MAAJABU YA AKIBA

Hivi ulisha wahi kwenda hospitali na kupata ushauri wa daktari juu ya afya ya mwili wako? Au basi ulisha wahi kumsikia mtu yeyoye pengine rafiki, ndugu, mke, kaka yako au mtu yeyote akisimulia kuhusu ushauri wa daktari katika kutunza na kuimarisha afya ya mwili wake?
Bila shaka ulisha wahi na kama bado usihamaki, kwani utaelewa tu.
Ukweli ni kwamba mara nyingi watu wamekuwa na utaratibu wa kwenda hospitali kwaajili ya afya za miili yao na hapo watapewa dawa za kutosha, ili kujiponya na malazi yanayo wasibu.
Na mara nyingi hupewa dawa za kutumia, wengine huchomwa sindano, wengine kupewa masharti ya namna ya
kutumia dawa hizo wengine huambiwa kula baadhi ya vyakula wengine mazoezi n.k
Kwa kawaida mwanadamu ameundwa na sehemu kuu mbili, nazo ni utu wa nje na utu wa ndani.
Utu wa nje ndio huu mwili ambao unashikika yaani, huu mwili wa damu na nyama.
Ili kuuimarisha mwili huu wanadamu wamekuwa wakifanya vitu kama mazoezi, kula vizuri na vitu vinavyofanana na hivyo.
Sasa kama ilivyo katika utu wa nje ambao umeundwa na damu, nyama, mifupa na misuli, ndivyo ulivyo na utu wa ndani huu unaundwa na akili (mind) ambao kiungo chake muhimu ni UBONGO.
Hii ni sehemu muhimu sana katika mwili wa mwanadamu kadharika nayo inahitaji kuwepewa lishe bora , kufanyishwa mazoezi yaimarishayo na kuoshwa kwa maji safi na salama.
Pia nichukue nafasi hii kukujuza kuwa mwanadamu yeyote anahitaji kuwa na aina kuu tatu za afya nazo ni afya ya akili, afya ya mwili na afya ya Roho yake mwenyewe.
Leo tutazungumzia sana afya ya akili ambayo ni muhimu sana
mtu kuwa nayo katika kutimiza malengo na kufikia ndoto yake. Kwa kuwa afya hii
ya akili imebebwa na inategemea sana kiungo ubongo tutakwenda kuzungumza njia
mbalimbali ambazo mtu anaweza kuzitumia ilikuosha akili iliyo ndani ya ubongo
wake yaani, namna gani utaweza kuusafisha
ubongo wako kama kiungo kibeba akili yako.
Ili ubongo na akili yako viweze kufanya kazi ipasavyo vinahitajika kusafishwa na kuoshwa kwa njia mbalimbali.
Hivyo zifuatavyo ni njia lukuki zitakazo kusaidia ili kuiosha akili yako nazo ni;
1. KULA CHAKULA NA LISHE BORA;
Kama ilivyo kwa mwili unahitaji sana rishe bora ili kuuimarisha, kadharika akili inahitaji rishe na chakula bora kuiimarisha.
Kwani, kuna vyakula vingi sana vimeripotiwa kutibu magonjwa ya akili na kuongeza utendaji kazi wa akili katika ubora wake.
Vyakula kama matunda, mbogamboga, carbohaydrate na vyakula vingine. Kama vikiliwa kwa utaratibu husaidia sana kuimarisha afya ya mwili ambayo inamahusiano ya moja kwa moja na afya ya akili pengine baadhi ya vyakula vina matokeo ya moja kwa moja katika akili kwa kuimarisha misuli ya ubongo ambao ndiyo nyumba ya akili.
2.
KUJIFUNZA
VITU VIPYA.
Kadiri mtu anvyo jifunza vitu vipya kila siku na kila wakati, ubongo wake unazalisha hormone kama vile endorphins na dopamine ambazo husaidia sana katika uzalisha na kuchochea furaha katika mwili wake ambayo husaidia kuondoa mawazo na msongo wa mawazo katika maisha yake.
Kadri uanavyokuwa na furaha ndivyo ambavyo ubongo wako unakuwa huru katika kufanya kazi.
Kwa hiyo kadiri unavyojifunza au kufanya vitu vipya na kuvifanikisha ubongo wako unakuwa katika hatua nzuri sana ya kusonga mbele na kuwa na afya njema.
Hivyo ndugu kuwa na utamaduni wa kujifunza kitu kipya kila siku.
Fanya hivi kwa kuuliza
watu,kusoma mtandaoni,kusoma vitabu, kutembea, kusikiliza muziki, kuhudhuria
semina na kuyafanyia kazi yale utakayojifunza, matokeo utayapata mwenyewe.
Kutafakari ni kufikiri kwa utulivu na umakini kuhusu jambo fulani hasa unapo lenga kujifunza zaidi au kupata suluhisho juu ya changamoto inayo kuhusu .
Wagojwa wengi sana marekani wameripotiwa kutibiwa kutokana na kutafakari kwa umakini na kwa kiina.njia hii huipa majukumu ubongo ya moja kwa moja katika kulijua na kulitatua tatizo husika .
Kwa hiyo tafuta sehemu tulivu ili kuzungumza na akili yako na utashangaa utakavyoona unapata mawazo makubwa na suruhu bora kuwahi kutokea.
kwani kwa kawaida katika kila dakika mwanadamu kuna zaidi ya maelfu ya mawazo ambayo humujia.Na njia rahisi ya kuya faidi ni kupitia kutafakari .
