MAAJABU YA AKIBA

Image
MAAJABU YA AKIBA Akiba (saving) ni kiasi cha fedha au rasilimali ambacho kimewekwa kwa matumizi ya baadaye, hata sasa kingeweza kutumika lakini umuhimu wake kwa kutumika baadaye ni mkubwa kuliko matumizi yake ya sasa. Hata katika biblia ``Mwanzo 41:35-36`` kama umewahi soma utaona Farao baada ya kutafsiriwa ndoto yake na kufahamu kuwa, imempasa kuweka akiba alilifanya hilo kwa uharaka ili kuhakikisha linaendelea vizuri ndio akamweka Yusufu kama msimamizi wa hili. Farao aliona kabisa kuwa nidhamu yake ya kujiwekea akiba haipo sawa hivo alihitaji msaidizi wa kumsaidia kama yeye alivyokuwa ndivyo tulivyo baadhi yetu siku za leo hatuwezi kujiwekea akiba ya vile tulivyo navyo. yaani huwa tunapenda kusema kesho itajisumbukia yenyewe,  Hata hivyo tangu zamani hata leo mataifa mbalimbali yamekuwa yakijiwekea akiba kwa manufaa na matumizi ya baadaye. Ukiangalia nabii Samweli alikuwa akijiwekea akiba na aliitoa pale Sauli alipomtembelea wakaila ile akiba ya chakula. Ni muhimu kujiw...

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 24.

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 24.

Ilipoishia....

" Baba nimeshakwambia, ufalme wa hawa wenzetu unanguvu kuliko sisi. Huoni mpaka sasa Elvine tunae, lakini bado mtu mmoja tu huko duniani anasababisha tusikamilishe mambo yetu?. 

Hili swala linaniuma sana kuona tunafeli mbele ya hawa watu. Yaani kumpata Elimina sio kazi nyepesi, maana analindwa mno na ufalme wake na anamsimamo sana yule mwanamke. 

Ila mimi nakuahidi baba naenda kumuangusha na akianguka, atalipia haya yote aliyoyafanya kwenye ufalme wa giza nasema atalipia, tena naapa ntafanya ajute na ajute tena labda asijichanganye" Erijini (Erika), aliongea kwa uchungu na hasira mpaka macho yakageuka rangi na kuwa rangi ya bluu....

Kusoma sehemu ya 23 bofya hapa.

Sasa inaendelea.........

 Efraim hakutaka kubishana sana bali aliamua kufanya sawasawa na hitaji la binti yake. Erijini alitoweka na kurudi Duniani kutoka kwenye ardhi iliyomficha Elvine Kwa kazi moja kubwa ya kumuangusha Elimina. 

Elimina alikuwa haachi kuomba kwaajili ya mumewe na pia hakutoa taarifa sehemu yoyote kuhusu kilichojitokeza kwa Elvine maana aliona itakuwa aibu sana kama familia ya Elvine itajua kilichomkuta Elvine na hasa alihofia namna ambavyo baba yake Elvine atakavyo chukia kwakutokupewa taarifa, kama Elvine kaasi huduma iliyomleta Duniani. Elimina alijipa moyo kuwa Elvine atarudi na hatosema jambo mpaka Elvine arudi.

Siku moja Elimina alikuwa akiwaza sana ghafla akapigiwa simu, alipopokea akagundua kuwa ni baba yake mkwe yaani Edwin ndiye anaepiga aliogopa sana. Akajiuliza atajibu nini kuhusu Elvine maana simu ya Elvine ilikuwa haipatikana na haijulikani iko wapi. 

Akawaza maneno ya kuongea. Kidogo apange na uongo wa kumtetea Elvine ili tu baba asijue chochote lakini kumbe ulikuwa ni mtego maana aliyekuwa anapiga alikuwa ni Erika ila aliweka mauzauza tu kwenye simu.

Elimina alianza kuwaza mengi lakini wakati anawaza alikuwa anahisi moyo unawaka moto na roho yake inamwambia kuwa makini usifanye maana unawindwa. Alitulia Kwa muda pasipo kupokea simu yake ilikuwa inaita mezani. Aliitazama kwa muda kidogo huku akiwa anamtafakari. Baada ya muda kama wa dakika moja na nusu aliipokea simu akiwa anatetemeka màana moyo wake unauchungu mno kuhusu Elvine lakini akaamua kujikaza.

"Haloo baba" aliongea sauti yenye mikwaluzo iliyojaa hofu,

"Ooh mka mwana wangu mzuri hujambo wewe?"

