WATU WENYE HESHIMA YA KWELI HUFANYA MAMBO HAYA 10.
WATU WENYE HESHIMA YA KWELI HUFANYA MAMBO HAYA 10.
Mara nyingi watu hupima mafanikio kwa fedha, elimu, cheo au umaarufu. Lakini ukweli ni kwamba, mojawapo ya vitu vinavyomtofautisha mtu mwenye busara na mwenye hekima ni namna anavyowatendea watu wengine boss.
Kwasababu tabia nzuri hazihitaji utajiri. Hazihitaji cheti. Hazihitaji nafasi kubwa katika jamii. Zinahitaji ufahamu, heshima, nidhamu na utu boss.
Haya ni baadhi ya mambo madogo ambayo yanaweza kujenga au kuharibu taswira yako mbele ya watu. Yaani, mambo madogo yanayofichua ukomavu wako kwa watu na jamii.
11. MSIFIE MTU HADHARANI, MPINGE FARAGHANI.
Ukiona mtu amefanya jambo zuri, msifie mbele ya watu moja kwa moja hata kama akiwa pekee yake siyo mbaya.
Lakini unapohitaji kurekebisha kosa lake, fanya hivyo faraghani.
Kumkosoa mtu hadharani mara nyingi huumiza heshima yake, humpa aibu na kumfanya awe na msimamo wa kujitetea badala ya kujifunza.
Watu wengi husahau maneno uliyosema, lakini hawasahau aibu na jinsi ulivyowafanya wajisikie.
12. USIKOSOE MUONEKANO WA MTU.
Unapokutana na mtu si lazima useme:
"Mbona umenenepa sana?", "Mbona umekonda sana?", "Mbona umezeeka hivyo?"
Hayo mara nyingi si maoni ya kujenga bali ni kama sindano ya kuchoma kimyakimya.
Badala yake sema: "Umependeza.", "Nimefurahi kukuona." Lakini usifanye kwa unafiki boss. Tell the fact.
Kama kuna jambo anataka kukueleza kuhusu hali yake, atakueleza yeye mwenyewe ndipo utakapotoa comment boss.
13. UKIONYESHWA PICHA KWENYE SIMU USICHUNGUZE PICHA NYINGINE.
Mtu anapokuonyesha picha moja kwenye simu yake, heshimu mipaka yake.
Usianze kusogeza picha kushoto au kulia bila ruhusa.
Huenda kuna vitu binafsi ambavyo hakukusudia kuvionyesha.
Heshima ya faragha hujengwa kwenye mambo madogo kama haya boss.
Si unawafahamu wale watu ukimpa simu aone picha fulani utashangaa ashaenda kwenye video mara kwenye message, kila kona an.
14. USILAZIMISHE KUJUA SABABU YA MTU KWENDA HOSPITALI.
Mtu akikuambia: "Ninaenda hospitali."
Huna ulazima wa kumuuliza maswali kama: "Unaumwa nini?", "Tatizo ni nini?"
Kama ataona inafaa kukuambia, atafanya hivyo mwenyewe.
Wakati mwingine mtu anahitaji dua, si mahojiano boss.
15. MHESHIMU KILA MTU BILA KUJALI KAZI, JINSI, UMRI, KABILA AU ELIMU YAKE.
Mheshimu: mfagizi, mlinzi, dereva, mhudumu, na bosi bila tabaka.
Kwa sababu thamani ya mtu haipimwi kwa cheo chake.
Heshima ya kweli huonekana pale unapowatendea vizuri watu ambao huwezi kunufaika nao moja kwa moja boss.
Tatizo letu waafrika tunaangalia vitu badala ya utu.
16. ONGEA NA MTU UKIMPA UMAKINI WOTE.
Hakuna kitu kinachoonyesha kutomheshimu mtu kama kuzungumza naye huku:
ukitazama simu, ukitazama televisheni au ukitazama kila upande isipokuwa yeye.
Mtu anapozungumza na wewe, mpe umakini wako wote.
Mwangalie machoni. Msikilize. Yaani, Onyesha kuwa unathamini uwepo wake.
17. USITOE USHAURI KAMA HUJAOMBWA.
Watu wengi hupenda kusuluhisha matatizo ya wengine kabla hata hawajaombwa.
Lakini nimekuja gundua kuwa, si kila anayesimulia changamoto zake anahitaji ushauri boss.
Wakati mwingine anahitaji: kusikilizwa,
kueleweka, kupewa faraja. Pole au nafasi ya kufikiri tu boss.
Hata hivyo boss hekima si kusema kila unachojua, bali kujua wakati sahihi wa kusema.
18. USIULIZE UMRI AU KIPATO CHA MTU BILA SABABU.
Maswali kama: "Una miaka mingapi?"
"Unalipwa shilingi ngapi kwa mwezi?"
"Biashara yako inaingiza kiasi gani?"
Maswali haya mara nyingi huingia kwenye eneo la faragha.
Kama mtu anataka kushiriki taarifa hizo, atafanya hivyo kwa hiari yake mwenyewe.
Heshima hujumuisha kuheshimu mipaka ya wengine boss.
19. VUA MIWANI YA JUA/UREMBO UNAPOONGEA NA MTU.
Macho ni sehemu muhimu ya mawasiliano.
Unapozungumza na mtu huku umevaa miwani ya jua: mawasiliano hupungua, connection hupungua, na wakati mwingine huonekana kama hauko makini.
Kama mazingira yanaruhusu, vua miwani yako na zungumza kwa uwazi boss.
20. KUWA MWANGALIFU NA MAMBO UNAYOJISIFIA.
Usizungumzie: utajiri wako kwa watu wanaopitia changamoto za kifedha,
mafanikio yako kwa lengo la kuwafanya wengine wajione duni,
au watoto wako kwa namna inayoweza kuwaumiza watu ambao hawajajaliwa kupata watoto boss.
Kuwa na huruma na ufahamu wa hali za wengine ndugu.
Kile ambacho ni furaha kwako kinaweza kuwa ni maombi, hitaji au maumivu kwa mtu mwingine boss.
Nimalize kusema, ustaarabu si kuvaa vizuri tu.
Ni: kuheshimu mipaka ya watu, kuwasikiliza kwa makini, kuwa na huruma, kuwasaidia wengine na kujua namna ya kuishi vizuri na wengine.
Mara nyingi watu hawatakukumbuka kwa pesa ulizokuwa nazo wala cheo chako.
Lakini watakumbuka:ulivyowafanya wajisikie walipokuwa karibu nawe boss.
Je, kati ya tabia hizi 10 ni ipi unaona watu wengi huipuuzia katika jamii yetu leo?
Andika sababu hapa chini.
#SeeYouNextLevel
Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.
Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026/06/malengo-6-ya-elimu-yanayoweza.html
#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork.
+255767653697.
