KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA.
KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA.
Boss! Siyo kila mara, kusahau ni ishara ya Ubongo dhaifu, mara nyingi ni namna tunavyojifunza ndugu.
Nimekutana na watu wengi wakisema:
"Mimi sina akili kubwa." Wengine
"Kumbukumbu yangu ni mbaya." Mara
"Ubongo wangu hauhifadhi vitu."
Lakini ukweli ni kwamba, mara nyingi tatizo si ukubwa wa akili yako wala uwezo wa ubongo wako.
Tatizo ni kwamba watu wengi hawajawahi kufundishwa jinsi kumbukumbu (memory) inavyofanya kazi boss.
Sikia ndugu; Ubongo wa binadamu umeumbwa kwa ustadi mkubwa. Kazi yake si kuhifadhi kila kitu unachokiona au kukisikia, bali ni kuchagua filtering taarifa muhimu na kuacha zisizo muhimu wala matumizi.
Kwa hiyo, kusahau si kasoro ya ubongo ni sehemu ya kawaida ya jinsi unavyofanya kazi.
Hebu tuangalie sababu kuu zinazowafanya watu kusahau mara kwa mara.
1. Kukariri Bila Kuelewa (memorising without understanding).
Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo wanafunzi na hata watu wazima hulifanya.
Ubongo haupendi kukariri maneno yasiyo na maana au kurudia rudia maneno reptition. Unapenda kuelewa boss.
Unapoelewa jambo, ubongo hulihusisha na maarifa ambayo tayari unayo. Hii huunda connection zinazofanya taarifa ibaki kwa muda mrefu.
Lakini ukikariri tu bila kuelewa, taarifa hiyo hukaa juu juu bila link na kisha hupotea haraka sana.
Kuelewa hujenga kumbukumbu; kukariri pekee na reptition hujenga kusahau ndugu.
2. KUTOKUWA MAKINI (LACK OF ATTENTION).
Ndugu askudanganye mtu, kumbukumbu huanza na umakini
Kama hukuweka umakini wakati taarifa inaingia, ubongo hauna kitu wala sahemu ya kuhifadhia.
Unaweza kuwa darasani, kwenye mkutano au unasoma kitabu, lakini mawazo yako yako sehemu nyingine.
Mwili upo hapo, lakini akili haipo.
Katika hali hiyo, ubongo hauchakati taarifa ipasavyo, hivyo kusahau huwa rahisi sana mwanangu
3. KUTOTUMIA ULICHOJIFUNZA (YOU DON'T USE WHAT YOU LEARNT).
boss, Ubongo hupokea maelfu ya taarifa kila siku.
Ili usizidiwe na mzigo wa taarifa overload, ubongo hujiuliza swali moja muhimu:
"Je, taarifa hii ni muhimu na itahitajika tena?"
Kama jibu ni ndiyo, hujaribu kuihifadhi.
Kama jibu ni hapana, huanza kuifuta polepole.
Ndiyo maana ukijifunza jambo lakini usilitumie kwa muda mrefu, ubongo huliona halina umuhimu na kuliondoa kwenye kumbukumbu za muda mrefu.
Maarifa yanadumu kwa kuyatumia katika maisha ya kila siku.
4. MSONGO wa MAWAZO (STRESS).
Ubongo hufanya kazi vizuri unapokuwa katika hali ya utulivu.
Lakini unapokuwa na msongo wa mawazo, hofu au presha kubwa, uwezo wa ubongo wa kujifunza na kukumbuka hupungua sana.
Stress ni kama kelele nyingi ndani ya akili.
Badala ya kuzingatia taarifa mpya, ubongo hujikita katika kushughulikia hali ya tahadhari.
Ndiyo maana watu wengi husahau kirahisi wanapokuwa na mawazo mengi ndugu yangu.
5. KUTORUDIA ULICHOJIFUNZA (NOT REVISTING THE INFORMATION).
Kujifunza mara moja haitoshi boss,
Kila unapojikumbusha au kurudia ulichojifunza, unauambia ubongo:
"Taarifa hii ni muhimu. Hebu itunze."
Lakini ukiacha kuirudia au kuitumia, nguvu ya kumbukumbu hupungua hatua kwa hatua.
Hii ndiyo sababu ya umuhimu wa marudio (revision).
Marudio huimarisha njia za kumbukumbu ndani ya ubongo wako.
6. USINGIZI DUNI (POOR SLEEP).
Watu wengi hudharau usingizi.
Lakini usingizi ni sehemu muhimu ya kujifunza.
Wakati umelala, ubongo hupanga, hupanga upya na huhifadhi taarifa ulizokusanya siku nzima.
Ukikosa usingizi wa kutosha au usingizi bora, mchakato huu huvurugika.
Matokeo yake ni: kusahau kwa urahisi, kushindwa kuzingatia,
na uwezo mdogo wa kujifunza.
Usingizi si kupoteza muda ni uwekezaji na utendaji bora wa ubongo wako boss.
JINSI YA KUIMARISHA KUMBUKUMBU YAKO
Kama unataka kumbukumbu bora kwa kifupi fanya haya;
....... Elewa kabla ya kukariri. Understanding
......Weka umakini kamili unapojifunza. Attention.
...... Tumia maarifa unayojifunza katika maisha halisi. Use the information.
......Rudia na kujikumbusha mara kwa mara. Revist hata kwa muda mchache.
.....Punguza msongo wa mawazo. Stress less.
.... Lala usingizi wa kutosha kila siku. Have enough sleep boss.
Hatua hizi zinaweza kuboresha uwezo wako wa kukumbuka kwa kiwango kikubwa.
Kwa hiyo sasa boss, Usijihukumu au kujilaumu haraka kwamba huna akili au kumbukumbu nzuri.
Mara nyingi tatizo si uwezo wa ubongo wako bali namna ulivyofundißhwa na jinsi unavyoutumia.
Kwasababu ubongo ni kama misuli; unavyoendelea kuutumia kwa njia sahihi, ndivyo unavyozidi kuwa imara na sahihi zaidi.
Hata hivyo boss Ubongo hauhifadhi kila taarifa. Unahifadhi taarifa UNAZOZIELEWA, UNAZIZITUMIA, na unazoonyesha kuwa ni MUHIMU KUPITIA MARUDIO REPTITION.
Boss.
Ni sababu ipi kati ya hizi unadhani ndiyo inakufanya usahausahau mara nyingi?
#SeeYouNextLevel
Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.
#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork.
+255767653697.