"Sijambo baba, jamani mwanangu nimewakumbuka mno, vipi Elvine mzima maana namtafuta hata hapatikani na nimemtafuta sana siku mbili hizi na sijampata"

"Ooh ! Elvine yupo safarini na mimi pia hata simpati, nadhani alipo kuna shida sana hasa ya mawasiliano naomba tumuombee tu baba" Elimina machozi yalianza kumtoka lakini alijikaza sauti isioneshe uchungu alionao wala isioneshe kuwa analia ila moyo wake tayari ulijaa ganzi na simanzi pamoja na maumivu makali kama alietoneshwa kidonda kikubwa na mtu asiyefaa. 

"Unamaana gani? Kwani kaondoka lini?

"Kaondoka jumapili baba?"

"Alafu sauti Yako haipo sawa mkwe! Unalia? Au unamafua?"

Elimina akaona hawezi kusema ukweli hapa akawa anajiandaa kudanganya, lakini wakati wote huo Elvila malaika wa Elvine alikuwa yupo pale lakini Elimina hakuwa anamuona. Elvila akaona sasa Elimina yupo hatarini kutekwa na yeye kupitia mambo madogo sana ya kimkakati zaidi. Akaamua kumsaidia kuongea kwa kumuingilia katika usemi wake.

" Hii sio biashara yako, mwana wakifalme huwa halii bali hutoa machozi kwakuwa anakaribia ushindi, kwahiyo mimi silii ila natoa machozi ya ushindi, na pia siogopi vita maana najua mimi ni wakushinda siku zote" Elimina alijikuta kasema hayo maneno Kwa sauti ya ujasiri sana mpaka yeye mwenyewe akajishangaa.

" Sawa mkwe, lakini Elvine hivi huduma yake inaendaje mpaka sasa?"

Elimina alipopiga hesabu akaona hana jibu. Akatamani adanganye tena kwa kusema inaendelea vizuri lakini akawa anasita maana haipo. Elvila akamuingilia tena katika usemi wake.

"Hakuna huduma ambayo ingeendelea pasipo utayari. Elvine hakujiandaa lakini alirudi salama huko aliko kuwa bila shaka atafungua huduma na atakuwa na nguvu sana tena kuliko mwanzo. 

Japo kwa sasa bado hajajipata. Ila nakuahidi hivi karibuni Elvine atarudi na hakuna atakayeweza kumzuia maana atakuwa kajifunza nini maana ya kutumikia huduma kikamilifu, yaani labda nisema yupo kwenye somo anakula kipindi ili aje afanye kazi vizuri"

Simu ilikatwa ghafla maana yale maneno yalimkera sana Erika. Erika alishangaa kila mtego anaoweka Elimina anautegua. Elimina hakuwa anajua kama ni mtego lakini akawa anawaza( hivi mimi nilikuwa naongea nini na baba mkwe, mbona nimemtumia maneno ya kejeri kwa namna fulani? 

Hivi mimi uchungu wangu ndio umenifanya namjibu baba mkwe kwa mitego hivi! Kwanza ujasiri huu nimeutoa wapi, asije akaniwazia vibaya!) Aliwaza mengi lakini alimkumbuka Elvine machozi yanakosa kizuizi.

Alikuwa amekaa kwenye sofa lililokuwa pale chumbani kwao akaona tayari halikaliki. Hakuona njaa wala hakuhisi kuchoka kuongea. 

Aliamua kukaa chini sakafuni na kuanza kulia tu maana kaomba kachoka sasa. Alikaa akajikunja na kujilaza sakafuni. Elvila akamuhurumia sana, akaamua kujidhihirisha kwake ili amtie moyo.

Elimina wakati kajikunja pale analia maana hajui hata aombe nini alihisi kaguswa kichwa na mtu akashtuka. Aliamka haraka kwa kuhisi labda Elvine karudi.

 Akamtazama pembeni na kumbe sivyo alivyodhani bali ni malaika wa Nuru. Alitazama na kumtazama malaika kwa muda na machozi yake yakaongezeaka zaidi. Malaika yule akamuhurumia sana.

"Elimina usilie sana maana maombolezo Yako yamekuwa makuu mno. Mimi naumia sana kuona wewe unateseka Kwa kosa ambalo hujafanya na hata hukushiriki" 

" Hapana ni makosa yangu pia, labda sikuwa namuombea Elvine vizuri au labda na mimi sikusimama kwenye zamu yangu kama mke bora na ndio maana hata Erika alitangulia kwanza kuja kwangu kunishawishi ili ampate Elvine. 

