MAAJABU YA AKIBA

Siku zote ukiishi katika dunia hii kila kukicha utakutanana
na migogoro na matatizo ya kutosha.Yaani, ukikwepa upande huu utakutananayo tu
upande wa pili. Kumbe matatizo katika dunia hii ni sehemu ya maisha. watu wengi
hawakubaliani na ukweli huu matokeo yake matatizo yamekuwa yakiwashangaza kila
leo. Nimewahi kukutana na usemi mmoja ambao sina budi kukujuza nawewe leo. Nao ni huu “kuishi duniani huku ukitegemea
kuishi bila matatizo ni chanzo cha matatizo yote.”, kuna watu wana amini kuwa
wao hawajaumbwa kukutana na matatizo yeyote hapa duniani, hapo utakuta mtu
anasema “hivi kwanini mimi tu Mungu yanipate haya ”. Ajabu kweli yaani
matatizo anataka yawapate watu wengine tu ila yeye hapana, ndugu ilihali unakaa kwa
hii dunia hiki kitu ni ngumu kukikwepa asee.
Ndugu yangu kama unakaa kwenye hii dunia matatizo yatakuja
tu aidha upende au usipende, uwe mwema au mbaya kiasi gani ,mcha Mungu au muovu
kiasi gani, uwe tajiri au uwe masikini, uwe mchapa kazi au uwe mvivu, matatizo yatakuja
tu na kila mtu anamatatizo yake. Hapa namaanisha hakuna mtu asiyekuwa na
matatizo ingawaje matatizo yanatofautiana baina ya mtu na mtu, ndiyo maana linaweza kuwa ni tatizo kwa mtu y lakini kwa mtu x wala! Kitu kikubwa hapa ni kukubali kuwa matati hapa duniani hayakwepeki na
ni sehemu ya maisha baada ya kukubali
kisha ni kujua njia gani nzuri ya kukabiliana nayo na kuchukua hatua ilikupambana
nayo haraka iwezekanavyo, vinginevyo utapata maumivu ya kudumu na yasiyoisha
kabisa.
NJIA
RAHISI ZA KUKABILIANA NA TATIZO LOLOTE KATIKA MAISHA YAKO.
1.
LIFAHAMU
TATIZO LENYEWE.
Hata
katika mapambano ya kivita au mapambano
yeyote yale mfano vita, mpira, mbio, ngumi n.k kumfahamu tu adui yako uimara na
udhaifu wake utakuta umeukaribia ushindi wako kwa 50% .Msemo huu wazungu
huusema kuwa” knowing your enemy your
about to win the battle”. yaani, kumfahamtu adui yako ni kuukalibia
ushindi. Rafiki fanya namna yeyote ulifahamu tatizo lako kabla ya kusonga mbele
kupambana nalo vinginevyo utatia aibu kubwa sana . Hapo ni sawa na kukimbiza
upepo. Kwa mfano wewe ni mfanyakazi umeajiliwa unaingia ofisin upo na mgogoro wa mara
kwa mara na boss wako, badala ya kuamua kuacha kazi au kumkimbia boss
ilikuepuka migogoro na boss wako hapo cha kufanya fahamu
kwanza shida iko wapi. Utakuja kugundua kuwa upo kwenye mgogoro wa kutukannwa na kufokewa sana
na boss wako, na hili ndilo tatizo lenyewe sasa.
2.
TAMBUA
CHANZO CHA TATIZO.
Hii
ni hatua ya pili baada ya kugundua tatizo lako ni nini,na hapa lazima ufahamu
kwa kina chimbuko au chanzo cha tatizo lako.kuna msemo mmoja unasewma” kutatua tatizo bila kujua chanzo chake ni
chanzo cha matatizo yote “.Ili utatue tatizo lako kwa urahisi ni lazima
ufahamu kitu gani kilichopelekea kuwepo kwa tatizo lako au chanzo chake ni kipi
hasa.Mfano katika tatizo letu hapo juu la migogoro wa kufokewa na boss wako ni
lazima ujiulize chanzo cha mgogoro wa
kufokewa na kutukanwa huu ni nini hasa?. kwa mfano unaweza kugundua kuwa chanzo
chake ni kufanya kazi chini ya kiwango hiki ndicho chanzo chenyewe cha tatizo lako
.hivyo kwa kufahamu kuwa upo na mgogoro wa kufokewa na boss wako hilo ni tatizo
tayari na kufahamu chanzo cha mgogoro huo ambao ni kufanya kazi chini ya
kiwango au kuchelewa kazini hapo unakuwa umeshagundua tatizo na chanzo cha tatizo lako.
