HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26. Ilipoishia.......... Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti... Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa. Sasa inaendelea......, Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda

SABABU ZA KUWEPO KWA MASIKINI WENGI KULIKO MATAJIRI;

TAMBUA KUWA;

Watu wengi sana wana malengo na wanatamani kuwa na mafanikio makubwa sana kuwahi kutokea hapa duniani yaani ukimuuliza mtu yeyote hata mtoto atakwambia ana ndoto ya kuwa dokta,mwalimu,nesi n.k wengine ma bilionea,  yani kiufupi hakuna asiyependa kufanikiwa sijaona kwakweli. Ingawa watu wote hutamani mafanikio makubwa sana swali moja limekuwa likinitesa na nimekuwa nikijiuliza kuwa kwanini kuna masikini wa kutosha kuliko hata matajiri na watu maarufu hapa dunian?.

swali Hili ndilo ambalo limenifanya niandike Makala hii .na Makala hii itakwenda kulijibu swali hili vizuri kabisa  hivyo kaa kwa kutulia nikupatie madude.

SABABU ZA KUWEPO KWA MASIKINI WENGI KULIKO MATAJIRI;

Rafiki zipo sababu kede wa kede zinazo watofautisha masikini na matajiri hapa duniani lakin utofauti wao mkubwa unakuja kwenye tabia zao ndiyo maana Mwandishi wa vitabu, mkufunzi wa mambo ya Uongozi na mfanyabishara, Mike Murdock aliwahi kusema “Siri ya mafanikio yako imefichwa katika tabia zako za kila siku”.

Lakini kwa leo hili halituhusu sana goja nikupe sababu kazaa ambazo huwafanya watu wengi kuwa masikini ingawa wana malengo kama yote;

1. HAWATAKI KUWAJIBIKA JUU YA MAISHA YAO

Hii ni changamoto kubwa sana kwa wengi kwani utakuta mtu anatamani kuwa mwandishi mbobevu kabisa, mwanasheria, mc,mwanasiasa,mwanahamasa,mneni,mwalimu,mwimbaji n.k lakini bado ametulia tu na hana mpango wala mkakati wowote wa kuanza kufanyia kazi kwa kile ana kitamani .watu wa hivi utawakuta wamekaa na kusubilia kuwa kuna siku tu mambo yatabadilika yenyewe yenyewe, wengine hutarajia kuwa kuna watu watakuja kutoka sehemu Fulani kuja kuwafanyia na kuwapeleka sehemu wanako hitaji .

Rafiki yangu nataka nikuambie kitu kimoja kuwa maisha yako ni wajibu wako mwenyewe kabisa kwa 100%.Na nikuhakikishie kabisa kuwa hakuna mtu hata mmoja atakae toka kokote kwaajili ya kuja kukutimizia malengo na ndoto ambazo umejiwekea hivyo kukaa huku ukitegemea na kusubilia watu wengine waje kukufanyia ni kujichelewesha mwenyewe  amka mzee.

Mara nyingi umekuwa ukituambia utakuja kuwa mtu mkubwa.mfanya biashara mkubwa ,mwanamuziki,mwimbaji n.k swali ni je utafanya lini? .fanya sasa na maisha yako ni wajibu wako 100% .

2.HAWAKO TAYARI KULIPA GHARAMA .

Moja ya kitu muhimu ambacho watu wengine hawaelewi kuhusu mafanikio ya watu maarufu na matajiri ambao wanawatamani na kitu hiki ni ulipaji wa gharama hiki ni kipengele muhimu sana kuhusu watu walio fanikiwa kwani wengi wanajua tu kuwa wao hao wamefika tu hapo walipo kama  bahati nasibu vile na bila kulipa gharama yeyote na wengine wakijua kuwa siku moja walilala wakaamka matajiri tayari .nataka nikuambie kua zipo gharama lukuki zilizojificha nyuma ya pazia la mafanikio ambazo wengi hawako tayari hata kuzisikia wala kuzifahamu. Gharama zenyewe ni pamoja na gharama ya muda,gharama ya fedha,gharama ya kujifunza,gharama ya kutumia akili  n.k gharama hizi Godius Rweyongeza  amezitaja katika kitabu chake cha jinsi ya kufikia ndoto yako.

Ukweli ni kwamba kama hautakuwa tayai kuzilipa gharama hizi kwako mafanikio na utajiri utaishia kuusikia tu. Godius Rweyongeza   anasema ‘mahali pekee ambapo unaweza kula kabla ya kulipia ni mugahawani’.

3. HAWANA UTHUBUTU WA KUANZA KUCHUKUA HATUA. 

Wakati mwingine kwa baadhi ya watu si kwamba hawana malengo,mikakati wala si kwamba hawajui ni gharama zipi wanapaswa kuzilipa ili kufika wanakotamania bali wanakuwa na woga katika kuanza kuchukua hatua za kufanyia kazi na kutekeleza malengo yao .Rafiki pengine unayo mipango na matamanio makubwa sana lakini kuna vitu vimekuwa vikikukwamisha hivyo jua ya kuwa wakati ndio huu sasa yaani anza sasa. isiwe kama yule mr perfectionist ambaye yeye anasubili awe na kila kitu ndiyo aanze anza na kidogo ulicho nacho kutafuta kikubwa unacho kitaka au tumia nguvu ya mlimbikizano  “COMPOUND EFFECT” itakusaidia sana.

Kwa uchache hizi ndizo baadhi ya sababu ambazo watu wengi zimekuwa zikiwa rudisha nyuma na kubaki na ndoto,malengo na mipango mingi sana pasipo na utekelezaji.zifahamu njia hizi kwa undani kisha uziepuke ili usiwe mmoja wao wa wasio timiza ndoto na malengo yao.

Naamini umejifunz kitu na mungu akubariki sana.

Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mwalimu Wa Saikolojia,Uchumi na Maisha.  Mwanzilishi na Mwendeshaji wa   mtandao wa https://addvaluetz. blogspot. com  karibu sana ujiongezee thamani yako. 

Kwa mawasiliano;

Sim na Whatsapp >>+255783327456 ||  +255767653697.

Email>> eliasmigongo120@gmail.com.

Facebook>> MIGONGO ELIAS

LinkedIn>>Migongoe. 

Kama umejifunza kitu,niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe. 

Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.