HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26. Ilipoishia.......... Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti... Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa. Sasa inaendelea......, Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23.

 

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23.

Ilipoishia......

Alipofika nje, alimkuta Elimina katahamaki sana tena anahasira sana. 

"Umefanya nini Elvine? Elimina aliuliza kwa ukali sana tena hadi macho yalikuwa mekundu kama damu kwaajili ya kujaa hasira....

Swali; kwanini Elimina anahasira? Na Elimina huyu anasiri gani na nyumba iliyoungua moto?

Kusoma sehemu ya 22 bonyeza hapa

  Sasa inaendelea......

Elvine alikuwa anatetemeka  kwa hofu ya yale anayoyaona lakini alistaajabu kuona ni kama mkewe hajali sana kuhusu yeye. Alimtazama kwa makini sana mkewe akiwa anajaribu kutafakari kwanini anaonekana kuwa na hasira juu yake. Elimina akajishitukia

"Hey, wewe! Nini sasa unanitazama hivyo?"

"Nakutafakari sipati majibu!'

"Nimefanyaje kwani?"

"Hamna ila sijajua kama umenihofia mimi au hilo swali lako linamaana gani?

"Elvine baba sina maana hiyo uliyoelewa wewe kabisa. Shida yangu mimi umefanya nini mpaka unataka kuhatarisha maisha Yako namna hii. Hujui namna gani mimi nimeogopa baada ya kuona nyumba inaungua. Kiukweli nilihisi sitakuona na ndio maana sipo sawa kabisa" Elimina aliongea maneno hayo huku machozi yakianza kumtiririka mashavuni.

Elvine alimuonea huruma mkewe hivyo akamkumbatia. Wakati akiwa amekumbatia Elimina alishangaa kuona mwili wa Elvine ni wabaridi kama mtu asie hai vile, na moyo wake pia ukawa hauna amani lakini hakumuuliza chochote. Wakiwa pale wamekumbatiana Efraim alikuja akiwa kama ametoka mahali fulani na wala sio ndani ya ile nyumba.

Alifika pale akiwa kawaka sana. Lakini Elimina alimkazia macho sana yule baba kabla hajasema chochote. Efraim akawatazama kisha akawaambia "mnaona sasa mlichokifanya? Sasa mtajua pa kwenda"

Elimina akaongea Kwa upole sana huku akiwa bado na kwikwi kwaajili ya uchungu alionao kuhusu kilichojitokeza. " sasa kaka yetu unadhani sisi tutaenda wapi saa tisa za usiku hizi? Sisi ni wageni huku, tunatafuta njia ya kurudi nyumbani, hatuna uwezo wa kuona njia pasipo wewe, ni kweli tumekusabababishia hasara lakini sasa tunafanyaje? Tusaidie!!"

"Mtajua wenyewe nasema mimi hainihusu kabisa, yaani umenisababishia hasara kubwa mno ambayo siwezi hata kuelezea, naomba muende sitaki kuwaona mbele yangu"

"Hivi ni kweli kabisa unamaanisha?

"Sina utani katika hili"

"Lakini...." kabla Elimina hajamaliza yule baba alifoka kwa sauti kubwa.. "nasema ondokeni kwangu!!!!"

Elvine aliogopa sana na moyo wake uliamini kuwa sasa kweli yupo njia ya jehamu na wala hakuna wa kuwapa msaada. 

Lakini akiwa anawaza akakumbuka kuwa wakati akiwa anatoka ndani aliona kuna mtu anamuombea katika picha iliyoonekana kwenye moto. Lakini hakuwa anakumbuka ilikuwa taswira ya nani. Yaani, kiufupi Elvine alikuwa anasahausahau kila baada ya dakika kadhaa.

Elvine alimtazama mkewe, akamuhurumia maana alijua kabisa kuwa Elimina Hana hatia ila chanzo ni yeye ila hakujua imekuaje Elimina kuingia kwenye ardhi hii ya ajabu. Elimina alianza kulia Kwa uchungu mno hadi akampigia magoti Efraim lakini Efraim hakusikia chochote ila aliwataka waondoke.

Waliamua kuondoka usiku ule wa giza nene wasijue wanakoelekea. Walipofika mahali fulani waliamua kukaa chini ya mti fulani karibu na msitu wakiwa wanatiana moyo. Wakiwa pale chini Elvine alisinzia wala hakujua kasinziaje maana kwa mambo waliyokutana nayo mtu kulala kizembe ingekuwa sio rahisi. 

Wakati Elvine akiwa amelala Elimina hakupata usingizi kabisa. Akawa anatazama huku na huko kuhakikisha usalama upo. Akiwa anawaza akaona mtu anakuja akiwa anawaka moto mwili mzima kama mfano wa malaika fulani  alianza kutetemeka na kuogopa. 

Kadri yule mtu alivyosogea na ndivyo mwanga ulivyozidi mwili wote ukiwaka moto (alikuwa anakuja). Elimina akaanza kumwamsha Elvine kwa nguvu huku akimtikisa kwa pupa.

"Elvine baba amka, amka... Onaaaa..  Mimi naogopa, amka basi please!, amka naogopa mimi, amka tukimbie mimi siwezi kukimbia na kukuacha mwenyewe hapa watakuua, amka please amkaaa..." Lakini Elvine hakuweza kuamka wala kumsikia. 

Elimina alisimama na kumtazama yule mtu aliyekuwa anakuja. Alipomtazama kwa makini akagundua kuwa ni Erika. Akaanza kulia tena.

