GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.
- Get link
- Other Apps
GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOTAKA.
“Ukiona vya elea,
ujue vimeundwa.” “Hakuna vya bure duniani.” “Mkono mtupu haulambwi.” Hizi ni baadhi ya kauli ambazo zimeenea karibia
kila kona ya dunia. Na lengo lake si kutukomoa au kutusema vibaya, laah hasha! Bali
ni kutaka kutuonyesha kuwa katika
kuyafikia mafanikio tunayoyataka ni lazima tulipe gharama. Kumekuwa na kasumba
ya watu wengi sana kutamanani mafanikio makubwa na kufika mbali sana katika
maisha yao. Lakini pamoja na kutamani huko, asilimia kubwa ya watu bado
kuufikia ukuu wanao utaka imekuwa ni gumuzo mtaani.
Watu wengi wanatamani sana mafanikio ya baadhi ya watu maarufu
na waliofanikiwa katika maisha yao au kutimiza ndoto zao. Na hapa wengi
wamekuwa wadau na wapambe wa mafanikio ya watu waliofanya vizuri kwa nafasi zao.
Wakati huo, huwa wanaona kama watu wengine wanabahati, wamezaliwa na na neema
kuliko watu wengine, na mara nyingi wameyachukulia maisha kuwa ni simpo sana.
watu wa namna hii, huchukulia mafanikio ni kitendo cha siku moja. Hayo yote sikatai lakini, ni muhimu tufahamu
kuwa mambo huwa hayatokei yenyewe tu kama wengi tunavyodhani. Ni lazima uyafanye
yatokee yaani, you must make them happen.
Kunaupande mmoja wa shilingi ambao watu wengi linapokuja
suala la mafanikio huwa wanasahau kabisa kuuzungumzia. Na upande huo ni ulipaji
wa gharama juu ya ndoto na malengo yetu katika kuyafikia. Na gharama utakayo
kuwa tayari kuilipa ndiyo itaonyesha ni matokeo kiasi gani unakwenda kuyapata. Wengi
tunamfahamu Yesu kuwa alikuwa ni mtenda miujiza
lakini nyuma ya kutenda miujiza hiyo ni wachache waliofahamu siri na gharama
zake. Ambapo wakati mwengine ilimlazimu kufunga, kukesha, kuomba, na mengine
kibao ili kufanya miujiza hiyo, kitu ambacho wengi wanataka tu kuona matokeo
lakini hawataki kabisa kuufuata mchakato wa kuufikia ukuu wenyewe.
Hapa nimekuuandalia gharama tano unazopaswa kuzilipa
katika kuufikia ukuu unao utaka katika maisha yako. Gharama hizi pia,
zimezungumzwa na waandishi mbali mbali akiwemo Godius
Rweyongeza katika kitabu cha jinsi ya kufikia ndoto zako. Na wewe, ni muhimu
kuzifahamu ili uanze kuzichukua mapema. Gharama hizi ni pamoja na;
Ya kwanza ni:
Gharama ya kujifunza. Ni kweli
watu wanatamani sana kufanikiwa katika maeneo mbali mbali pendwa ya maisha yao.
Lakini ajabu ni kuwa, watu hawa hawako tayari kabisa kulipa gharama ya kujifunza. Kunamsemo mmoja naupenda nao
unasema “Continous learning is the minimum requrement
of success in any field ”
Yaani, “kujifunza kwa mwendelezo ni hitaji la chini la mafanikio
katika eneo lolote”. Hiii ni sawa na kusema, kama unataka uwe mfanyabiashara bora
jifunze zaidi kuhusu biashara, kama unataka uwe mtaalamu wa afya jifunze zaidi
kuhusu afya, vivyo hivyo kwa wachezaji, waimbaji, mainjinia, n.k. na hapo
waweza kuweka mkakati wa kujifunza kitu kipya kila siku katika eneo husika
utashangaa utakavyo kuwa mbobevu katika eneo hilo.
Ya pili ni:
Gharama ya kuacha baadhi ya vitu. Hapa
ni pagumu kidogo, kunanamna mtu anakuwa anatamani kuwa mtu fulani hivi lakini,
jinsi anaishi sasa ni tofauti kabisa. Kitu hiki kimefanya watu kuwa na tabia
nyingi sana ambazo zinawasaliti kuuelekea ukuu wao. Kunausemi maarufu katika
eneo hili nao unasema “inorder to get into something new you will have to get
out from something old else well” yaani, “ilikuingia kwenye kitu kipya
ni lazima utoke kwenye kitu cha zamani pia”. Kunatabia, marafiki, au wakati
mwengine ni vitu pendwa kwako vitakubidi uvitoe ili kuufikia ukuu unaotaka. Mfano
ukitaka uishi chini ya pato lako kunatabia, marafiki au vitu itakubidi uachana
navyo kwanza mf. Tabia ya ulevi, ununuzi vitu holela n.k. yaani kiufupi
kufanya maajabu ni kufanya vitu tofauti na wengine.
Ya tatu ni:
Gharama ya fedha. Nikili
tu kusema kuwa, gharama hii watu wengi wanaifahanu sana. Sema ni vile tu watu
wanaamini kuwa kunasiku moja mambo yatajipa yenyewe tu. Ukweli ni kwamba,
kunawakati ndoto yako itakuhitaji ulipie gharama ya fedha kama kulipia mafunzo,
waalimu, mtaji na vitu vingine husika. Watu wengi hawako tayari kuilipa gharama
hii, huku wakitegemea kuamka mambo yametiki yenyewe. Hapa ni kuambia tu ndugu
yangu utasubiri sana na pengine huenda ukaenda kuyanufaisha makaburi
Ya nne ni:
Gharama ya muda. Gharama
hii pia inajulikana na watu wengi, sema watu wengi ukiongea nao huonekana kuwa bize
sana hata kwa mambo ambayo hayako bize. Uzuri ni kwamba, watu wote hupewa saa
24 kwa siku, shida inakuja kwenye namna ya kuzitumia saa24 hizo na kuweka vipaumbele.
Wengi hulalama na kudai kuwa hawana muda wa kutosha. Huku ni kukwepa majukumu
yao waziwazi. Ifahamu ndoto yako, tambua na fahamu ni muda kiasi gani unautenga
kwaajili ya ndoto yako kisha, fanyia kazi kila siku. Usianze kulalamika kama
wengine wafanyavyo.
Ya tano ni:
Gharama ya kuchukua hatua ya kufanyia kazi. Pamoja
na kuwa baadhi ya wengi kufahamu wao ni akina nani katika safari ya mafanikio
yao. Kufahamu wanakoelekea, mikakati na njia za kuelekea huko. Lakini bado
wengi suala la kuchukua hatu ya kufanyia kazi bado ni tatizo. Tunajua umefundishwa
kwenye semina, kanisani, nyumbani, na sehemu zingine kwamba yapi yakupasayo kutenda
lakini kuchukua hatua na kutenda bado ni kimbembe kwa waswahili wengi. Hata hivyo, kama unataka
kuufikia ukuu unao utaka hakuna namna ukafanya kazi tena kwa bidiii, yakupasayo
kutenda. Si unajua matendo yanasauti kuliko hata maneno yenyewe.
Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza
kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine
namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa
moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO
ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha.
Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz. Karibu
sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697
/+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu,
niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe
- Get link
- Other Apps