MALENGO 6 YA ELIMU YANAYOWEZA KUBADILISHA MAISHA YAKO KABISA.
MALENGO 6 YA ELIMU YANAYOWEZA KUBADILISHA MAISHA YAKO KABISA. Watu wengi wanaposikia neno elimu, jambo la kwanza linalokuja akilini ni: shule, mitihani, vyeti, Pesa au ajira. Asilimia kubwa jamii yetu inaamini sana katika ajira, kwamba ukiwa msomi/ mwenye elimu huku hujaajiriwa unaonekana si lolote wala chochote. Lakini ukweli ni kwamba elimu ni kubwa zaidi ya hayo. Boss, elimu siyo tu kukariri taarifa darasani au kupata alama nzuri kwenye mtihani ndugu yangu. In short boss, Elimu si karatasi ya cheti tu, bali ni mchakato wa kumjenga mwanadamu kamili. Hapa namaanisha kuwa, Elimu ya kweli ni mchakato wa kumjenga mtu kiakili, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kimaadili ili aweze kuishi maisha yenye maana na mchango kwa jamii. Kwa kifupi boss, elimu inapaswa kumbadilisha mtu kutoka alivyo leo na kumpeleka katika kiwango bora zaidi cha maisha yake na yawatu wanaomzunguka. Kitu hiki ndo kimenisukuma leo tuangalie malengo makuu sita ya elimu kwa mtu husika boss. 1. KUKUZA AKIL...