3.
FAHAMU
NJIA SAHIHI YA KUKABILIANA NA TATIZO LAKO.
Kufahamu
tatizo na chanzo chake ni hatua nzuri sana ya kuliendea na kulitatua tatizo
lako kitu kikubwa sasa ni kuhakikisha unatafuta njia nzuri na sahihi Zaidi itakayo
kusaidia kulitatua tatizo lako fanya hivi kwa kusoma vitabu na kufuatilia
tatizo lako katika mitandao ya kijamii kama vile geogle, fb, youtube n.k
au kuwauliza watu ambao unahisi ni sahihi kwako na unawaamini kuwauliza ili
kukupa ushauri na hatua zingine katika kutatua tatizo lako.angalizo katika hili
ni kwamba usishirikishe kila mtu tatizo lako.katika kupata ushauri kuna watu
wengine ni wanafiki wapo kufurahia kufeli kwako kwahiyo ukimpa nafasi katika
hili anakumaliza kabisa.Aidha si kila ushauri unapaswa kuufanyia kazi kwa maana
ushauri na maneno hutolewa bure lakini
kuwa makini kuchukua ule unao kufaa tu. Ndiyo maana raisi Kiwete wa awamu
ya nne Tanzania amewahi “kusema akili za
kuambiwa changanya na za kwako”.
Nimalizie kusema unapochagua njia bora ya kutatua tatizo lako jitahidi uwe na machaguo mengi zaidi ya njia moja na ugundue uzuri na ubaya wa kila njia ya kuliendea tatizo lako. Mfano katika tatizo letu hapo juu njia za kutatua tatizo Hilo zaweza kuwa, kuacha kazi, kumkimbia boss, kujiongezea maarifa na kubobea katika eneo husika. Mfano mwingine labda huna hela Hilo ni tatizo tayari na njia za kulitatua zinaweza kuwa, kwenda kuiba na kukaba, kwenda kutafuta kazi ya kufanya mfano kibarua, kutwa n.k, kuongeza vyazo vya kipata n.k
Sasa ukiangalia karibia katika kila tatizo Kuna chaguzi kibao za kulitatulia lakini, Hoja yangu hapo ni kuchagua njia iliyo bora zaidi. Siyo bora tu yaani bora zaidi, na hapo utakuwa umeupiga mwingi na Kama ni ng'ombe ushaila yote kasoro tu mkia na mkia wenyewe ndo unaofuata hapo.
4. FANYIA KAZI NJIA BORA KUTATUA TATIZO LAKO.
Kufahamu tatizo na njia ya kulitatua ni jambo moja, kuifanyia kazi njia hiyo katika kulitatua tatizo lako ni jambo lingine kabisa . Hoja ni kwamba watu wengi wanaojua njia sahihi hasa za kuleta mabadiliko katika maisha yao wengi wao hawazifanyii kazi kabisa na hali wakitegemea matokeo tofauti , hili nalo ni tatizo haswaa. Ndugu yangu utekelezaji “implementation”ni hatua muhimu sana katika kuleta mabadiliko yoyote unayo yataka hapa duniani hata kama yawe ni mabaya au mazuri. Hivyo tafuta njia yako sahihi zaidi ya kutatua tatizo lako chukua hatua mara moja kuifanyia kazi ili kuleta matokeo ambayo unayahitaji katika maisha yako, na matokeo utayapata naamini utafurahia.SeE yOu NeXt LeVeL!
Makala
hii imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa
Saikolojia,Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa
mtandao wa Add ADDVALUENETWORK. Karibu sana ujiongezee
thamani yako.
Kwa
mawasiliano;
Whatsapp/Sim >>+255767653697 / +255783327456.
Email>>
eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>>
MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama
umejifunza kitu,niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Jacob · 104 weeks ago
Migongo · 104 weeks ago
Lilian · 85 weeks ago
Elias · 85 weeks ago
Nyamtondo · 54 weeks ago
Elias · 54 weeks ago
Agnes Sebastian · 54 weeks ago
Migongo Elias · 54 weeks ago
Nesta · 54 weeks ago
Migongo Elias · 53 weeks ago
Gcheyo · 54 weeks ago
Elias Migongo · 54 weeks ago
Eric janiary · 54 weeks ago
Elias Migongo · 54 weeks ago