Fanya kutafakari kuwa ni utaratibu wako kila siku kwa kutafuta sehemu tulivu au fanya hivyo usiku wakati wengine wamelala kama matajiri na mabilionea wafanyavyo hapa dunia.
4.
MICHEZO
NA MAZOEZI YA VIONGO.
Nji mwili wako unavyopata mazoezi ya viungo ndivyo unavyozidi kutanua na kuimarisha misuri yake. hii inafanya mtu kuwa na furaha muda mwingi.
Kama afya yako ya mwili ikiimarika hata misuli ya ubongo nayo huimalika. Na swala linguine hapa ni michezo.
Michezo ya pamoja kama mpira
kuimba kuigiza, kucheza magemu huchangia sana kuifanyisha mazoezi akili yako.
Hivyo ndugu chagua kuimalisha afya yako ya ubongo kwa kufanya mazoezi walau mara 4 kwa wiki itakusaidia sana kwani mazoezi huimaliza misuli na kuondoa uzembe usio wa lazima .
Asilimia kubwa ya wakurugenzi mahili duniani hufanya michezo na mazoezi ya viungo wanajua siri hii fanya hivyo na wewe leo.
5.
KUTATUA
MATATIZO NA KUFANYA MAZOEZI YA UBONGO.
Mtoto mmoja alikuwa akipewa kazi ngumu na kuwafanyia maswali magumu ya home work watoto wenzake alikuwa akifanyiwa hivyo na mama wa kambo na lengo kubwa ilikuwa ni kumkomoa.
Lakini kadri muda ulivyozidi kusonga ndivyo alivyokuwa na uwezo mkubwa sana wa kukabiliana na matatizo na changamoto za maisha na watoto wengine waliokuwa wanadekezwa walikuwa na uwezo mdogo sana wa akili.
Hii itoshe tu kusema kadri unavyo tatua changamoto kubwa na nyingi kwenye maisha yako ndivyo unavyo ongeza uwezo wako wa kufikiri .
Na kitu kingine katika hili ni kufanya mazoezi ya akili na ubongo , ubongo wako unaweza ukaufanyisha mazoezi kama vile kuvuta kumbu kumbu ya matukio ya nyuma na majina ya watu, kucheza magemu magumu, kutafakari na kujifunza lugha mpya hii itakusaidia sana.
6.
KUULIZA
MASWALI NA KUWA MDADSI
Uchunguzi ulifanyika na kuonyesha kuwa watu wenye akili na ubongo makini wanatabia zinazofanana kabisa, ile tabia ya kuwa wachunguzi wa mambo na wanasifa ya kuuliza maswali sana.
kitu hiki kimedhibitishwa kuwa ni moja ya njia ya kujifunza vitu vipya kutoka kwa watu na mazingira mbalimbali ambapo hali hii humfanya mtu kuongeza uwezo wa akili yake kuweza kufanya kazi vizuri.
Hivyo ndugu yangu kama unataka na wewe
kula meza moja na watu wanao upiga mwingi katika maswala haya jifunze kuwa
mdadsi, uliza maswali itakusaidia kuwa na taarifa nyingi na kufahamu vitu vingi
vitakavyo kufanya kuwa mtu muhimu sana kwa dunia ya leo si unajua dunila ya
sasa ni dunia ya taarifa, ujuzi na maarifa neeh!
7.
SOMA
VITABU NA MAKALA MBALI MBALI.
Kipengele hiki kwa kawaida kilitakiwa kiwe katika ile point ya kujifunza ,lakini kutokana na umuhimu na uzito wake wacha tuipe mji ijitegemee.
Rafiki njia rahisi ya kujifunza kwa makosa ya watu walio tutangulia ni kusoma vitabu. kurudia makosa ambayo watu wengi huko nyuma waliyafanya huku ungeweza kuyaepuka kwa kusoma vitabu huu ni ujinga.
kama tunavyojua kuwa chanzo kikubwa cha taarifa na maarifa ni kwenye maandishi ingawa vipo vyanzo vingi lakini hii imeshika hatamu kutoka enzi na enzi.
kusoma vitabu kutakuongezea wingi wa maarifa, utajifunza vitu vipya vingi, utatatua matatizo yako, utakula meza moja na wasomi, wanasheria, waalimu, wajasiliamali, wandishi na watu mashuhuri waliopita.
Hii nayo itakupa furaha na kukupunguzia msongo wa mawazo kwa kuwa msongo wa mawazo una athari kubwa sana katika akili na ubongo wa mwanadamu.
Na isitoshe tabia hii inapunguza msongo wa,mawazo kwa 68%. Nikushauri tu rafiki jenga tabia ya kusoma vitabu hautakuja kujuta kamwe watu wengi walioshindikana wameripoti kubadilishwa kabisa kupitia kusoma vitabu.
Ifanye kuwa ni tabia ya pili ya maisha yako na kama unachangamoto katika hili naomba wasiliana na mimi moja kwa moja naamini utasaidika.
Ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu rafiki!
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi, maendeleo binafsi na Maisha.
Mwanzilishi na Mwendeshaji wa mtandao wa addvaluenetwork.
karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa
mawasiliano;
Sim
na Whatsapp >>+255783327456 / +255767653697.
Email>>
eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS|| Add Value Network.
Kama
umejifunza kitu,niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Jacob · 103 weeks ago
Migongo · 103 weeks ago
mosest Amrani · 47 weeks ago