MAAJABU YA AKIBA

Kuna njia nyingi sana tumeambiwa
na kufundishwa kwa namna tofautitofauti sana ilikupambana na maisha yetu hasa
katika kuyafikia malengo na mafanikio yetu.na kwa bahati nzuri au mbaya njia hizo
zimekuwa zikiwasaidia wengi na wengine kuwahalibia kabisa na wengine kuwaboresha
huku wengine zikiwabomoa kabisa .kiuhalisia hakuna njia ambayo imethibitishwa
na kutumika kuwa ni njia bora kwa 100% ambayo inaleta mafanikio kwa watu wote
kwa kweli bado sijaona.kwasababu njia ambayo ilimfanikisha John akiitumia Anna
kwa namna ileile inaweza kumfilisi na kumharibia kabisa,njia iliyo mfilisi Huyu
ndiyo itakayo mfanikisha yule.Unaweza ukaambiwa weka malengo,amka mapema ,weka vipa
umbele,fanya kazi kwa bidii,fanya mambo kwa utofauti,fanya kwa ubora,jifunze
vitu vipya kila siku ,ajabu ni kwamba unaweza kufanya yote hayo na ukapata
matokeo tofauti kabisa na ulivyo tarajia sababu zipo nyingi sana naomba
tutaelezana wakati mwingine lakini leo
wacha nikupe hii kwanza.
Pamoja na kwamba hakuna njia
ambayo kwa 100% inaleta matoke sawa kwa wote leo nataka nikufundishe njia na
kanuni moja ambayo ukiitumia kikamilifu na kwa uaminifu matokeo mazuri utayapata naamini utanipenda.Kanuni hii
imezunguzwa na waandishi kadhaa akiwemo Amos Mwanasaikolojia na mtaalamu wa
elimu maalumu.
Na katika kanuni hii
nazungumza na mtu ambaye tayari ana malengo na Ndoto zake yaani kiufupi anajua
yeye ni nani na anataka kuwa nani .lakini kama wewe huna malengo na hujui
unataka kuwa nani mwongozo unakuja siku si nyingi au kwa kuharakisha waweza
kuwasiliana na mimi moja kwa moja naamini nitakusaidia sana kwani wengi
wemeripoti kusaika sana. kanuni hii imegawanyika katika sehemu kuu nne kama
nilivyo ielezea hapa chini .
a)
KUANGUKA:
Katika safari ya kuyaendea mafanikio yako kuna njia
itabidi uipitie na njia hii si nyepesi kama unavyo dhani kwani kuna misukosuko na
changamoto lukuki sana ambazo zitakutaka kukata tamaa,kurudi nyuma ,kujihisi
huwezi wala husitahili na lengo ni kukufanya usiishi ndoto yako.hizo ni pamoja
na maneno ya watu,kufeli,kukosa mtaji,kukosa msaada na mengine mengi.kwa
vyovyote vile utaanguka na kufeli mara kadhaa ,nataka kukwambia hii ni sehemu
ya maisha na ni hatua muhimu sana katika kuya fikia mafanikio yako kwani hata
unao waona wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa hawakuanza juu moja kwa moja na
kufika hapo walipo kwa mbahati mbaya
bali walianguka mara nyingi sana wakapalangana hadi kufikia hapo walipo leo.yaani
hakuna namna ukakwepa kufanya makosa hapa dunia kikubwa tu usikate tamaa . kwani
“makosa yanatuongezea uzoefu na uzoefu
unatupunguzia makosa hivyo usiogope kufanya makosa”.
Kunamsemo mmoja maarufiu sana
nao unasema “kama hautajifunza kutokana
na makosa/matatizo unayokutana nayo basi utateseka na tatizo moja miaka nenda
miaka rudi”.watu wengi wamekuwa na tabia mbaya ya kulaumu na kulalamikia
sana matatizo yanapokuja ,ndugu naomba kukutaarifu kuwa matatizo unayokutana nayo
yanakuwa yamebeba tahadhari na ujumbe maalumu kwaajili yako.kubwa Zaidi ni
kukufundisha kuwa njia hii siyo sahihi hivyo ukipuuzia na kuona kuwa ni upuuzi
hutojifunza chochote na badala yake utakuwa ni mtu wa kulalamika kwa kila gumu
unalo pitia ,hii itapelekea kuteseka na changamoto hiyohiyo kila wakati.Hivyo penda
kujiuliza kwanini hili limenitokea na je nimejifunza nini kutoka katika
hili.yaani “failure teaching us a way by
showing us which isn’t the way” makosa yanatufundisha njia kwa kutuonyesha
njia gani siyo sawa.
c)
INUKA:
Kwasababu kila changamoto na gumu unalopitia linalo funzo
na ujumbe maalumu kwaajili yako hivyo jitahidi kupata ujumbe na kujifunza
kutokana na ujumbe huo na kisha chukua hatua kwa kuinuka na kuanza tena kwa
kasi mpya ,ari mpya na nguvu mpya.kosa ambalo hutakiwi kulifanya ni kuanza upya
pasipo kupata funzo kwa kilicho kuangusha ukifanya hivyo utalia na kitu kimoja
siku zote za maisha yako.jiulize kitu gani kimenifanya nishindwe kupata nilicho
kitarajia kisha kitafute chukua hatua ya kujifunza kwa watu waliofanikiwa,jifunze
mtandaoni na jifunze kwa kusoma vitabu kisha pata ufumbuzi na anza upya .kuanguka
siyo shida shida ni kubaki umelala pasipo kuanza upya .rafiki anza anza anza
anza inawezekana tena.
d)
SONGA
MBELE:
Moja ya kitu muhimu unapaswa
kukifanyia kazi na kuwa sehemu ya maisha yako ni kusonga mbele yaani kuwa na mwendelezo
pale ulipo ishia waingeleza wanasema consistency.
kuendelea kufanya kazi kila siku bila kukata tamaa hata kama matokeo hayaji
kama ulivyo kusudia kwani utakutana na vitu vingi sana vya kukurudisha nyuma
usikubali kukata tamaa.endelea kufanya kazi na ufanyia kazi kila mara.Inawezekana
na hapa inatakiwa uwe mtu wa kujifunza kila kukicha kwani ubongo wetu
unahitajika kuoshwa na kusafishwa kila siku ili uwe na afya bora kama ilivyo
miili yetu vinginevyo kusonga mbele itakuwa ni tatizo kubwa kwako.
Naamini umejifunza kitu ni furaha
yangu kuona umesaidika katika hili na kuona ukisonga mbele katika maisha yako.
Hivyo katika safari ya kuyafikia mafanikio yako utakutana na
magumu,makosa,changamoto nyingi sana ili zikurudishe nyuma na pengine utaanguka
mara kwa mara tena hata mara nyingi sana ,kama ni ndoto yako kweli nakusihi
usikubali kubaki umeanguka hakikisha unajifunza kwa changamoto hiyo kisah anza
upya tena inuka kwa kasi mpya,ari mpya na nguvu mpya rafiki! usikate tamaa hadi
itokee mwisho kabisa kuwa mtu wa kuendelea mbele kila siku songa mbele pambana
kila siku uwe bora kuliko jana utatoboa .
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala
hii imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa
Saikolojia,Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa
mtandao wa addvaluetz karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa
mawasiliano;
Sim
na Whatsapp >>+255783327456 / +255767653697.
Email>>
eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>>
MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama
umejifunza kitu,niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe.
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.