MAAJABU YA AKIBA

Kabla ya kwenda mbali Zaidi ni
muhimu tujue maana ya maneno haya mawili nayo ni Mkopo na Deni. Mkopo ni aina ya fedha
ambayo mtu au taasisi inachukua kutoka kwenye
chanzo kingine cha fedha kwa masharti fulani ya kurudisha fedha hizo kwa muda
fulani na kwa kiwango cha riba. Mkopo unaweza kutolewa na benki au taasisi
nyingine za kifedha, serikali, au hata mtu binafsi. Sasa pale mtu anaposhindwa
kutimiza masharti na makubaliano ya mkopo huo. Hapo ndipo inageuka na kuwa
deni na kwa wingi ni madeni. Madeni si
mabaya sana, kama yatakuwa yamefanyika kwa utaratibu maalum wa lengo la
kuongeza thamani yake kila baada ya muda fulani. Lakini, kama si hivyo yatakuwa
ni mabaya sana kuwahi kutokea.
Pamoja na hayo zipo sababu
nyingi sana zinazowapelekea watu wengi kuingia kwenye madeni yasiyoisha na
mbaya zaidi wamefanya kila linalowezekana ili kuondokana na madeni hayo lakini
imekuwa changamoto isiyoisha kwao. Hili nalo bado ni tatizo kubwa sana. Leo
nataka nikushirikishe sababu ambazo watu wengi zimewapelekea kuingia kwenye
madeni yasiyo isha. Na sababu hizi, zimezungumzwa na waandishi mbali mbali ndani na
nje ya nchi akiwemo Joel nanauka kwenye kitabu chake cha jinsi ya kuondokana na madeni. na wengine wengi hivyo soma hadi mwisho naimani utasaidika sana.
SABABU ZINAZO SABABISHA WATU KUINGIA KWENYE MADENI YASIYO KOMA.
1.
KUISHI
JUU YA KIPATO CHAKO.
Kwa kawaida kadiri unavyoongeza kipato ndivyo na matumizi yako
yanazidi kuongezeka zaidi. Angalia tu hata katika maisha ya watu waliokuwa na
kipato cha kawaida walikuwa na matumizi na wailiishi maisha ya kawaida sana, Lakini, kadiri
vipato na pesa zao zinavyozidi kuongezeka na matumizi yao yanazidi kuongezeka pia. Hiki
kitu ndicho alichokizungumzia bwana parkson mtaalamu wa masuala ya fedha. Watu
wengi wamekuwa wakiishi katika kundi hili, yaani pesa kidogo tu ashabadilisha
kila kitu anabadili mighahawa ya kula ,anasomesha shule za gharama kuliko uwezo
wake ,anaanza kujionyesha kuwa tayari yeye kashafanikiwa, anatumia na kuishi
maisha ya juu sana kwa kuwaonyesha watu kuwa ashafanikiwa tayari, hali hii ni
mbaya na imesababisha watu wengi kuingia kwenye madeni yasiyoisha .
Ndugu yangu usipende kujipandisha hadhi na kuishi juu ya
uwezo wako. Hivyo, Inakupasa uishi chini ya kipato chako pia ishi maisha kulingana
na hali yako ya sasa. kwani maisha unayo yatamani na kuyaigilizia utayafikia tu
kama utafanya kazi kwa bidii na ubora.
2. KUZOEA MADENI.
Kuna watu wameyazoea madeni
na kuyafanya kuwa ni sehemu ya maisha yao. Utakuta mtu kila kitu yeye ni kukopa
tu. Hela ya kalo ana kopa , chakula anakopa, bili za maji, umeme anakopa hela
ya nguo anakopa yaani, ameshakuwa mtu wa kuhamisha deni kutoka kwa mtu huyu na
kwenda kwa mdeni mpya. Na wengine wana misemo yao kabisa wakisema “hata mabilionea
wenyewe wana kopa” mwingine utakuta anasema kama nchi inadaiwa trioni kadhaa
mimi ni nani nisikope ?? Rafiki mikopo siyo mibaya tatizo ni kwamba, unakopa
kwaajili ya nini? Kama mkopo wako haukuzalishii pesa au faida yeyote labda ni
kwaajili ya matumizi ya kawaida tu mfano kulipa ada,kodi madeni n.k hapo
jiandae kuingia kwenye dimbwi kubwa la madeni.
3.
ULEVI
WA POMBE.
