MAAJABU YA AKIBA

Image
MAAJABU YA AKIBA Akiba (saving) ni kiasi cha fedha au rasilimali ambacho kimewekwa kwa matumizi ya baadaye, hata sasa kingeweza kutumika lakini umuhimu wake kwa kutumika baadaye ni mkubwa kuliko matumizi yake ya sasa. Hata katika biblia ``Mwanzo 41:35-36`` kama umewahi soma utaona Farao baada ya kutafsiriwa ndoto yake na kufahamu kuwa, imempasa kuweka akiba alilifanya hilo kwa uharaka ili kuhakikisha linaendelea vizuri ndio akamweka Yusufu kama msimamizi wa hili. Farao aliona kabisa kuwa nidhamu yake ya kujiwekea akiba haipo sawa hivo alihitaji msaidizi wa kumsaidia kama yeye alivyokuwa ndivyo tulivyo baadhi yetu siku za leo hatuwezi kujiwekea akiba ya vile tulivyo navyo. yaani huwa tunapenda kusema kesho itajisumbukia yenyewe,  Hata hivyo tangu zamani hata leo mataifa mbalimbali yamekuwa yakijiwekea akiba kwa manufaa na matumizi ya baadaye. Ukiangalia nabii Samweli alikuwa akijiwekea akiba na aliitoa pale Sauli alipomtembelea wakaila ile akiba ya chakula. Ni muhimu kujiw...

JINSI YA KUSEMA UKWELI NA KUWA MWAMINIFU

Siku Moja nilikuwa katika pitapita zangu nikasikia mtu akisema siku hizi kumpata mtu mkweli haiwezekani. Nilipouliza kinagaubaga akasema watu ni waongo sana, hakuna anayeweza kuongea ukweli wakati Wote na Uongo umekuwa ni sehemu ya Maisha yetu. Na akachimba zaidi akasema kama utachagua kuwa mkweli itakubidi utafute kadunia Kako ukaishi kivyako huko.

Ni kama kuna kaukweli Fulani hivi ukiangalia kadiri siku zinavyozidi kwenda watu wanazidi kupoteza UKWELI na UAMINIFU. Utashangaa mtu unamuuliza umefika wapi nipo hapa corner nakuja chapu,unakaa saa za kutosha hata hatokei kumbe bado yupo nyumbani kabisa.Mwingine anakwambia tutakutana saa 4:00 afu haonekani kabisa, mwingine anaenda kutoa sadaka hewa ili aonekane ametoa, yaani uongo umetapakaa Kila mahali UAMINIFU umekuwa bidhaa adimu sana. UKWELI umefichika umekuwa wa kumlika na tochi.

kuwaridhisha na kujionyesha kwa wengine ni moja ya kitu kinachopelekea kusambaa na kuenea kwa uongo kuliko UKWELI. Hiki kitu kimekuwa ni kilio Cha wengi sana.Kwani watu wengi huishi Maisha ya kuwaridhisha na kuwapendeza wengine.Wamekuwa wakifanya hivi wakijua wanajenga kwa kupendwa zaidi kumbe ndivyo wana bomoa kabisa .

TAMBUA kuwa huwezi kumridhisha au kumpendeza Kila mtu haiwezekani kwani"WATU HATUFANANI NA HATUWEZI KUFANANA" . Kwanza hata vitu tunavyo viamini vinatofautiana hivyo na mitazamo yetu lazima iwe tofauti ndiyo maana Unaweza kujitahidi kuwa mwema sana kumbe mtu mwingine anaona kama unajipendekeza unaweza ukafanya kitu kizuri sana kwa mtu huyu kumbe ukamuuzi tena huyu. Ndiyo maana rafiki yangu Julian aliwahi kusema "ukitaka kuwapendeza Wote basi jiandae kuwaudhi Wote". 

