewe. Edger alizungumza mengi sana mabaya tu kuhusu mkewe na wala hakuonesha japo jambo moja zuri kuhusu mkewe. Elimina alishangaa sana. 

Wakati wa mazungumzo yao yote Edger alikuwa anamsifia sana Elimina hadi akashtuka kidogo, lakini Elimina haikumpa shida sana kuhusu hilo maana alijua kabisa mjomba wake hajaokoka na kwa namna walivyokuwa wanaheshimiana alikuwa anamuamini sana kuwa hawezi kufanya jambo baya kwake kwahiyo walikaa pale sebuleni muda mrefu sana wakiwa wanapiga stori za hapa na pale. Katika mazungumzo yao yote Edger hakuacha kumsifia Elimina kila baada ya dakika kumi.

*.       *.        *.      *.     *.     *

Elvine aliishi na Elimina pasipo kujua sio Elimina halisia. Elimina ambaye kwa uhalisia alikuwa ni Efraim alijitahidi sana kuiga matendo mema mbele ya Elvine katika ardhi ile iliyojaa ukiwa na utisho. Elvine alitamani sana kurudi nyumbani lakini haikuwa rahisi. 

Kuna wakati alimwambia Elimina ajitahidi kumuombea, akianza tu habari za kuomba alikuwa anasahaurishwa hivyo anasahausahau, kwahiyo alikuwa anasahau alichokuwa anazungumza maana ardhi ile haikuruhusu maombi yoyote yenye jina la Yesu ndani yake na isitoshe walioikalia walikuwa ni watu wa ufalme wa giza.

Elvine aliishi na Elimina wa ardhi ile kwa mateso sana maana kuna wakati walilala njaa lakini Efraim aliyechukua sura ya Elimina hakuwahi shinda njaa japo mbele yake alionekana kushinda njaa. Efraim alikuwa anamtoroka Elvine mara nyingi  kwenda kwenye kazi zake mbalimbali pamoja na kula. Elvine kwake ilikuwa mateso na kama kifo hakikumtaka na kilikuwa kikimuepuka Kwa namna fulani maana alitamani hata kufa muda fulani. Alikuta Elvine na aliumia zaidi kuhusu Elimina maana aliona kama amemponza mkewe pasipo kujua zote ni njia za kumtesa kiakili yaani asipate muda wa kufurahi. Muda mwingi akiwa kule alitawaliwa na maumivu moyoni na uchungu na Elimina feki  alioneshwa kulia pamoja naye, lakini ukweli yalikuwa ni mauzauza tu maana Elimina yule hakuwahi kulia ila kwakuwa Elvine alipungukiwa nguvu za Mungu hakuweza kutambua chochote cha Rohoni.

Efraim Kuna wakati alimnyonya Elvine damu pasipo yeye kujua jambo ambalo lilimfanya Elvine kudhoofika zaidi na mara nyingi alimfanyia hivyo baada ya kumlevywa kwa usingizi mzito. Elvine alikuwa akijikuta muda fulani analala tu ghafla pasipo kutegemea na pindi anapoamka anajikuta kachoka sana na mwili umeishiwa nguvu, lakini hakujua kwanini jambo hilo lilimkuta.

Kuna siku Efraim alijigeuza mnyama wa polini na kumuadhibu Elvine Kwa kumkwarua na makucha katika kupambana naye ili mradi tu ateseke mpaka afe maana wao Kwa nguvu zao walishindwa kumfanya chochote.

Elvine alikuwa akila mizizi na matunda poli katika mji ule wa ajabu. Na matunda hayo yalikuwa machungu mno na wala hakuona uchungu huo saana kwaajili ya njaa aliyokuwa nayo. Mateso yalikuwa makali mno, alilala popote; chini ya miti, juu ya miti, kwenye nyasi' hata juu ya miti.

Kuna wakati njaa ilizidi na akawa Hana chakula na Elimina. Elimina akajifanya kuzimia Elvine aliona nyoka anapita alijikaza na kisha akamuuwa nyoka yule kwa kutumia kijiti, aliwasha moto kama walivyofanya mababu wa kale na kisha akamchoma yule nyoka na kumpepelekea mkewe kisha wakala yule nyoka. 

Elvine aliuwa nyoka lakini hakuwa nyoka. Elvine aliuwa mtu yaani alikula nyama ya mtu kabisa. Alishangaa sana radha ya ile nyama lakini hakujua masikini kama ni mtu. Kuna wakati maombi ya mkewe Elimina duniani yalipozidi alipata urahisi wa maisha yaani, alikuwa haoni njaa siku nzima na hahisi kuchoka na kuna wakati alikuwa anajisikia vizuri na hata matunda alikuwa anayapata mazuri lakini kuna wakati mambo yalikuwa magumu sana kwa upande wake.

Miezi ilizidi kwenda na hatimaye ikafika miezi tisa akiwa katika ardhi ile na Elimina feki. Alikonda akawa moja kama sio one. Kufa hakufa ila chamoto alikiona. Akiwa kule Elvine alijuta, najilaumu, kajiadhibu na kajifunza vingi lakini ambacho hakufanya ni kumkufuru Mungu maana aliona yote yanamstahili kwakuwa makosa ni ya kwake.

