P2. WATU WENGI WANATAFUTA PESA NA KUSAHAU KITU HIKI MUHIMU SANA.

 


P2. WATU WENGI WANATAFUTA PESA NA KUSAHAU KITU HIKI MUHIMU SANA.


Watu wengi wanapozungumzia mafanikio mara nyingi  hujikita kwenye vitu kama: pesa, biashara,
elimu, assets au connections.
Lakini kuna kitu muhimu sana ambacho wengi hukipuuzia ambacho ni AFYA YA MWILI BOSS.

Hata hivyo ukweli ni kwamba: Huwezi kuwa na maisha makubwa ukiwa na mwili dhaifu legelege mwili ulio katika duni na dhaifu.

Unajua kwa nini boss?
Simple ni kwa sababu: mwili wako ndiyo unafanya kazi kama gari la ndoto zako boss.
Na kama unavyojua tu gari likiwa na matatizo mfano likapata pancha, likamalizq mafuta likakata spring au shida yeyote tu, safari yote inakuwa ngumu na huendq ukafika kwa kuchelewa au usifike kabisa uendako boss.

BOSS KUNASOMO NILIZUNGUMZA KUHUSU AKILI NA MAARIFA.
MWILI NA AKILI VINAFANYA KAZI PAMOJA
Watu wengi hudhani afya ni suala la hospitali tu, kumbe ni zaidi ya hapo boss.
Elewa kuwa  afya ya mwili ni muhimu sana sababu inaathiri: namna unavyofikiri, maamuzi yako, energy yako, mood yako, furaha na productivity yako boss.

Ndugu Mwili wenye nguvu: Unasaidia akili kufanya kazi vizuri, Unaongeza umakini,
Unaongeza confidence,
na unakupa nguvu ya kupambana na changamoto za maisha boss.

Lakini kinyume chake nikweli MWILI DHAIFU : Huleta uchovu wa kila mara, uvivu, stress, kushuka kwa morali, kukosa kujiamini na wakati mwingine kukata tamaa kabisa tajiri.

Ndiyo maana nasema afya si anasa  ni msingi wa maisha bora kwa mtu makini.

MAZOEZI SI STAREHE NI UWEKEZAJI
Watu wengi wanaona mazoezi kama kitu cha watu wenye muda mwingi, wanamichezo, matajiri na watu fulani hivi walioshauriwa na daktari, hii siyo fair kabisa boss.

Ukweli ni kwamba: Mazoezi ni uwekezaji kwenye:
nguvu zako, akili yako, roho yako, mwili na maisha yako ya baadaye.

Kwasababu mazoezi: yanaongeza nguvu,
Yanaboresha afya ya akili,
Yanapunguza stress,
Yanaboresha usingizi,
na yanajenga nidhamu,
Hata dakika 20–30 kwa siku zinaweza kuleta mabadiliko makubwa sana katika maisha yako
.
Kumbuka Mwili usiofanya mazoezi huanza kudhoofika taratibu boss.

LISHE BORA = NGUVU BORA
Kila unachokula kinaathiri: mwili wako,
mood yako, na uwezo wako wa kufanya kazi.

Tatizo la wengi ni: kula ovyo, kula bila mpangilio, kula vitu vinavyoharibu afya kwa muda mrefu.

Nakumbuka siku moja Daktari mmoja aliwahi kusema kwamba, chakula kinaweza kuwa dawa au sumu kulingana na uchaguzi wako. Hii ni kweli ifike wakati tule ilikujenga miili yetu na si kula ilitusife.
Lakini pia, wili wako unahitaji: Maji ya kutosha,
Vyakula vya asili, Matunda na mboga, na lishe yenye uwiano

Boss Usisubiri kuumwa ndiyo uanze kuthamini afya yako.

USINGIZI WA KUTOSHA NI SILAHA YA UTENDAJI
Watu wengi wanadhani kulala ni kupoteza muda noo. Unapolala si kwamba umelala tu, bali  usingizi: hujenga upya mwili, huipa akili nafasi ya kupumzika, na huongeza uwezo wa kufikiri vizuri.

Lakini Ukikosa usingizi wa kutosha: akili huchoka, maamuzi yanaharibika, hasira huongezeka,  productivity hushuka

Hata hivyo Kupumzika si udhaifu. Ni sehemu ya performance nzuri ya mwili wako.

Ukweli wa chuma,
Watu wengi wanahangaika kutafuta pesa huku wakiharibu afya zao.
Halafu baadaye wanatumia pesa nyingi kutafuta afya waliyoiharibu. Soma tena.
Wewe Usifike huko boss.
Kwa sababu: Mafanikio bila afya hayana ladha boss.
Utajiri bila nguvu za kuufurahia hauna maana kubwa.

Kumbuka AFYA NI TABIA, SI TUKIO
Afya nzuri haitokani na: motivation ya siku moja,
au mazoezi ya wiki moja.
Inajengwa kupitia: consistency, discipline
na uchaguzi wa kila siku.

Kwa mfano mambo madogo tu kama:
kunywa maji vizuri, kutembea, kula vizuri, kulala mapema, kupunguza stress,
yakifanywa kila siku hujenga maisha yenye nguvu sana na tija boss.

To conclude,
Mwili wako ndiyo foundation ya ndoto zako zote.
Ukijenga: akili nzuri, fedha, mafanikio
lakini afya yako ikaanguka mambo mengi yataanza kupoteza maana katika maaisha yako

Linda afya yako kama unavyolinda future yako boss.
Kwa sababu: Mwili wenye nguvu unakupa nafasi kubwa ya kuishi maisha yenye nguvu.
Fanya hata mazoezi madogo,
Kunywa maji ya kutosha,
Punguza vitu vinavyoharibu afya yako,  Lala vizuri
Na anza kuutunza mwili wako kwa makusudi

Kumbuka: Afya bora si bahati — ni maamuzi ya kila siku.

#SeeYouNextLevel

Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.

Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026/05/anza-kufanya-haya-mapema-kabla.html

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork.
+255767653697. 

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29