Sababu nyingine ni kushindwa kusema HAPANA . Zoezi hili kimekuwa gumu na changamoto kwa baadhi ya watu waliowengi kwa hii Dunia. Na wengi wamekuwa wakifanya hivi ili wakubarike na kuwafurahisha wengine yaani mtu anaogopa kukataa eti watu watamchukia.Wamekuwa watu wa kukubali Kila kitu matokeo yake wamejikuta wakiweka ugomvi wa kudumu badala ya kuaminiwa wamechukiwa sana. Mfano unajikuta mtu ni MC labda anatenda ijumaa na watu wanamfahamu yupo vizuri kwa kazi hiyo anakuja mteja mwingine anahitaji huduma yake ijumaa hiyohiyo sasa ili asionekane amemwangusha anakubali na mtu wa tatu vivyo hivyo matokeo yake anakuja kugonganisha kazi na anaharibu UAMINIFU wake kwa Wote.

Hivi ulisha wahi kufanya appointment na baadhi ya mafundi wa nguo?, Au basi mafundi selemara je? Na mafundi viatu vipi? Nimekutana na watu wengi wanawalalamikia sana Hawa jamaa kwa habari ya UAMINIFU na UKWELI wa kazi yao . Ubaya wa haya maneno unaweza ukayakwepa kuyatumia ukazani unajenga kumbe unabomoa .
Ndugu yangu nipende kukwambia kwamba pamoja na gubiko kubwa la uongo waaminifu na wakweli wapo sana na Mimi nikiwepo miongoni mwao. Na ukitaka kuishi Maisha ya UKWELI na UAMINIFU ishi Maisha yako mwenyewe yaani usiige Maisha ya watu, usiishi kuwalidhisha watu, jifunze kusema HAPANA. Kitu kama kipo nje ya uwezo wako sema tu UKWELI harafu Kusema HAPANA siyo dhambi eti!.Kubwa jifunze kusema HAPANA kwa heshima bila kuwaudhi wengine.Kuna msemo mmoja husema "Honesty is a very expensive gift,don't expect it from cheap people" kwamba UAMINIFU ni dhawadi ghari sana na usitegemee kuipata kutoka kwa watu wa kawaida. Ni kweli UAMINIFU na UKWELI ni adimu hebu isiwe kwako . Na kubwa zaidi ni kwamba usiwaamini watu kupitiliza. Jiamini mwenyewe ishi Maisha yako halisi yaani ishi wewe kama wewe.usibadilishe uhalisia wako kwasababu ya mazingira au changamoto Fulani acha watu wakujue wewe kama wewe hata katika shida na raha hapo utakuwa umemaliza asee. 

Nimalize kwa kusema "HONESTY AND TRUTH ARE THE BEST POLICIES" Yaani UAMINIFU na UKWELI ni sera Bora.
Ishi Maisha ya UKWELI chagua UAMINIFU unalipa sana rafiki . 

SeE yOu NeXt LeVeL!

Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia,Uchumi na Maisha.  Mwanzilishi na Mwendeshaji wa   mtandao wa https://addvaluetz.blogspot.com karibu sana ujiongezee thamani yako. 

Kwa mawasiliano;

Whatsapp/Sim >>+255767653697 / +255783327456.

Email>> eliasmigongo120@gmail.com.

Facebook>> MIGONGO ELIAS.

LinkedIn>>Migongoe. 

Pinterest>>eliasmigongo.

Kama umejifunza kitu,niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe. 



Comments (2)

Loading... Logging you in...
  • Logged in as
Elisha ndidi's avatar

Elisha ndidi · 42 weeks ago

Nashukuru sana hakika nimeongeza thamani Sina budi kudumisha na kuboresha hili ili niwe na matokeo Bora yasiyobadirika kwa watu.
Elias Migongo's avatar

Elias Migongo · 42 weeks ago

Leaving testimony nzuri

Post a new comment

Comments by

Popular posts from this blog

NJIA 7 ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.