Nahisi hatia.... Nimeshiriki kumuangusha mume wangu, yaani mimi... mimi hapa Elimina ni sababu ya haya pia kumkuta Elvine, nahisi hatia, najuta kumfahamu Erika, natamani siku zirudi nyuma lakini kivipi sasa? Hebu niambie kivipi, nifanyaje mimi, nimekata tamaa mimi ni heri na mimi nife tu..."

"HAPANA!!!" malaika yule alimkemea tena kwa sauti ya ukali mpaka Elimina akashtuka kidogo.. 

" Elimina, hapana usiwaze kufa, usijilaumu, wala usikate tamaa na usiogope, falme ya Nuru na Giza lazima zipigane sikuzote lakini nafasi ya kushinda unayo. Hivi unajua Elvine hawezi kuguswa na kiumbe chochote bila wewe kudhibitiwa?"

"Hapana sijui, na kwanini iwe hivyo?"

"Mke na mume ni mwili mmoja, wewe nisehemu ya Elvine, sasa unadhani Elvine anauliwaje wakati mwili na roho ya Elvine ipo sehemu mbili?"

"Unamaana gani? Bado sijaelewa" Elimina alifuta machozi na kukaa vizuri pale chini ili apate kulisikia neno hili kutoka Kwa Elvila.

"Mume na mke ni mwili mmoja kwa watu wawili, nafsi zao huungana na Mungu hueshimu hilo. Elimina maombi yako na kutokukata tamaa kwako kunaweza kumrudisha Elvine maana wewe ni sehemu ya mwili na nafsi ya Elvine. 

Kwahiyo unanguvu juu yake na juu ya maisha yake maana hawawezi kumuuwa Elvine wakati nafsi ya Elvine imedhoofishwa upande mmoja tuna upande wa pili ipo na nguvu sana"

"Hii inamaana gani? Yaani Elvine hawezi kufa ila mimi ndio ninaweza kumuua Elvine au kumfanya Aishi si ndiyo?" 

"Na hiyo ndiyo maana yangu Elimina. Wewe bado unamlinda yule maana wewe na yeye ni mtu mmoja mbele za Bwana. Kwahiyo jipe moyo. Ila hakika hukosei hata kidogo yaani tunza utakatifu wako. Wewe ni ufunguo wa pekee ambao Mungu anataka autumie kwaajili ya Elvine"

"Aty nini? Mungu? Kama Mungu anaweza kumsaidia si amsaidie tu, kwanini mpaka sasa kamuacha anateseka Elvine wangu kama anaweza kumsaidia! Kwani si...".

"Elimina, Mungu hawezi kumsaidia mtu pasipo sababu, Elvine kakosea sana na ni mkosaji kweli. Lakini sio kwamba Mungu hampendi. 

Hivi unajua kuwa shetani ni dhaifu sana, na ndio maana huwa anapenda kulaumu sana, yaani Mungu kampa mtu uwezo wa kuamua mwenyewe njia gani apite ili kuonesha namna alivyo fair sana. 

Lakini wewe kama mwanamke unaweza kumsaidia Mungu kupata sababu ya kupambana na ufalme ule kwakuwa Mungu atamsaidia kwa point moja. "SIWEZI RUHUSU MWANANGU ALIE" 

"Ooh!! Sasa nimeelewa vizuri sana! Kumbe!"

"Na ndiyo maana kuna wakati ukimuombea sana mtu kutoka huwa anaokoka, maana sababu ni wewe, yaani, Mungu anamwambia shetani "SIJAKUNYANG'ANYA MTU BALI NIMEMSAIDIA MWANANGU KWA KUMWOKOA MTU HUYU, Kwahiyo Elimina wewe  inatakiwa utumike kama sababu ya kumrudisha Elvine tena kwa kuomba bila kuchoka wala usikate tamaa sawa?"

"Ooh asante YESU maneno yako yamenipa na kiburi juu ya hawa watu, sahizi siwaogopi na wala hawaniwezi na Elvine lazima arudi haijarishi kwa namna gani? Nataka nimpe Mungu Sababu ya kumsaidia Elvine" Elimina akafuta machozi, akajua aombe nini kwa sasa maana hataomba tena maombi ya kulalamika na maombi ya kwanini!! Akatabasamu halafu akasema " SASA VITA IANZE NAJUA SILAHA YANGU....

Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa


Simulizi  hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            &, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.

Tu follow kwenye.

Facebook page>>> Add Value Network.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.


Comments

Loading... Logging you in...
  • Logged in as
There are no comments posted yet. Be the first one!

Post a new comment

Comments by

Popular posts from this blog

NJIA 7 ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.