Siku moja Elvine akiwa anatembea tembea katika msitu akiwa na Elimina alifika mahali fulani ambapo palimshangaza sana maana ni kama mahali ambapo amewahi kufika yaani ni kama anakumbukumbu fulani na eneo hili japo ilikuwa katikati ya msitu na kulikuwa na miti mingi mirefu na vichaka vya namna zote. Akiwa anajaribu kutafakari eneo hilo alimwambia Elimina kuwa eneo lile lina muembe wenye maembe matamu sana. 

Kwa mshangao Elimina yule alimuuliza "umelijuaje eneo hili? Umeshawahi kufika?"

"Nadhani nimewahi fika, japo sijui ni lini na ilikuwaje!" Waliposogea mbele kidogo kweli walikutana muembe wenye maembe mengi mno, muembe ulikuwa mrefu lakini kwa namna ulivyo Kaa mtu yeyote angeweza kuupanda hata mtoto mdogo. Elvine alikuwa wakwanza kupanda juu lakini Elimina alipotaka kupanda pale alipigiwa shoti na ule mti jambo ambalo hata yeye alilishangaa maana hata ule mti hautambui na upo kwenye ardhi yao. 

Kwakuwa Elvine hakuona tukio la Elimina kupigwa shoti, Elimina alijitetea kuwa hawezi kupanda kwenye ule muembe maana miguu inamuuma na amechoka sana. Kwahiyo Elvine akawa anachuma maembe na kumrushia Elimina pale chini.

Wakati anachuma maembe kuna embe moja alilishangaa sana maana lilikuwa jekundu mno akalikazia macho like embe na akataka kulichuma lakini akasita maana wekundu wake ulikuwa tofauti na maembe yote ya ule mti. 

Akakaa dakika kama mbili analitazama baadaye akaamua kulichuma na kuanza kulila. Akiwa anakula like embe alitazama chini akiwa pale juu na ndipo kumbukumbu zilipomjia. Alikumbuka ndoto moja aliyoiota siku nyingi zilizopita akiwa duniani.

Ilikuwa hivi:-

Elvine alikuwa ameketi juu ya mti katikati ya poli fulani akiwa na amani sana. Akiwa pale aliweza kuona umbali mrefu sana. Alishangaa baada ya kumuona mtoto wa kiume mwenye umri kama wa miaka 7 hivi anazunguka zunguka mule polini. Akacheka sana halafu akasema "Kuna vitoto vya ajabu Duniani jamani. Sasa angalia huyu mtoto anataka nini huku polini muda huu?" Akatabasamu akachuma embe lililoiva kwenye ule mti na kuanza kulila.

Yule  mtoto alikuwa akijiimbia "ukutiukuti" mwenyewe. Elvine akamtazama kwa makini yule mtoto na akahisi kama anamfahamu. Kwakuwa alikuwa mbali hakuweza kumtambua vizuri. Aliacha kumtazama yule mtoto huku akaendelea kula maembe matamu yaliyokuwepo kwenye mti  mkubwa aliokuwa ameketi.

  Moyoni ni kama aliambiwa amlinde yule mtoto lakini hakujali maana maembe yalimpendeza zaidi. Na kwakuwa hakuona hatari yoyote mahali pale hakumzingatia sana yule mtoto. Baada ya muda alipomtazama tena yule mtoto hakumuona. Akajiuliza kaemda wapi lakini hakupata majibu na wala hakuweza kumuona.  

Kidogo alipatwa na wasiwasi akahofia yamkini kaliwa na wanyama au kuna jambo baya limemkuta. Aliamua kushuka mtini na kuanza kumtafuta. Paaap! Alimuona yule mtoto yupo mbele yake. Alishtuka kidogo lakini akaona kawaida. Lakini sura ya yule mtoto alihisi anaifahamu kabisa.

     Alimsogelea mtoto yule huku anatabasamu Ili amuulize maswali. Alipopiga hatua kusogea na yule mtoto alisogea kwake. 

"Unaitwa nani mtoto?"

"Wewe" yule mtoto alijibu akiwa siliazi sana.

..,........ Yule mtoto alimuachia Elvine na kuanza kuondoka. Nyuma yake yule mtoto alikuwa kavaa shati iliyokuwa imeandikakwa maandishi mekundu yaliyorembwa vizuri sana * YOU MUST WIN THE BUTTLE BEFORE THE BUTTLE WINS YOU". (Rejea sehemu ya 17)

              Elvine akumbuka kila kitu, akajitambua na akakumbuka kila kilichotokea akiwa kwenye Ile ardhi akajiuliza kuhusu Elimina na akatambua ukweli kuwa yule alienaye hawezi kuwa Elimina maana kuna vitu vingi alivyofanyiwa vibaya ambavyo Elimina asingeweza kufanya....

Swali; Elvine kajitambua, je atarudi Duniani? Nani atamsaidia?

Itaendelea......


Hadithi  hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            &, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.

Tu follow kwenye.

Facebook page>>> Add Value Network.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.


Comments (2)

Loading... Logging you in...
  • Logged in as
Hii story ni nzuri saana kwani inafunzo kubwa ndani yake
Ubarikiwe sana kwa simulizi nzuri

Post a new comment

Comments by

Popular posts from this blog

NJIA 7 ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.