MAAJABU YA AKIBA

Image
MAAJABU YA AKIBA Akiba (saving) ni kiasi cha fedha au rasilimali ambacho kimewekwa kwa matumizi ya baadaye, hata sasa kingeweza kutumika lakini umuhimu wake kwa kutumika baadaye ni mkubwa kuliko matumizi yake ya sasa. Hata katika biblia ``Mwanzo 41:35-36`` kama umewahi soma utaona Farao baada ya kutafsiriwa ndoto yake na kufahamu kuwa, imempasa kuweka akiba alilifanya hilo kwa uharaka ili kuhakikisha linaendelea vizuri ndio akamweka Yusufu kama msimamizi wa hili. Farao aliona kabisa kuwa nidhamu yake ya kujiwekea akiba haipo sawa hivo alihitaji msaidizi wa kumsaidia kama yeye alivyokuwa ndivyo tulivyo baadhi yetu siku za leo hatuwezi kujiwekea akiba ya vile tulivyo navyo. yaani huwa tunapenda kusema kesho itajisumbukia yenyewe,  Hata hivyo tangu zamani hata leo mataifa mbalimbali yamekuwa yakijiwekea akiba kwa manufaa na matumizi ya baadaye. Ukiangalia nabii Samweli alikuwa akijiwekea akiba na aliitoa pale Sauli alipomtembelea wakaila ile akiba ya chakula. Ni muhimu kujiw...

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 25.

 

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 25.

Ilipoishia......

"Ooh asante YESU maneno yako yamenipa na kiburi juu ya hawa watu, sahizi siwaogopi na wala hawaniwezi na Elvine lazima arudi haijarishi kwa namna gani? Nataka nimpe Mungu Sababu ya kumsaidia Elvine" Elimina akafuta machozi na akawa kajua aombe nini kwa sasa maana hataomba tena maombi ya kulalamika na maombi ya kwanini!! Akatabasamu alafu akasema " SASA VITA IANZE NAJUA SILAHA YANGU...

Kama hujasoma sehemu ya 24 bofya hapa.

Sasa inaendelea....

Elimina baada ya kujipa moyo akapata kiburi mbele ya hao maadui zake maana alijua umuhimu wake katika kumlinda Elvine. Aliamua kutoka pale ndani na kufuta machozi yake na akajisemea sasa sitalialia tena nimaombi ya vita mwanzo mwisho. 

Aliamua kutoka na kwenda dukani kwake ili kuendelea na kazi zake. Ilikuwa imepita wiki sasa pasipo yeye kufika dukani kwake hivyo hata wateja walipungua maana kila walipokuja hawakumkuta. Alifungua duka lake akakaa nje ya duka mpaka jioni, japo alipata wateja wachache lakini yeye lengo lake ni Erika aje maana alijua tu lazima atakuja kumdhihaki Kwa kujifanya hajui chochote kuhusu Elvine. 

Ilipofika saa 2:30 usiku Erika alikuja dukani kweli, tena akiwa mpole sana kama mwana wa kondoo tena mwana wa mwisho wa uzeeni. 

"Dada jamani ulikuwa wapi wiki nzima? Nimekukumbuka sana. Kaka Elvine pia nilienda kule kazini kwake naambiwa hayupo hajafika kazini sijui shida nini?"

"Kwanini hukuja kututazama nyumbani kama umetukumbuka kweli" Elimina alimuuliza huku kamkazia macho sana usoni. 

"Nyumbani.... Kule mbali kila nilipotaka kuja ratiba iliingiliana" 

"Aisee kweli?.

"Ndio dada"

"Sasa kama uliweza kwenda mpaka kazini kwa Elvine ulishindwaje kuja nyumbani? Maana kule mbali zaidi?"

"Jamaniii dada mbona maswali mengi hivyo?"

"Ni mengi ndio lakini si yanajibika tu, we nijibu"

"Mmh! Basi ntakuja kesho nyumbani"

"Uje maana huwezi jua vizuri Elvine alipo pengine hata yupo nyumbani"

"Yupo nyumbani?" Erika aliuliza kwa mshtuko kidogo

"Vipi kwani! Mbona kama umeshangaa?"

"Hamna dada, ni... Ni.... Yaani... Ooh hamna nimeshangaa maana hata simu zangu hajibu"

"Baada ya kuona hajibu mbona mimi hujawahi kunitafuta sasa?"

"Samahani dada bhana na wewe! Hahahah" Erika baada ya kuona maswali yamekuwa magumu kwake akaanza kujichekesha chekesha ili aage kisha aende zake maana alijua Elimina hajui chochote kuhusu yeye na alijua Elimina atakuwa dhaifu sana na mwenye huzuni lakini alishangaa maana alichotarajia na alichikutana nacho ni tofauti sana. 

Aliamua kujitetea kuwa anawahi nyumbani. Elimina akamwambia kama anawahi nyumbani haina shida lakini kwakuwa muda umeenda basi Elimina atampeleka mpaka nyumbani na gari lake. Binti alishangaa kwanini Elimina anataka afike kwao usiku ule. Akaona itakuwa hatari maana Elimina anaonekana kama kuna kitu anafahamu. Alijifanya kukubali Elimina wakati anafunga duka Erika alikimbia na kuondoka zake, Elimina alipogeuka hakumuona; Elimina alitabasamu na kufunga duka kisha akarudi nyumbani.

Elimina aliamua kutafuta mfanyakazi na kumkabidhi duka kisha yeye akaanza kusimamia kampuni ya mumewe Elvine. Elimina hakutoa taarifa mahali popote kwa ndugu zake wala kwa ndugu wa Elvine kuwaambia Elvine kapotea maana alikuwa anaomba Kila siku na maombi yake yalikuwa ya vita kwa kuamini kuwa Elvine atarudi.