"Kumbe ni wewe shetani, kaa mbali na mume wangu kaa mbali nasema!"

Erika hakuwa anasema kitu zaidi ya kutabasamu. Alipofika karibu zaidi akaanza kucheka.

" Yaani we ni mwigizaji hatari"

" Unamaana gani?

"Kwani wewe unafikiri  nina maana gani? Yaani, kama mwana wa miungu vile, unajua na kujua tena. Nimependa na nimejivunia sana wewe!"

Yule binti alimtazama Erika kisha akafuta machozi na kutabasamu na vicheko vikafatia.

" Unajua nini Erijini, Kuna muda Elvine anakera sana hadi natamani nimle hata nyama lakini sasa najikaza tuu!"

"Usijali part! Huyu mwisho wake unakaribia. Tatizo ni yule binti kule, anasumbua balaa halafu sahizi analindwa sana. Yaani inatakiwa mashambulizi makubwa yawe kule ili na sisi tuikamilishe hii sadaka yetu"

"Na ndio maana nachukia. Elimina anafanya mambo ya ajabu kweli. Elvine angetolewa sadaka usiku wa leo lakini angalia hasara iliyotokea!. Elimina kachoma nyumba yote kwaajili ya kumuokoa Elvine lakini bado tunaweza kumshinda maana Elvine yupo mikononi mwetu"

"Swala sio kuwa mikononi mwetu, tatizo hatuwezi kumdhuru Elvine tusipomdhibiti yule mwanamke kule. Erika sikia fanya unachojua kumteka Elvine akuamini kabisa ili hata vita yoyote ikitokea Elvine awe tayari kuwa upande wako. 

Halafu kuhusu yule mwanamke kule Duniani, mimi nitapambana nae na sasa hivi nipo tayari kuwatoa hata sadaka baadhi ya wanachama wetu ili kumdhoofisha Elimina. Kwa kuwa naweza kujigawa nitajaribu kufanya mambo yote mwenyewe au nitajua namna ya kugawa majukumu"

Wakati wanaendelea na mazungumzo yao Efraim alikuja naye akiwa anawaka mwili mzima kwa moto. Moto uliwafanya wao kuonana vizuri maana kulikuwa na giza sana. Alikuwa na hasira bado.

"We binti mdogo vipi mbona unajadili na nafsi yako badala ya kufanya kazi?" Aliongea na Elimina fake. 

"Baba!" Elimina alienda kumkumbatia Efraim na hapo hapo alibadilika na kuwa Erika yaani kukawa na Erika wawili. Yule aliyekuwa amekuja anawaka moto akaingia ndani ya Erika alijifanya Elimina na akawa mtu mmoja. 

" Unajua nini baba, najua hasara iliyotokea kwenye ufalme wetu leo, najua namna ambayo tumepoteza misukule na madawa wengi katika ufalme wetu, lakini usijali najua sio muda Elvine tutamnasa. Na kuhusu Elimina najua wewe humuwezi ila mimi nitajua cha kufanya. Sasa naomba usiwe na hasira maana nataka nikupe kazi hapa baba yangu kipenzi"

"Umeanza! Kazi gani hiyo?"

"Nataka unisaidie jambo!"

"Gani hilo? Si useme?"

"Nataka wewe uwe Elimina!"

"Ati nini? Yaani Mimi nijifanye Elimina?"

"Ndio! Lazima ufanye hivyo. Mimi nataka kuhamishia mashambulizi kwa Elimina kule, maana najua wewe humuwezi. Ulishafanya makosa toka mwanzo. Hawa wana wa kifalme Kwa upande wa Mungu wao yule anayejiita mwenye nguvu kuliko sisi, huwezi kumuangusha mtu wake pasipo kuwafarakanisha. 

Nataka nikamfanye Elimina amkosee Mungu ili nipate kumuangamiza na hapo ndipo tutamuweza Elvine. Hakikisha Elvine hakushitukii na kama akishituka basi jitahidi kumlainisha tena maana udhaifu wake upo kwa mkewe kwa sasa na pia anasahau kila baada ya dakika 10 kwahiyo ni rahisi sana kumraghai"

"Sawa lakini usichelewe kurudi, maana wewe mambo yako huwa yanachukua muda mrefu sana mpaka kukamilika"

“Baba nimeshakwambia, ufalme wa hawa wenzetu unanguvu kuliko sisi. Huoni mpaka sasa Elvine tunaye, lakini bado mtu mmoja tu huko duniani anasababisha tusikamilishe mambo yetu?. Hili swala linaniuma sana kuona tunafeli sana mbele ya hawa watu. Yaani mpaka kumpata Elimina sio kazi nyepesi maana analindwa mno na ufalme wake na anamsimamo sana yule mwanamke. 

Ila mimi nakuahidi baba naenda kumuangusha na akianguka, atalipia haya yote aliyoyafanya kwenye ufalme wa kiza nasema atalipia, tena naapa nitafanya ajute, na ajute tena labda asijichanganye" Erijini (Erika), aliongea kwa uchungu na hasira mpaka macho yakageuka rangi na kuwa rangi ya bluu....

Kusoma sehemu ya 24 bofya hapa.


Simulizi  hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            &, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.

Pamoja na SOPHIA FREDRICK. Mhariri.

Mawasliano. +255745675197

Tu follow kwenye.

Facebook page>>> Add Value Network.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.




Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.