MAAJABU YA AKIBA

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.
“Sometimes your joy is the source
of your smile, but sometimes your smile can be the source of your joy.” Wakati
mwingine furaha yako ni chanzo cha tabasamu lako, lakini pia tabasamu lako linaweza
kuwa chanzo cha furaha yako. Tunaishi kwenye dunia ambayo watu wamevurugwa na
maisha, huku wakiwa bize au sirious na maisha yao. kana kwamba kuona tabasamu na furaha yao
imekuwa ni adimu sana. kwa kawaida tabasamu na kucheka huwa ni viashiria vionekanavyo
katika kuonyesha au kuashiria furaha, licha ya kuwa vipo viashiria vingine lakini
tabasamu na kicheko hutafsirika mapema kama viashiria vya furaha. Wakati mwingine
mtu anaweza akacheka na kutabasamu lakini akawa na machungu ndani yake goja
tuachane nayo leo hii.
Tafti zinaonyesha kuwa mtoto mdogo mwenye umri wa miaka
4-6 hucheka mara 300-400 kwa siku huku mtu mzima hucheka mara 15 tu kwa siku
huu ni utafri ambao haujathibitishwa. Lakini kilichothibitishwa ni kwamba
kucheka na kutabasamu kunaimarisha maisha yako, afya yako, hali ya ubongo wako
na hata ubunifu wako. Pamoja na kwamba kunawatu hucheka na kutabasamu kwa
musimu yaani mara chache sana watu hawa ni tofauti sana na watu wanaocheka na
kutabasamu mara kwa mara. Kwani huwa ni wepesi wa kusongwa na msongo wa mawazo
wakati mwingine hata ugumu wa maisha ingawaje hawezi kusema, hii ni sawa na
sumu ndani ya mtu ambayo kiafya siyo nzuri.
Tabasamu
kadiri unavyoweza hata kama hauna sababu ya kutabasamu we tabasamu tu, kwani
unapotabasamu unapeleka taarifa chanya kwenye ubongo wako ambayo huimarisha
utendaji kazi wa ubongo na kuleta furaha zaidi. Kitu kama hichi Marc Reklau amewahi
kusema “When you smile your entire body sends out the message
“Life is great” to the world.” Tafsiri yake ni kwamba unapo tabasamu mwili
wako unapeleka ujumbe “Maisha ni mkuu” kwenye dunia.
Vitu ambavyo huvijui kuhusu kutabasamu ni kwamba;
1.
Ukitabasamu unachilia homoni ya serotonin
(ambayo hutufanya tujisikia vizuri). Ndiyo maana mtu akitabasamu anaonekana
hanashida wala changamoto.
2.
Ukitabasamu unaachilia homoni ya endorphins (ambayo hupunguza maumivu). Hii
humfanya mtu asahau matatizo na kutua mzigo wa shida zake huku akifurahi na
kuondoa stress. Hivi ulisha wahi kuvurugwa ukajisikia maumivu ndani yako, na
ukaenda kuangalia hata comedy? Utashangaa kuona unaanza kucheka na kusahau
kabisa maumivu yale hii ni kuwepo kwa homoni hii.
3. Hupunguza mganzamizo wa damu(blood presure). Hii ni kutoka na na kuwepo kwa homoni hizo hapo juu ambazo husaidia kuondosha stress.
4.
Huongeza ufanisi wa utendaji kazi wa kinga ya
mwili
5.
Humfanya mtu kuonekana
hana shida wala changamoto za maisha.
6.
Humfanya mtu kuonekana
mwepesi kufikika na kubadilishana mawazo nae. Watu
wa aina hii ni tofauti kabisa na wale wenye kuwa serious muda wote kwani huogopeka
sana.
Wana saikolojia husema kuwa tabasamu ni moja ya njia muhimu sana za kuongeza mvuto na ushawishi wa mtu kwa watu wanao mzunguka, aidha wawe ni wale wanaomfahamu au wasio mfahamu lakini pindi atakapo tabasamu huonekana kama wanafahamiana kabisa. Unaweza kufanya hivyo pindi unapokutana na watu hata ambao hujawahi kukutana nao utashangaa kuona nao wanavyo tabasamu.
Kutabasamu au kucheka siyo lazima na wala mtu asipo tabasamu wala kucheka atakufa hapana! Kutokana na faida hapo juu na nyingine lukuki ambazo hatujazijadili hapa unaweza kuchagua kutabasamu. Kwani hakuna gharama yeyote inayohitajika ili kutabasamu, pili unapotabasamu unayapa thamani na maana maisha yako. Kama ni hivyo kwanini usichague kutabasamu na kufurahi hivi kutabasamu na kucheka ni shingapi kwani?
Na kama hujawahi kutabasamu wala hujazoea kabisa unaweza kuanza kutabasamu mara nyingi kadiri unavyo weza napo fanya hivyo kwa kutumia kioo chako kisha jitazame kabla hujatabasamu. Halafu tabasamu huku ukiwa umejitazama kwa kioo hapo utachagua yule wa kwanza kabla ya kutabasamu na yule wa pili baada ya kutabasamu ni yupi amekaa poa? Kisha fanya hivyo mara kwa mara kila siku.
Pamoja na hayo kuna mahali pa kutabasamu, kucheka na kufurahi na siyo kila sehemu na kila wakati na kwa kila mtu inatakiwa utabasamu. Onyesha kufurahi lakini tambua kuwa kila jambu na wakati wake.
Najua hujatoka kama ulivyo ingia hivyo ulicho kipata anza kukifanyia kazi na kile hujakipenda achana nacho hicho siyo chako.
Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza
kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya
kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano
hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT
lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS
Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na
Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluenetwork.
Karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Instagram>>migongo_elias.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi
kujifunza pamoja nawe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Suzan Phares · 84 weeks ago
Elias · 84 weeks ago
Ezron · 84 weeks ago
Migongo · 84 weeks ago
Chy · 84 weeks ago
Elias · 84 weeks ago
Gody · 84 weeks ago
Nuru · 84 weeks ago
Migongo · 84 weeks ago
Japhary Seth · 84 weeks ago
Elias · 84 weeks ago
Elisha W Ndidi · 83 weeks ago
Hatua Funzo
Migongo · 78 weeks ago
Timotheo · 53 weeks ago
Elias · 50 weeks ago
Trice · 48 weeks ago
Migongo Elias · 48 weeks ago
Mosest · 47 weeks ago
Migongo · 40 weeks ago
Mhenga bf · 40 weeks ago
Elias · 40 weeks ago
Rachel gakay · 32 weeks ago
Cheyo · 32 weeks ago