MAAJABU YA AKIBA

Mtu mmoja alisikika akisema
nimekusamehe lakini sitakusahau katika maisha yangu kwa hichi ulicho nitendea!
Kama utakuwa mfuatariaji na
mdadsi wa mambo na watu utagundua kuwa suala la kusamehe limekuwa ni changamoto
kubwa sana kwa watu wengi. Wengi wamebaki na vinyongo, visasi, machungu, na hasira
kupita kiasi kuhusu ulio wakosea au
kutokuwasamehe.
Mwalimu
mmoja aliwaagiza wanafunzi wake kila mmoja aje na nyanya kulingana na idadi ya watu anaowachukia. Wanafunzi walikuja nazo siku iliyofuata, wengine walikuja na nyanya moja, wengine mbili, wengine tano, na wengine nyanya za kutosha na walipo kuja nazo
aliwaambia waandike majina ya watu wanaowachukia ko, waziache kwenye mikoba yao na
mwalimu aliwaambia watakuwa wanakuja nazo kila siku bila kuzitupa au kuziacha. Baada ya siku kadhaa wanafunzi walianza kulalamika kuwa mzigo umekuwa mzito na
umekuwa ni ngumu kuja nao kwani zilikuwa zimeshaanza kuoza na kunuka
hivyo yalikuwa yanaharibu daftari zao na walimwomba sana mwalimu wao awaambie
wayatupe ili kuepuka kuchafuka na kuharibu daftari zao halafu kwanza mzigo ulikuwa ni mzito hasa kwa wale waliokuja na nyanya nyingi.
Hivyo ndivyo ilivyo hata
katika maisha ya kawaida kumchukia mtu
ni kujibebesha mzigo mzito sana ambao hata wewe mwenyewe kuubeba ni taabu sana. Na kushindwa kusamehe ni sawa na kunywa
sumu wewe ili afe mtu mwingine. Hiki kitu hakiwezekani. Linapokuja suala
la kusamehe tunasamehe kwa faida yetu wenyewe hata kama waliotukosea ni wao.
Tatizo kubwa la watu hasa
linapokuja suala la kusamehe, wengi wanashindwa kufanya hivyo kwasababu wanajua
kuwa watawanufaisha wengine na matokeo yake wana baki na vinyongo, hasira, na
chuki ya kudumu mioyo mwao. Ndugu yangu, hapa ni sawa na kunywa sumu ili afe unayemchukia, katika hili utasubiri sana, hasa ukikutana mtu kama mimi ambaye
huwa sijali unisamehe au usinisamehe ni sawa tu, lakini ni lazima nije kukuomba
msamaha kiroho safi kabisa sasa suala la kusamehe ni lako juu yako mwenyewe.
Kusamehe
ni kujipenda mwenyewe . Haijarishi mtu amekutenda makubwa
kiasi gani jukumu la kuomba msamaha ni lake ndiyo lakini, wajibu wako wewe ni kusamehe. Ndiyo maana hata
maandiko yanasema samehe saba mara sabini, hiki ni kiwango kikubwa saba cha
kusamehe lakini maana yake ni kwamba tunalo jukumu la kusamehe kila tunapo
hitajika kufanya hivyo. Pamoja na kusamehe pia tunatakiwa kuomba msamaha kwa
kila tunapokosea au kwenda kinyume. Samahani ni neno dogo sana lakini matokeo yake
ni makubwa sana. Kipindi tunasoma hiki kitu tulikiita msuli sisimizi matokeo
tembo yaani unasoma kidogo tu unafauli sana kama vile jiniazi ani.
Ukishindwa
kusamehe unajizibia Baraka na utashindwa kufungua ukurasa mpya. Ili kuanza upya unahitaji kuachilia maumivu vinyongo na hasira hapo ndipo
utaanza ukurasa mpya. Sasa swali la kujiuliza utawezaje kuanza ukurasa mpya hali
ya kwamba bado umeng’ang’ania ukurasa wa zamani hiki kitu ni ngumu kutokea.
Mwandishi mmoja alisema when we begin to release the negative
emotional we begin to release pains. Yaani, tunapoanza kuachilia mawazo hasi
tunaanza kuachilia maumivu.
Joel nanauka anasema “Unaposamehe
haimaanishi kuwa unakubaliana na makosa uliyofanyiwa ila inamaanisha unajua
umuhimu wa kuanza upya na kusonga mbele kwenye maisha yako”.
Usiposamehe
hutauona ufalme wa Mungu. Watu wengi tunasubiria kuuona ufalme wa Mungu
kwa namna yoyote ile hata kwa kuchelewa sana ilimradi tu! tufike lakini ukweli
ni kwamba tabia ya kusamehe ni ya Mungu mwenyewe na Mtu asipo samehe hatauona ufalme
wa Mungu soma utusamehe deni zetu kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu (mathayo
6:12).
Rafiki yangu kusamehe
ni kwa faida yako. William Shakespeare alisema, “Tusitwishe mzigo mzito
kumbukumbu zetu kwa jambo zito ambalo limepita”. Jambo likisha fanyika huwezi
kulibadilisha kwa kubadilisha matokeo yake badala yake ni kujipanga umpya kwa
kugundua ni wapi umekosea na kisha kurekebisha.
Oprah Winfrey, aliposema: “Learn to Forgive and Let it go” (Jifunze kusamehe na kuachilia).
Pamoja na kuwepo kwa maumivu makali sana ya kuwasamehe watu lakini pia suluhisho kubwa katika hili ni kusamehe na kuachilia hii ni njia moja ya kupatau ponyaji wa kudumu ili usonge mbele.
Unaposamehe
haimaanishi kuwa unakubaliana na makosa uliyofanyiwa ila inamaanisha unajua
umuhimu wa kuanza upya na kusonga mbele kwenye maisha yako.
Jaribu Leo kukumbuka kila mtu ambaye unajua hujamsamehe na umekuwa na kila sababu ya kutokumsamehe. Tangaza msamaha katika moyo wako, kisha tangaza msamaha kwa kusema pia kwa kumtaja jina: “ fulani, nimekusamehe.”.
Nipende kukujuza kuwa
unaposamehe haimanishi kuwa hautasahau, hapana kusamehe unasamehe kwa moyo wote
sema tukio hilo litabaki kama kumbu kumbu kama yalivyo matukio mengine ya
kufurahisha au kuhuzunisha hatujayasahau hadi leo na hii haimaanishi kuwa
hatuja samehe ,tunasamehe lakini ubongo sababu kazi yake ni kutunza kumbukumbu basi tukio hilo ni ngumu kufutika hivyo kukumbuka tukio husika hakuhusiani
kabisa na kusamehe .
Tambua kuwa
watu dhaifu hawawezi kusamehe, kusamehe ni ishara ya ujasiri, na wewe ni mtu
jasiri.
samehe kwa faida yako.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala
hii imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri &Mwalimu Wa
Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa
mtandao wa addvaluetz karibu sana ujiongezee thamani yako.
Sim
na Whatsapp >>+255783327456 / +255767653697.
Email>>
eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>>
MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama
umejifunza kitu,niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Jacob · 104 weeks ago
Migongo · 104 weeks ago
Mhitaji · 94 weeks ago
Elias Migongo · 94 weeks ago
Nesta · 94 weeks ago
God bless you Migongo Elias, Na Mungu aendelee kukutumia zaid na zaid.
Elias Migongo · 94 weeks ago