Alipopigiwa na ndugu zake na Elvine kuulizwa kwanini Elvine hapatikani alikuwa anasema simu ya Elvine inashida na alipoambiwa yuko wapi alijibu kwa sasa sipo nae jirani ila akirudi ntampa taarifa kuwa ulimtafuta. Alifanya hivyo kwa kila aliyemtafuta Elvine na siku zikazidi kwenda. Erika hakuthubutu kuja tena dukani, ofisini wala nyumbani kwa Elimina maana alishapata wasiwasi kuwa Elimina anapambana na kitu anachokijua na sio kama alivyojua mwanzo. 

Miezi mitatu ilipita Elvine hakurudi na ndipo Edger mjomba wake na Elvine alipoamua kuja Dodoma kumtafuta Elvine maana aliona hampati japo shughuli za ofisini zilionekana kwenda vizuri na pesa iliingia kwenye account vizuri ila alikuwa na mambo mengi sana ya kiofisi kuzungumza na Elvine. 

Alikuja mchana kutoka Iringa na alikuja bila taarifa jambo ambalo kwa Elimina hakulitegemea. Edger alipofika pale ofisini alishangaa sana kumkuta Elimina ndiye anafanya kazi kama meneja. Lakini hakutaka kujaji moja kwa moja maana alijua namna ambavyo Elvine na mkewe wanavyopendana kwahiyo sio ajabu sana hawa watu kusaidiana kazi kama hivi. 

"Elimina mama nakuona katika uwepo wa Elvine hapo" Edger alimsalimu kwa kumchangamkia, 

Elimina alipata mshtuko mpaka akahisi tumbo linauma na mtoto anatetemeka baridi tumboni maana ujauzito wake ulikuwa na miezi mitatu sasa. Aliogopa lakini akajikaza na yeye akatabasamu na kumjibu Edger "ooh! Mjomba karibu sana, shikamoo"

"Marhabaaaaaa mwanangu, vipi lakini Elvine yuko wapi maana sijaongea naye muda mrefu na nina mambo mengi ya kujadili naye. Elimina alipata utata ajibu nini maana alishaona dalili za kudanganya, na alijua kabisa akidanganya tu 'kibarua kinaota nyasi' yaani Elvine atapata shida zaidi kule aliko, akatulia kidogo kisha akatabasamu.

"Sasa mjomba twende nyumbani kwanza alafu hayo tutazungumza maana Elvine kaenda mbali kidogo na aliko mawasiliano ni shida kidogo"

"Yaani kasafiri?"

"Mmmmh, sijui nisemaje ila kwasasa huwezi kumpata na hata mimi huwa simpati"

"Hee!, kaondoka lini na safari yake inahusu nini?"

"Nii.... Aah mjomba naomba hayo tutaongelea nyumbani"

"Alafu ninavyokutazama naona kama umepungua, shida nini au Elvine anakutesa?"

"Ooh hapana mjomba Elvine ananipenda sana, hawezi kunitesa"

"Sasa unamawazo ya nini?"

"Mbona hamna mjomba mimi nipo sawa kabisa"

"Sawa basi mimi nitarudi badae kuna watu nikawatembelee, alafu ntakuja nyumbani moja Kwa moja, sawa binti yangu?"

"Sawa mjomba hakuna tatizo" Elimina alijibu lakini moyoni mwake alikuwa na mawazo mengi sana, aliwaza ni kwanamna gana atakavyo mkwepa mjomba wake Elvine asijue chochote kuhusu Elvine. Alijipa moyo huku akijisemea 'Ee Mungu nisaidie'

Alirudi nyumbani saa 2:30 usiku. Alifika nyumbani akapika na baada ya muda Edger akapiga simu kumuuliza kama kasharudi nyumbani ili naye aje kutoka Kwa rafiki zake alipokuwa ameenda, Elimina alijibu ndio nimerudi. 

Edger wakati anakuja njiani aliona kuna binti kalala katikati ya barabara akashangaa. Na kwa haraka akajua labda yule binti kagongwa na gari au labda kafanyiwa vibaya na wahuni, akaamua ashuke ili akajue ni nani huyo na nini kimemkuta. Alishuka taratibu huku akiangalia usalama wake maana alihofia usije ukawa mtego pia, maana njia ile haikuwa na magari mengi kwakuwa mtaa waliokuwa wanakaa akina Elvine ulikuwa pembeni kidogo ya mji na uliitwa mji mpya kwa kwakuwa watu ndio kwanza walikuwa wameanza kujenga hiyo sehemu na nyumba zikizojengwa huko zilikuwa za watu wenye pesa. Kwahiyo hakukuwa na watu wengi sana wala kelele bali kila mtu na nyumba yake. 

Edger alisogea mpaka karibu na yule binti kisha akamgusa maana alikuwa kalala kifudifudi, akataka kumgeuza. Alikuwa anamgeuza huku akimuita "binti, binti... Umepatwa na nini... Hey.." yule binti hakutikisika wala kutoa sauti yeyote. Yaani kana kwamba kazimi japo hakuwa na jeraha wala  damu popote ya kuashiria kugongwa na gari, kwahiyo Edger akashindwa kujua hasa tatizo la binti yule ni nini!.

Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa kwenye mabega akiwa ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti...

Kusoma sehemu ya 26 bofya hapa

Hadithi  hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            &, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.

Tu follow kwenye.

Facebook page>>> Add Value Network.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.


Comments (2)

Loading... Logging you in...
  • Logged in as
Kazi nzuri
1 reply · active 48 weeks ago
Elias Migongo's avatar

Elias Migongo · 48 weeks ago

Ahsante sana ndugu

Post a new comment

Comments by

Popular posts from this blog

NJIA 7 ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.