Tunawafahamu watu wengi kwenye mazingira yetu ambao wao pombe imekuwa kisukumo kikubwa Cha kuingia kwenye madeni lukuki. Tafiti zinaonyesha kuwa watu wengi wanaojihusisha na ulevyi
wa pombe imekuwa ngumu sana kwao kuendelea katika maendeleo yeyote yale
hii ni kwasababu pombe inaathiri ubongo
wa binadamu moja kwa moja, ndiyo maana walevi wengi hupoteza uwezo wao wa kumbu
kumbu, uwezo wa kufikiri , uwezo wa kupanga mipango ya maendeleo na mafanikio yao, yaani
anakuwa anawaza pombe tu anakuwa katika URAIBU, Hapo anaweza kukopa kwaajili ya
pombe anaweza kuuza mali na vitu vyake vya thamani kwaajili ya pombe hali hii
ni mbaya sana na mtu wa namna hii inampasa abadilishe sehemu za kutembelea na
marafiki wa kuambatana nao na kama tatizo litakuwa kubwa sana watafute
wataalamu wa saikolojia au wasiliana nami
moja kwa moja kwa mawasiliano hapo chini kwa msaada zaidi.
4.
KUSHINDWA
KUSEMA HAPANA.
Steve jobs mkurugenzi na mwanzilishi wa kampuni ya APPLE
aliulizwa nini maana ya focus alijibu na kusema “focus ni uwezo wa kusema
hapana kwa mambo ambayo yapo nje na malengo yako”.
Watu wengi sana wemeingia kwenye madeni ya kuwatosha kwasababu tu ya kushindwa kusema hapa. Wengine wamelazimishwa hata kununua vitu ambavyo hawakuvihitaji wala havikuwa kwenye malengo yao kwa kushindwa tu kusema hapana. Wengine wamelazimisha kuahidi vitu ambavyo hawawezi hata kuvilipa eti kwa kushindwa tu kusema hapana. Ndugu, kama kitu huna uwezo nacho sema nashukuru kwa kuniamini na kunishirikisha kitu hiki lakini kwa sasa sitaweza kwasababu 1,2,3 hivyo naomba tufanye wakati mwingine.
5.
KUTOKUWA NA ELIMU YA FEDHA.
Pamoja na kwamba karibuni kila kitu kinatumia na kinahitaji
fedha katika dunia ya leo, lakini ajabu ni kwamba elimu ya fedha bado
haifundishwi mashuleni na hata vyuoni hili limepelekea watu wengi kuwa wajinga
wa fedha yaani hawajui usahihi na nini wafanye ili kuzalisha pesa,kutunza fedha
na kuwekeza fedha kwa kukosa elimu hii watu wamekuwa wahanga wa uchumi na
kushindwa kuyaendesha maisha yao kwa vipato vyao badala yake wanakimbilia
kwenye mikopo na kuzalisha madeni ya kuwatosha.
6. UNUNUZI WA VITU HOLELA (SHOPAHOLIC)
Ulisha wahi kuona mtu yeye kila kitu akikutana nacho
kinauzwa tu atatamani kununua wakati huohuo hata kama ni pipi hata kama yeye ni
wa kiume zikapita nguo za kike zinauzwa atatamani tu anunue akampe hata mtoto
wa binamu yake ,kitu hichi ndicho kinaitwa SHOPAHOLIC yaani, ulevi wa kununua
vitu bila mipangilio. Hawa watu pesa inakuwa kama inawawasha na hawawezi kutulia
na pesa na utawajua tu wakiwa na pesa hawezi kutulia watakuwa bize kweli kweli
ni mwendo wa kukupungia mkono tu kwa mbali anapotea ,akimaliza pesa sasa
anakuwa mpole sana tena mdogo kama pilitoni hahahaha.
Kama na wewe ni mmoja wao nikushauri uweke budget ya matumizi ya pesa zako kabla ya
kuzitumia na kama pia unaweza kuwa unatembea na pesa ya kukutosha tu kwa
wakati huo ili kuepuka tamaa na vishawishi wa pesa.
kwa uchache hizi ndizo baadhi ya sababu ambazo watu wengi zimekuwa zikiwa vuta na kuwaweka katika madeni makubwa na yasiyo lipika pasipo hata wao kujua. zifahamu sababu hizi kwa undani kisha uziepuke ili usiwe mmoja wao wanaoteswa na kulizwa na madeni kila kukicha.
naamini umejifunza kitu na mungu akubariki sana.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa mtandao wa addvaluetz karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;Sim na Whatsapp >>+255783327456 / +255767653697.
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu,niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Jacob · 104 weeks ago
Migongo · 104 weeks ago
Abel Banene · 93 weeks ago
Elias Migongo · 93 weeks ago
Ayusto Busanda · 93 weeks ago
Migongo Elias · 93 weeks ago
Jaredy Naftali · 93 weeks ago
Migongo Elias · 93 weeks ago
Gchyo · 93 weeks ago
Elias · 93 weeks ago
Jacob · 93 weeks ago